Sunday, December 4, 2016

KKKT JIMBO LA MUFINDI LATOA MSAADA KWA WAHANGA WA KAGERA

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William akipeana makono na mmoja katia ya wachungaji walioambatana na Mkuu wa jimbo.
Mkuu wa jimbo la Mufindi mchungaji Antoni Kipangula akiwa amemkabidhi fedha Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William.
 
Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) jimbo la Mufindi limekabidhi zaidi ya  shilingi milioni 02 kwa Mkuu wa wilaya ya Mufindi ikiwa ni sadaka maalum iliyotolewa na waumini wa kanisa hilo kwa wahanga wa janga la tetemeko la ardhi  lililotokea Mkoani Kagera mnamo septemba 13 mwaka huu.
Taarifa ya kitengo cha habari na mawasilino cha halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa vyombo vya habari, emeeleza kuwa, msaada huo wenye jumla ya shilingi  milioni 02 laki 02 na 52 elfu, umewasilishwa na mkuu wa jimbo la Mufindi mchungaji ANTONI KIPANGULA wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Ofisi ya mkuu wa Wilaya Bomani mjini Mafinga.

Mchungaji KIPANGULA amesema wakati wa mkutano wao wa jimbo ulioketi  mapema mwezi oktoba, kwa kauli moja walikubaliana  kutoa  sadaka maalum kwa lengo la kusaidia wahanga wa janga hilo kubwa na lakihistoria hapa nchini.

Akitoa shukrani mara baada ya kupokea misaada hiyo kwa niaba ya serikali, Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William, amewashukuru waumini wote waliojitoa kwa sadaka hiyo maalum kwa ajili ya waathirika wa Kagera na kuahidi kuikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa, kisha akaziomba taasisi za dini ziendelee kuisadia serikali na jamii kwa ujumla katika masuala mbalimbali ya kijamii.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More