Saturday, March 31, 2018

UWT IRINGA WATOA NEEMA KWA WATOTO YATIMA MKOANI HAPA

Katibu wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Iringa Chiku Masanja akiwa mwenyekiti wa UWT wilaya ya Iringa Ashura Jongo na katibu wa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati wakati walipowatembelea watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga nje kidogo ya manispaa ya Iringa kwa kuwafariji na kutoa msaada Katibu wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Iringa Chiku Masanja akiwa mwenyekiti wa UWT wilaya ya Iringa Ashura Jongo,katibu wa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati pamoja katibu wa umoja wa vijana mkoa wa Iringa (UVCCM) Mgego
Wadau mbalimbli pamoja na watoto yatima wakiwa wanasikiliza maneno ya kufariji kutoka kwa Katibu wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Iringa Chiku Masanja 

Na Fredy Mgunda,Iringa.


Yatima wanaoishi katika kituo cha Tosamaganga mkoani Iringa wamepata neema kutoka kwa katibu wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Iringa Chiku Masanja akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali ambao walifika kituoni hapo kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya sikuku ya pasaka kwa watoto hao.

Akiongea na waandishi wa habari kuhusu hatua hiyo ya kutoa msaada kwa watoto wanaokaa mazingira magumu, Masanja alisema kuwa lengo lao kubwa ni kujikwamua kwenye mazingira magumu na ikiwezekana kusiwepo kabisa na watoto tegemezi.

“Lengo letu kuu nikujikwamua kutoka kwenye mazingira magumu na kufuta kabisa uwepo wa watoto tegemezi kwenye jamii yetu” alisema Masenza

Aidha katibu Masanja alisema kuwa wanafanya hivyo kwa sababu watoto yatima wanaoishi kwenye mazingira yanayoonekana na yanayoizunguka jamii hivyo itapelekea wao kuondokana na upweke na kujisikia furaha kama watoto wengine wanaoishi mazingira ya kawaida.

Masanja alisema kuwa wameguswa kutoa msaada katika kituo hicho kwa kutenda matendo ya huruma wakati wa kipindi hiki cha sikuku ya Pasaka kwa watoto kwa kuwa wanamahitiji mengi pia ni kuwapunguzia ugumu wa maisha walezi wa watoto hao.

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Iringa Ashura Jongo alisema jamii inapaswa kuwajali yatima na wanyonge.

Jongo alisema watanzania ni jamii ya watu wanaopendana hivyo, watoto hao wanapaswa kuangaliwa kwa hali na mali ili wasihisi upweke wa kuwakosa wazazi wanapaswa kuangaliwa kwa jicho la tatu kwani hao ni wanyonge.

Lakini Jongo alisema inampasa kila mmoja kwa wakati wake kurudi mwenyewe na kuangalia namna ya kuwasaidia watoto hao wanyonge, kwani nao wanahitaji upendo na misaada mingine kama watoto wenye kulelewa na baba na mama

Nae Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Tosamaganga amewashukuru viongozi wote,wananchi wote pamoja na mkuu wa mkoa kwa kuwaona kwa jicho la pekee na kwenda kuwapa msaada katika kituo hicho.

KAMPUNI YA IVORI IRINGA YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA TOSAMAGANGA

Huu ndio msaada ulitolewa na kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa kwa ajili ya kituo cha Watoto Yatima Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa kwa lengo la kuwapa faraja ya kusherekea sikuku ya pasaka wakiwa na furaha
Watoto wa kituo cha Watoto Yatima Tosamaganga wakiwafurahia kupewa zawadi ya pipi ambazo zinatengenezwa na kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa ambazo zipo kwenye ubora unaotakiwa
Watoto wa kituo cha Watoto Yatima Tosamaganga wakiwafurahia kupewa zawadi ya pipi ambazo zinatengenezwa na kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa ambazo zipo kwenye ubora unaotakiwa
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa wakifurahi kutumia bidhaa bora kabisa kutoka kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa ambazo zipo kwenye ubora unaotakiwa walipokuwa wameenda kuwatembelea watoto wa kituo cha Watoto Yatima Tosamaganga

RC MASENZA ATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA TOSAMAGANGA

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masnza na viongozi mbalimbali wameanza kusherekea mapema ya Pasaka kwa kutoa msaada wa chakula na viu mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Watoto Yatima Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masnza na viongozi mbalimbali wakikabidhi mbuzi katika kituo cha Watoto Yatima Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa.

 Wadau mbalimbali waliojitokeza kutoa zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa.
Viongozi mbalimbali wa serikali waliojitokeza kutoa zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa.
 
Na Fredy Mgunda,Iringa.

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na viongozi mbalimbali wameanza kusherekea mapema ya Pasaka kwa kutoa msaada wa chakula na viu mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Watoto Yatima Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa.

Watoto hao kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Kituo hicho, Sista Winfrida Mhongole, ni wale waliopoteza mama zao wakati wakizaliwa.

“Kituo kinapokea watoto wenye umri wa siku moja na kuendelea na tunaishi nao hapa kwa miaka saba kabla hatujawarudisha kwa ndugu zao waliowaleta,” alisema Sista Mhongole.

Pamoja na chakula hicho kilichojumuisha mchele, mbogamboga, mafuta ya kula na mbuzi, mkuu wa mkoa Masenza na viongozi wengine waliwapa watoto wanaoishi kituoni hapo zawadi zingine zilizojumuisha pipi na mafuta ya kupaka na kiasi cha zaidi ya shilingi lakini nne ambazo zilichangwa na wadau waliofika katika kituo hicho.

Masenza alisema kuwa ofisi yake inatambua umuhimu wa dhana ya maendeleo shirikishi na ndio maana wamekuwa wakijitolea kusaidia kuchangia shughuli zingine za kibinadamu mara kwa mara wanapopata fursa.

“Tulichotoa ni kidogo, lakini tunaamini kimesaidia kuwapa watoto hawa faraja na kujiona sawa na watoto wenzao waliopo majumbani kwao,”alisema.


Akishukuru kwa msaada huo, Sista Mhongole alisema mbali na watoto hao waliopo kituoni hapo, kituo kina watoto wengine katika shule mbalimbali za msingi, sekondari na vyuo ambazo kwa ujumla wake kinafanya kituo kiwe na jumla ya watoto 280.

Alisema watoto hao wamepokelewa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo ya Iringa, Mbeya, Njombe, Morogoro, Dar es Salaam na Morogoro.


“Mbali na mapato yatokanayo na shughuli za kilimo tunazozifanya kama kituo, kituo hiki kinaendeshwa kwa michango ya wahisani mbalimbali wa ndani na nje. Kwa kweli hatuna wafadhili wa kudumu,” alisema na kuomba wahisani waendelee kujitokeza kuwasaidia.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More