Kamishna
wa Elimu nchini amekataa maombi yote ya shule za msingi na sekondari
zisizo za Serikali kupandisha ada katika mwaka huu wa masomo na ameagiza
shule zilizopandisha ada kinyume cha tamko la Serikali kusitisha ada
hizo mpya.
Kutokana
na uamuzi huo, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi
imeziagiza shule zote za binafsi ambazo zimepandishia ada kiholela bila
kupata kibali cha wizara hiyo, kurejesha ada waliyokuwa wanatoza mwaka
jana, la sivyo hatua kali zitachukuliwa kwa shule itakayokaidi.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ithibati ya Shule, Hadija Mcheka amesema
baada ya tangazo la wizara hiyo kuzitaka shule binafsi zinazotaka
kupandisha ada kuwasilisha maombi kwa Kamishna wa Elimu na kutoa sababu
za kupandisha ada, ni shule 45 tu zilipeleka maombi ya kupandisha ada
wakati shule zingine 900 ziliomba ziendelee kutoza ada ya mwaka jana.
“Hizi
shule 45 hazikupata kibali cha kupandisha ada maana sababu walizozitoa
hazikumridhisha Kamishna wa Elimu hivyo akaamuru zibakie na ada ya mwaka
jana,” alisema Mcheka.
Tanzania ina jumla ya shule za msingi 14,000 na kati ya hizo shule binafsi ni 1,000.
Tanzania ina jumla ya shule za msingi 14,000 na kati ya hizo shule binafsi ni 1,000.
Kwa
upande wa sekondari, shule binafsi ziko zaidi ya 1,400 kati ya
sekondari 4,000. Mcheka alifafanua kuwa baadhi ya shule zilitoa sababu
kuwa wanapandisha ada kwa sababu wana ujenzi, jambo ambalo kamishna
aliona halimhusu mzazi.
“Mwingine
anasema anataka kupandisha ada kwa vile anataka kuajiri walimu kutoka
nje ya nchi, hili nalo halimhusu mzazi ndio maana tumewanyima kibali cha
kupandisha ada,” alieleza.
Pia
alisema shule zingine zilinyimwa ruhusa ya kupandisha ada kwa sababu
hazikutoa sababu yoyote zaidi ya kueleza kuwa wanataka kupandisha ada
kutokana na gharama za uendeshaji.
“Sababu zote hizi hazikumridhisha kamishna ndio maana tumewataka watii agizo la Serikali hadi hapo baadaye.” Alifafanua.
Mcheka
alisema hatua ya kuzitaka shule zote zibaki na ada ya mwaka jana ni
kutokana na wizara hiyo kumwajiri mtaalamu mwelekezi anayefanya kazi ya
kujua gharama za kumsomesha kila mwanafunzi ili kuisaidia Serikali
kuweka ada elekezi.
Alisema ada elekezi hiyo ndio itakayoisaidia wizara kupanga ada elekezi kwa shule binafsi.
Aliwaonya wamiliki wa shule binafsi ambao wamepuuza agizo hilo kwa kisingizio kuwa hawajapelekewa barua na wizara husika kwamba watachukuliwa hatua kali za kisheria zilizoainishwa wakati shule inaposajiliwa.
Aliwaonya wamiliki wa shule binafsi ambao wamepuuza agizo hilo kwa kisingizio kuwa hawajapelekewa barua na wizara husika kwamba watachukuliwa hatua kali za kisheria zilizoainishwa wakati shule inaposajiliwa.
Alisema
Serikali inafanya kazi kupitia waraka, matamko na maagizo ambayo lazima
wahusika wanaohusika kuyatiii na sio kusubiri kuandikiwa barua.
“Katika
hili hatutanii kama zipo shule ambazo hazikutii tamko lile la Serikali
na wakapandisha ada naomba wasitishe ada hizo mpya,” alionya.
Mcheka
aliwataka wazazi na walezi walioanza kulipa ada hiyo mpya kusitisha
malipo hayo mara moja na kwamba wahakikishe kuwa ada yote watakayolipa
kwa mwaka huu ifanane na ile iliyolipwa mwaka jana na sio vinginevyo.
“Kama
mwaka jana alilipa Sh milioni 1.5 na mwaka huu amepandishiwa hadi Sh
milioni 1.8, na kwa kuwa mzazi analipa kwa term (muhula)na tayari
ameshalipa term ya kwanza, naomba atakapolipa muhula wa pili alipe pesa
pungufu ya kile alicholipa term (muhula) ya kwanza ili zitimie Sh
milioni 1.5 na sio Sh milioni 1.8,” alisema Mcheka.
Aliwataka
wazazi na walezi kutoa taarifa wizarani na ofisi za elimu za wilaya kwa
shule ambazo zitakaidi agizo hilo ili hatua ziweze kuchukuliwa.
0 comments:
Post a Comment