Tuesday, September 30, 2025
VIONGOZI, WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUDHIBITI MOTO MISITUNI
Sunday, September 28, 2025
ELIMU YA USALAMA NA AFYA KAZINI YAWAFIKIA WASIOONA.
Afisa Mafunzo wa OSHA, Bw. Simon Lwaho, akiwasilisha mada kuhusu vihatarishi mahali pa kazi na udhibiti wake kwa wanachama wa Jumuiya ya Wasioona Tanzania (TAB) katika semina ya mafunzo iliyoandaliwa na OSHA kwa kundi hilo.Friday, September 19, 2025
OSHA YAKABIDHI VIFAA CHUO CHA UFUNDI MIRONGO JIJINI MWANZA
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi, akiwasilisha hotuba yake wakati wa Bonanza la OSHA la Huduma kwa Jamii (OSHA CSR BONANZA 2025) lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Nyakabungo Jijini Mwanza akiwa ni Mgeni Rasmi wa Bonanza hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda wakimkabidhi Mkuu wa Chuo cha Ufundi cha Mirongo vifaa mbalimbali vya msaada vilivyotolewa na OSHA kukiwezesha chuo hicho. Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na kompyuta, makoti ya usalama na vifaa vya michezo.
Na Fredy Mgunda,Kwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mheshimiwa Amina Makilagi, amewataka waajiri na wafanyakazi kote nchini kuitekeleza kikamilifu Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Na. 5 ya mwaka 2003 ili kupunguza au kuondoa kabisa ajali na magonjwa yanayotokana na mazingira duni ya kazi.
Mheshimiwa Makilagi alitoa wito huo jana wakati wa Bonanza la OSHA la Huduma kwa Jamii (OSHA CSR Bonanza 2025) lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Nyakabungo, Wilaya ya Nyamagana, Jijini Mwanza. Bonanza hilo lilihusisha shughuli mbalimbali za kijamii na michezo kwa lengo la kuimarisha mshikamano kati ya OSHA na jamii inayohudumiwa, pamoja na kutoa msaada kwa wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Mirongo, wakiwemo wenye ulemavu.
Katika tukio hilo, OSHA ilikabidhi vifaa mbalimbali kwa Chuo cha Ufundi Mirongo, vikiwemo kompyuta, vifaa kinga vya usalama kazini, pamoja na vifaa vya michezo kama mipira na jezi za michezo.
Akizungumza kama Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Makilagi aliipongeza OSHA kwa juhudi zake za kuhakikisha mazingira salama na yenye afya sehemu za kazi na kuonesha moyo wa huruma kwa makundi maalum katika jamii.
“Nitoe rai kwa waajiri na wafanyakazi nchini kuisoma na kuitekeleza Sheria Na. 5 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003. Sheria hii ikitekelezwa ipasavyo, maeneo ya kazi yatakuwa salama, bila ajali wala magonjwa, hivyo kuongeza tija kazini,” alisema Mkuu wa Wilaya Makilagi.
Aidha, aliihakikishia OSHA ushirikiano wa Halmashauri na Ofisi yake katika kusimamia usajili na ukaguzi wa maeneo ya kazi, sambamba na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya maboresho ya mazingira ya kazi.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, alisema Bonanza hilo ni sehemu ya mpango wa taasisi hiyo wa kurudisha kwa jamii (Corporate Social Responsibility) na kwamba msaada uliotolewa kwa Chuo cha Mirongo umetokana na tathmini iliyofanywa na wataalam wa OSHA baada ya kutembelea chuo hicho.
“Tunaamini kuwa kwa kusaidia vyuo vya ufundi kama Mirongo, tunachangia kwa kiasi kikubwa maandalizi ya wataalamu wa baadaye katika fani muhimu za kiufundi na kazi,” alisema Bi. Mwenda.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mirongo, Bi. Herieth Richard, pamoja na mwanafunzi wa fani ya ushonaji, Bi. Aneth Augustino, waliishukuru OSHA kwa msaada huo ambao wamesema umeongeza ari ya kujifunza na kushiriki katika shughuli za kijamii.
Bonanza hilo lilihusisha michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, riadha, na michezo ya jadi kama kukimbia kwenye magunia, kukimbia na ndimu kwenye kijiko, rede na kukamata kuku. Washiriki walitoka OSHA na vyuo vya Ufundi vya Mirongo, Nyakato na Kisesa.
Chuo cha Ufundi Mirongo kinamilikiwa na Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), na hutoa mafunzo ya umeme, useremala, ushonaji na uchomeleaji kwa vijana wakiwemo wenye mahitaji maalum.
Thursday, September 18, 2025
MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI WODI YA MAMA NA MTOTO MWAMI NTALE
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Ismail Ali Ussi, ameweka jiwe la msingi katika wodi ya mama na mtoto katika Kituo cha Afya cha Mwami N’tale, kilichopo kata ya Heru, Halmashauri ya Mji Kasulu.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Ussi amesisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao kwa amani, utulivu, na kuchagua viongozi wanaowataka. Amesema kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu inahimiza amani kama msingi wa maendeleo ya taifa.
“Maendeleo tunayoyaona leo ni matokeo ya utulivu na amani inayotamalaki nchini. Hivyo ni wajibu wetu kuilinda na kuithamini hali hii,” alisema Ussi.
Mradi wa ujenzi wa kituo hicho umegharimu kiasi cha Tsh milioni 300, na tayari umekamilika kwa asilimia 100. Utaanza kutoa huduma za afya kwa kina mama na watoto katika eneo la Heru na maeneo jirani.
Kituo hiki kinatarajiwa kupunguza kwa kiwango kikubwa vifo vya mama na mtoto kwa kutoa huduma bora, za karibu, na za uhakika kwa wananchi.
Mwenge wa Uhuru umeendelea kuwa chombo muhimu katika kuhamasisha maendeleo, uwajibikaji, na uzalendo miongoni mwa Watanzania.
Wednesday, September 17, 2025
MWENGE WA UHURU WAZINDUA KITUO CHA POLISI NYAKITONTO KWA AJILI YA KUONGEZA USALAMA
Tuesday, September 16, 2025
TRA NACHINGWEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAJASIRIAMALI WADOGO
Na Fredy Mgunda, Nachingwea Lindi.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wilayani Nachingwea imezindua rasmi dawati maalum la kushughulikia changamoto za wajasiriamali wadogo, ikiwa ni hatua ya kuwawezesha kiuchumi na kuwainua kutoka ngazi ya chini ya biashara hadi kuwa wafanyabiashara wakubwa.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja wa TRA wilaya ya Nachingwea, Novatus Chamu, alisema kuwa dawati hilo litakuwa chombo muhimu cha kusikiliza kero, kutoa elimu ya kodi, na ushauri wa kukuza mitaji kwa wajasiriamali wadogo.
“Kupitia dawati hili, tutaweza kusikiliza kero zao moja kwa moja, kuwapa elimu ya kodi na pia kuwashauri namna ya kukuza mitaji yao ili waweze kuchangia pato la taifa kwa ufanisi zaidi,” alisema Chamu.
Aliongeza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali kusogeza huduma karibu na wananchi, hasa wale waliopo kwenye sekta isiyo rasmi ambao mara nyingi hukumbwa na changamoto ya uelewa mdogo kuhusu masuala ya kodi na taratibu za biashara.
Kwa upande wake, mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Stella Kategile, alieleza kuwa dawati hilo ni jukwaa muhimu la kukuza uchumi wa wafanyabiashara wadogo. Alisisitiza kuwa serikali inalenga kuwawezesha wajasiriamali kupitia utatuzi wa changamoto zao badala ya kuwabana kwa kodi bila kuelewa hali zao halisi.
“Lengo la serikali siyo kukusanya kodi tu, bali pia kusikiliza na kutatua changamoto za wajasiriamali ili waweze kukua na kuchangia kikamilifu katika pato la taifa,” alisema Kategile.
Baadhi ya wajasiriamali waliopata fursa ya kuzungumza walipongeza hatua hiyo ya TRA, wakisema kuwa imekuja kwa wakati muafaka kwani changamoto nyingi zimekuwa zikiwakwamisha katika kuendeleza biashara zao.
“Kwa muda mrefu tumekuwa hatuna pa kupaza sauti zetu. Kupitia dawati hili, tuna matumaini kuwa sauti zetu zitasikika na biashara zetu zitakua,” alisema mmoja wa wajasiriamali hao.
Dawati hilo linatarajiwa kuwa kiunganishi muhimu kati ya TRA na wajasiriamali, na mchango wake unatarajiwa kuleta mabadiliko chanya katika muktadha wa ukusanyaji wa mapato na ukuaji wa sekta ya biashara nchini.
Thursday, September 11, 2025
BALOZI SIRRO;AWATAKA WANANCHI KULINDA AMANI ILIYOPO KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI.
Saturday, September 6, 2025
KASULU YAANDAA BONANZA LA MICHEZO KUHAMASISHA UCHAGUZI NA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu,mkoani Kigoma, Mhe. Kanali Isaac Mwakisu, amesema wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru pamoja na Uchaguzi Mkuu ujao, kwani matukio hayo ni ya kitaifa na yanabeba taswira ya mshikamano wa Watanzania.
Na Fredy Mgunda, Kigoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu,mkoani Kigoma, Mhe. Kanali Isaac Mwakisu, amesema wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru pamoja na Uchaguzi Mkuu ujao, kwani matukio hayo ni ya kitaifa na yanabeba taswira ya mshikamano wa Watanzania.
Akizungumza leo Jumamosi, Septemba 6, 2025, katika bonanza la michezo mbalimbali lililofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Kiganamo, Kanali Mwakisu amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa wilayani humo Septemba 17 na 18, ambapo siku ya kwanza utapokelewa Kasulu Vijijini eneo la Mvugwe na siku inayofuata itakuwa Kasulu Mjini.
“Maudhui makuu ya bonanza hili ni kuwakumbusha wananchi kuwa Mwenge utakimbizwa katika wilaya yetu, na tunapaswa kushiriki kwa wingi ili kuonesha mshikamano na kuthamini amani na utulivu wa nchi yetu,” amesema.
Amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ni tunu kubwa ya taifa, na wananchi wanapojitokeza kuupokea kwa shangwe ni kielelezo cha kuthamini amani na utulivu kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi.
Aidha, amewakumbusha kuwa kwa mujibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Uchaguzi Mkuu utafanyika Oktoba 29, 2025, hivyo wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi baada ya kusikiliza sera za wagombea na kuwachagua viongozi wanaowataka.
Mmoja wa wananchi, Nelstella Kihoza, akizungumza na mwandishi wetu amesema kuwa umati mkubwa uliofurika viwanjani hapo ni ishara tosha ya mwamko wa wananchi wa Kasulu, na kwamba watajitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa kuchagua viongozi wanaowataka, sambamba na kushiriki kikamilifu katika Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Naye Mwalimu Yusufu Hamisi amrmpongeza Mkuu wa Wilaya kwa ubunifu wa kuandaa bonanza hilo, akisema limempa ari ya kuendelea kuhamasisha wananchi wengine kushiriki kikamilifu matukio hayo mawili muhimu ya kitaifa.






Tuesday, September 30, 2025
mwangaza wa hbari












.jpg)
.jpg)



















