Saturday, December 31, 2016

UONGOZI WA SERIKALI YA MTAA WA MARUZUKU BUGURUNI JIJINI DAR ES SALAAM WATOA SARE ZA SHULE KWA WATOTO 200

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maruzuku katika Kata ya Mnyamani Buguruni Manispaa ya Ilala, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Jabiri Sanze (kulia), akimkabidhi sare za shule mtoto, Hamad Ali Dar es Salaamleo, ambaye ataanza darasa la kwanza mwezi huu. Serikali ya mtaa huo imetoa sare za shule, daftari na penseli kwa  watoto 200 watakaoanza darasa la kwanza mwaka huu wa 2017. Katikati ni mama wa mtoto huyo, Farida Rashi...

Friday, December 30, 2016

MAONI YA WATEJA NI MUHIMU KWA UKUAJI WA BIASHARA YAKO

Na Jumia Travel Tanzania KUJA kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia hususani mtandao wa intaneti kumebadilisha kwa kiasi kikubwa mienendo ya matangazo ya utoaji wa huduma mbalimbali duniani na hii ni kutokana na uwezo wake wa kuwaruhusu wateja kutoa ushuhuda, kukosoa au kutoa maoni juu ya walichohudumiwa na kujionea. Tofauti na kipindi cha nyuma kidogo ambapo wataalamu wa masoko walikuwa wanatumia zaidi njia za luninga na redio kuwafikia wateja wao, siku hizi mfumo wa intaneti unapewa kipaumbele zaidi kutokana na namna unavyofikia watu wengi zaidi ndani ya muda mfupi, kwa haraka na gharama kidogo. Matangazo ya luninga na redio yanaweza kuwa hayana ushawishi mkubwa ukilinganisha na mtandao wa intaneti kwani...

HARUSI YA WADAU JACKSON BINAGI NA MONICA SYAGA WA TARIME MKOANI MARA YAFANA.

Leo Disemba 29, 2016 ni siku ya furaha kwa ndugu, jamaa na marafiki wa kijana Jackson John Binagi, wa Kenyamanyori Tarime mkoani Mara (wa tatu kushoto),aliyefunga ndoa na Bi.Monica Syaga wa Mogabiri Tarime, Mara. Maharusi na wapambe wao, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki Maharusi na wapambe wao Maharusi katika ubora wao Wazazi wa bibi harusi wakiongozwa na baba, wakimpa baraka bibi harusi Ni furaha kwa ndugu, jamaa na marafiki kucheza ngoma ya asili ya kikurya (Ritungu) kwenye harusi hiyo. TAZAMA PICHA ZAIDI HA...

MBUNGE MUSSA WA JIMBO LA TANGA AWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA WANANCHI WA JIMBO LAKE

Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF) Mussa Mbaruku amewatakia heri ya sikukuu ya mwaka mpya wakazi wa Jimbo lake  na kuwataka wajitume zaidi ili kuweza kupata mafanikio. Akitoa salamu hizo kwenye ofisi yake wakati akizungumza na waandishi wa habari leo,Mbunge Mussa aliwataka wananchi hao kutambua kuwa wanashirki kwenye shughuli za kimaendeleo ili kuweza kujikwamua kiuchumi. Alisema licha ya kushiriki huo lakini pia wakulima watambue katika kipindi hiki wanapaswa kutayarisha mashamba yao ili kuweza kulima kilimo cha kisasa chenye tija. Aidha pia aliwataka kuhakikisha wanawajibika kusafisha maeneo yao ili yaweze kuwa na muonekana mzuri ili waweze kuepukana na magonjwa ya milipuko yanayoweza kutokana na kuwepo kwa hali...

TAASISI YA MO DEWJI YATOA ZAWADI KITUO CHA TUMAINI LA MAISHA

Taasisi ya MO Dewji Foundation imeweza kuwakumbuka watoto wanaopatiwa matibabu ya magonjwa ya kansa katika kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam. Katika kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka ikiwemo kuingia mwaka mpya wa 2017, MO Dewji Foundation imeweza kutembelea watoto wa kituo hicho cha Tumaini la Maisha na kutoa zawadi kwa watoto hao ili kuwasaidia katika kipindi wawapo kituoni hapo wakiendelea na kliniki ya matibabu yao. Kwa zaidi ya miaka mitatu MO Dewji Foundation imekuwa ikitoa ufadhili na mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula kwa watoto hao, mafunzo kwa watoto hao wawapo kituoni hapo, gharama za usafiri kwa watoto kuja na kurejea kutoka mikoa mbalimbali kwa ajili ya matibabu...

Thursday, December 29, 2016

TAMWA WAPOKEA MALALAMIKO KUTOKA KWA MAKUNDI MAALUM YALIYOSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA 2015 MANISPAA YA IRINGA

Baadhi ya washiriki walikuwa wakijadili ripoti ya tathmini ya jinsi vyombo vya habari (televisheni, magazeti na redio) vilivyoripoti habari zao wakati wakitia nia na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi Mkuu wa 2015 na mjadala huo uliongozwa na  Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA). Na fredy mgunda,iringa MAKUNDI maalumu yanayohusisha vijana, walemavu na wanawake wa mjini Iringa walioingia katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 wakitoa masikitiko yao ya namna vyombo vya habari vilivyowapa nafasi finyu katika mchakato huo.Makundi hayo yalikuwa yakijadili ripoti ya tathmini ya jinsi vyombo vya habari (televisheni, magazeti na redio) vilivyoripoti habari zao wakati wakitia nia na kugombea nafasi mbalimbali katika...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Diseba 29

...

Page 1 of 69412345Next
Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More