Tuesday, March 20, 2018

MBEGU BORA YA MAHINDI YA WEMA 2109 KUWAONGEZEA TIJA WAKULIMA CHALINZE


Mkurugenzi wa Fedha wa Fedha na Utawala wa COSTECH, Shabani Hussein (wa pili kulia), akimkabidhi Mwenyekiti wa Kikundi cha Gezaulole, Ali Hussein Rajab (kulia), mbegu ya mahindi ya Wema 2109 katika uzinduzi wa shamba darasa uliofanyika leo katika Kata ya Msoga mkoani Pwani. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Jovin Bararata, Matifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu, na Ofisa Kilimo Mkoa wa Pwani Kapilima George. Mbegu hiyo imetolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB).

Mkulima wa  kutoka Kikundi cha Gezaulole kilichopo Msoga, Shabani Mbogo akielezea changamoto za kilimo katika eneo hilo.
Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Pwani,Kapilima George (wa pili kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la Kikundi cha Gezaulole katika Kata ya Msoga.

 Mkulima Ally Mhenga akichangia jambo kuhusu changamoto za kilimo zinazowakabili.
 Mwenyekiti wa Kikundi cha Gezaulole, Ali Hussein akiangalia mbegu ya Wema.
 Mkulima akisubiri majibu ya maswali yake kuhusu mbegu 
ya Wema.


 Matifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu (wa nne kushoto), akielekeza namna ya kupanda mbegu hiyo kwa wanakikundi cha Gezaulole.
 Hapa akielekeza vipimo vya upandaji wa mbegu hiyo.
 Zoezi la upandaji wa mbegu hiyo likiendelea.
 Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Jovin Bararata, akizungumza na wakulima wa Kata ya Kibindu.
 Mkurugenzi wa Fedha wa Fedha na Utawala wa COSTECH, Shabani Hussein (wa pili kulia), akimkabidhi Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kibindu, Juma Athumani (kushoto), mbegu ya mahindi ya Wema 2109 katika uzinduzi wa shamba darasa uliofanyika leo katika Kata hiyo Mbwewe mkoani Pwani. Wengine kutoka kulia ni ni Matifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu, Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Jovin Bararata, Diwani wa Kata ya Kibindu, Ramadhani Mkufya na Ofisa Kilimo Mkoa wa Pwani, Kapilima George. 
 Wanawake wa Kata ya Kibinda wakiwa kwenye uzinduzi wa mbegu hiyo.
 Matifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu, akitoa maelezo ya upandaji wa mbegu hiyo kwa wakulima wa Kata ya Kibindu.
 Diwani wa Kata ya Kibindu, Ramadhani Mkufya , akichangia jambo.
Ofisa Kilimo Mkoa wa Pwani, Kapilima George, akizungumza na wakulima wa Kata ya Kibindu.

Na Dotto Mwaibale, Chalinze

WAKULIMA wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoani wa Pwani wamefurahia kupokea mbegu bora ya mahindi aina ya Wema 2109 kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kwa ajili ya kupandwa kwenye mashamba darasa katika halmashauri hiyo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mbegu hiyo kwenye uzinduzi wa mashamba darasa katika vijiji vya Diozile na Kibindu vilivyopo Kata ya Msoga mkoani humo Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Pwani,Kapilima George alisema mbegu hiyo itasaidia kuongeza tija ya uzalishaji wa mahindi katika halmshauri hiyo hivyo amewataka wakulima kuichangamkia.

"Tuwashukuru COSTECH na OFAB kwa kutuletea mbegu hii ambayo kwetu itakuwa ni mkombozi mkubwa katika mkoa wetu hasa kwa wakulima wa Kata ya Kibindu ambao ni vinara kwa kilimo cha mahindi katika mkoa wetu" alisema George.

Alisema mkoa wa Pwani kwa mwaka jana ulizalisha tani 110 za mahindi huku tani 65 zikizalishwa na Kata ya Kibindu jambo la kuwapongeza wakulima wa kata hiyo.

Alisema mbegu hiyo itaongeza msukumo wa kilimo ilimo cha mahindi kwenye halmashauri hiyo hivyo kujikwamua kupata baa la njaa na ziada kuuza. 

Aliwaomba wakulima hasa kwa wanavikundi waliopata mbegu hizo kuhakikisha wanayatunza mashamba darasa hayo kwa manufaa ya wakulima wote wa wilaya hiyo.  

Akizungumza kwa niaba ya  Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH wakati wa kukabidhi mbegu  hizo, Mkurugenzi wa Fedha wa Fedha na Utawala wa COSTECH, Shabani Hussein alisema 
kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala yote yanayohusu  Sayansi na Teknolojia na kusimamia tafiti zote za kisayansi katika maeneo mbalimbali na kilimo na kuhakikisha zinawafikia walengwa ambao ni wakulima.

Alisema mbegu hizo walizozikabidhi zimefanyiwa utafiti na zitapandwa katika mashamba darasa na baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima kukabiliwa na mbegu ambazo zilikuwa hazina ubora.

Matifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu alisema iwapo mkulima atafuata ushauri wa upandaji wa mbegu hiyo ya Wema 2109 katika ekari moja atapata magunia 35 tofauti na mbegu nyingine ambapo wanapata chini ya hapo.

Aliongeza kuwa mbegu hiyo italeta matokeo mazuri iwapo kanuni za kilimo bora zitafuatwa kama vile kufuata vipimo, maandalizi ya shamba, matumizi ya mbolea zote ya kupandia na kukuzia na kuwa mbegu hiyo ni moja kati ya mbegu 11 zilizofanyiwa utafiti.

Ofisa mradi huo kutoka COSTECH, Bestina Daniel alisema kwa mkoa huo wametoa mbegu kilo 58 kwa ajili ya mashamba darasa katika wilaya ya Bagamoyo na Chalinze ambapo kwa wakulima mmoja mmoja wametoa kilo 42 pamoja na mbolea ya kupandia.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More