Friday, March 23, 2018

CCM MANISPAA YA IRINGA YATUMIA ZAIDI YA MIL 18 KUTEKELEZA AHADI YA MBUNGE MSIGWA SOKO KUU

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Manispaa ya Iringa Said Rubeya akiongea na wananchi na wafanyabiashara wa soko kuu manispaa ya Iringa wakati wa kukabidhi televisheni tano aina ya Samsung, nne zikiwa za inchi 43 na moja ya Inchi 65, ving’amuzi na Sabu wufa ambazo matumizi yake katika pembe tofauti za soko hilo.
    Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Manispaa ya Iringa Said Rubeya akimkabidhi kiongozi wa wanyabishara hao televisheni tano aina ya Samsung, nne zikiwa za inchi 43 na moja ya Inchi 65, ving’amuzi na Sabu wufa
 Hii ni moja ya kati ya televisheni tano aina ya Samsung, nne zikiwa za inchi 43 na moja ya Inchi 65, ving’amuzi na Sabu wufa zilizotolewa na chama cha mapinduzi.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Iringa kimetumia zaidi ya Sh Milioni 18 katika kutekeleza ahadi ya Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka miwili tangu aitoe kwa wafanyabiashara wa Soko Kuu la Iringa mjini wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Kwenye moja ya mkutano wake wa hivi karibu alisema kuwa chama cha mapinduzi kimepeleka TV katika soko hilo hiyo atateleza ahadi yake kwa kupeleka TV kumi ambazo zitasambazwa katika maeneo mbalimbali ya soko hilo ambazo ziwawezeshe wafanyabiashara na wateja kufuatilia mambo mbalimbali yanayotokea ndani na nje ya nchini.

Akizungumza wakati wa kukabidhi TV hizo Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wa Manispaa Iringa Marko Mbanga alisema   walipoleta TV ya kwanza walipokea maombia ya kuomba kuongezewa TV hizo katika kwa kuwa soko hilo limegawanyika katika maeneo mbalimbali ambayo yote yanahitaji huduma ya kupata habari na matukio mengine yanayojiri nje na ndani ya nchi.

"Wakati tukikabidhi vifaa hivyo vya kutazamia matangazo ya ndani na nje ya nchi, wana jumuiya hao walituomba tuangalie uwezekano wa kuongeza Televisheni nyingine kwa kuzingatia ukubwa wa soko hilo ambalo limegawanyika sehemu mbili, la zamani na jipya," alisema.

Akiongea na wananchi pamoja na wafanyabiashara waliojitokeza katika soko hilo mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Iringa Said Rubeya alisema kuwa ahadi ya Mchungaji Msigwa imekuwa ahdai hewa hivyo chama cha mapinduzi CCM kimeamua kutekeleza ahadi kwa kutoa Televisheni nyingine tano aina ya Samsung, nne zikiwa za inchi 43 na moja ya Inchi 65, ving’amuzi na Sabu wufa ambazo matumizi yake katika pembe tofauti za soko hilo.

Rubeya alisema alisema kuwa mbunge huyo alitoa ahadi ya kutoa TV kumi kwa ajili ya soko hili hivyo wanampa muda wa mwezi mmoja kuahkikisha anatimiza ahadi yake la sivyo tutaleta Televisheni nne zilizobaki ili kumalizia ahdi za Mchungaji Msigwa na akishindwa tutajua namna ya kufanya kwasababu CCM tunawapenda.

Rubeya alisema chama cha mapinduzi kinawathamini na kuwajali watanzania na katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano, kinafanya kila linalowezekana kushughulikia changamoto mbalimbali za wananachi.

Alisema kuwepo kwa luninga katika soko hilo ni jambo muhimu kwa watanzania wote wanaotumia soko hilo kutoa na kupata huduma na ndio maana CCM ikasikia kilio hicho na kukifanyia kazi kwa kasi hiyo.

Pamoja na uzinduzi wa matumizi ya televisheni hizo, Rubeya alipokea kero mbalimbali za wafanyabiashara hao na kwa niaba ya chama chake aliahidi  kuzifanyia kazi, likiwemo ombi la kuziruhusu daladala kupita katika njia za soko hilo ili kuiweka huduma hiyo ya usafiri jirani na wateja na wafanyabiashara wa soko hilo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Miyomboni lilipo soko hilo, Mahazi Hepautwa alisema atapeleka ombi katika kikao cha baraza la madiwani ili muda wakufunga  biashara katika soko hilo uongezwe kutoka saa 12.00 jioni hadi saa 4.00 usiku. 

"Lengo ni kuboresha shughuli za utoaji huduma ya soko kwa wananchi. Tunataka kuona biashara katika soko hili zinakuwa kwa kuwaongezea wateja fursa ya kupata huduma zake," alisema.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More