Mtoto
wa miaka 11, Nchambi Tungu, ameuawa kikatili na mama yake mzazi kwa
kuchapwa fimbo kisha kumfunga kamba shingoni na kumning’iniza kwenye
tawi la mwembe ili ionekane kuwa amejinyonga mwenyewe.
Wazazi
na Walezi wa Wanafunzi wanaosoma kitengo cha elimu ya Watu Wazima katika Shule
ya Sekondari Pasiansi iliyopo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, wameiomba
Serikali kuondoa ada kwa wanafunzi hao ili nao waweze kunufaika na mpango wa
elimu bure nchini.
Wanasheria nchini wamemtaka Rais John Magufuli ingilie kati sakata la Zanzibar kwa sababu sintofahamu inayoendelea kutokea visiwani humo ni aibu ya Tanzania mbele ya Jumuiya ya Kimataifa.
Watu watatu wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya toyota Noah yenye namba za usajili T243 DGB lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Tabora kugongana uso kwa uso na basi la abiria la kampuni ya Adventure lenye namba za usajili T 852 CBF lililokuwa likitoka mkoani Kigoma kuelekea jijini Dar es Salaam katika kijiji cha Buingiri madukani wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
MBUNGE wa Nzega Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hussein Mohammed Bashe amejitokeza hadharani na kumtaka Waziri wa Zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuacha kulipotosha taifa kutokana kauli zake juu ya utendaji wa Rais John Magufuli.
Mshindi wa Ubunifu mitindo Jocktan Cosmas Maluli A.k.a Makeke(aliyeshika cheti)
akiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa shindano hilo kuanzia
kushoto ni Zamda George, Comfort Badaru, Martin Kadinda, Reuben Nabora na
Stanley Kamana.