Thursday, June 11, 2015

MASHINDANO YA MUUNGANO YAMEFIKIA MWISHO KWA MAFANIKIO MAKUBWA SANA,HUKU DAUDI YASSINI AKING’ATUKA

 DAUDI YASSINI AKIMKARIBISHA MKUU WA WILAYA YA MUFINDI MBONI MAHITA KATIKA UWANJA WA WAMBI MJINI MAFINGA
 MKUU WA WILAYA MBONI MAHITA AKIKAGUA TIMU KABLA YA MCHEZO
 MSIMAMIZI DAUDI YASINI NA MGENI RASMI MBONI MAHITA WAKIWA KATIKA PICHA MOJA NA MABINGWA  WA MUFINDI CUP TIMU YA MKOBA
  MSIMAMIZI DAUDI YASINI NA MGENI RASMI MBONI MAHITA WAKIWA KATIKA PICHA MOJA NA  TIMU YA DODOMA ACADEMY
 SEHEMU YA MASHABIKI WA WALIOJITOKEZA KATIKA MCHEZO HUO WA FAINALI
 SEHEMU YA MASHABIKI WA WALIOJITOKEZA KATIKA MCHEZO HUO WA FAINALI

 na fredy mgunda,iringa


mashindano ya muungano cup yafikia tamati hapo jana kwa mafanikio makubwa huku timu ya mukoba ikishinda  na kuwa bingwa mpya kwa kumfunga timu ya dodoma academy goli mbili bila.

katika mchezo ulikuwa na mashabiki wengi katika uwanja wa wambi uliopo mafinga mjini na kuchezeshwa na marefa wenye weledi wa kazi yao na kuuchezesha mchezo kwa hali ya juu kiasi ambacho mashabiki walifurahia uwepo wa marefa hao katika mchezo huo.

mchezo huu ulikuwa wa vuta nikuvute kutokana na timu zote mbili kuwa katika kiwango bora katika mchezo huo hali iliyokuwa ikiwapa raha mashabiki kila muda kutokana na burudani ilikuwa ikitolewa uwanjani na wachezaji wa timu zote mbili.

kwa upande wake msimamizi wa mashindano hayo DAUDI YASINI alisema kuwa ni kazi ngumu sana kufanikisha mashindano hayo kutokana na kukosa wadhamini wa kudumu hivyo juhudi zake binafsi ndio zilizosababisha mashindano hayo kufanyika kwa mafanikio kipindi chote wakati akiwa msimamizi wa mashindano hayo.

baada ya mashindano hayo kumalizika katika uwanja wa wambi DAUDI YASINI alisimama mbeli ya maelfu ya mashabiki waliokuwa wamejitokeza na kuwaambia kuwa amejuudhuru rasmi kuendelea kusimamia mashindano hayo ambayo amekuwa akisimamia kwa miaka kadha iliyopita.

DAUDI YASSINI aliwapondeza wadau mbalimbali waliokuwa wakimuunga mkono katika harakati zote za kuandana mashindano hayo na kuwaomba waendelee kuwaunga mkono  wasimamizi wengine watakao kuwa wakisimamia hapo baadae.




0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More