Mbunge wa jimbo la Isman na
waziri wa ardhi nyumba na makazi Wiliamu Lukuvi ametabidhi jumla ya kompyuta
ishirini na tano (25) kwenye sekondari za jimbo hilo kwa lengo la kuboresha
elimu kwa wanafunzi ili kuendana na teknolojia ya sasa.
Mbunge wa jimbo la Isman na
waziri wa ardhi nyumba na makazi Wiliamu Lukuvi ametabidhi jumla ya kompyuta
ishirini na tano (25) kwenye sekondari za jimbo sita za jimbo lake
Mbunge wa jimbo la Isman na
waziri wa ardhi nyumba na makazi Wiliamu Lukuvi ametabidhi jumla ya kompyuta
ishirini na tano (25) na hapa akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa sekondari ya Ilambilole
Mbunge wa jimbo la Isman na
waziri wa ardhi nyumba na makazi Wiliamu Lukuvi ametabidhi jumla ya kompyuta
ishirini na tano (25) kwenye sekondari za jimbo hilo kwa lengo la kuboresha
elimu kwa wanafunzi ili kuendana na teknolojia ya sasa.
Mbunge wa jimbo la Isman na
waziri wa ardhi nyumba na makazi Wiliamu Lukuvi ametabidhi jumla ya kompyuta
ishirini na tano (25) akiwa na mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Isman
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge wa jimbo la Isman na
waziri wa ardhi nyumba na makazi Wiliamu Lukuvi ametabidhi jumla ya kompyuta
ishirini na tano (25) kwenye sekondari za jimbo hilo kwa lengo la kuboresha
elimu kwa wanafunzi ili kuendana na teknolojia ya sasa.
Akizungumza katika shule ya
sekondari Ilambilole Lukuvi alisema kuwa ameamua kutafuta njia ya kuendelea
kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa kompyuta ambazo zitawasaidia walimu na
wanafunzi kujua kuwa ulimwengu unaendaje.
“Saizi tunasema kuwa dunia ipo
kiganjani kwako hivyo sekondari zangu zisipokuwa na kompyuta itakuwa nyuma
kiteknolojia hivyo anafanya kila liwezekalo kuhakikisha shule zote za jimbo la
Ismani zinaendana na sayansi na teknolojia” alisema Lukuvi
Lukuvi aliwata walimu kufanya
kazi kwa kujituma kuhakikisha wanafunzi wanafaulu kwa wingi na kuifanya elimu
katika jimbo hilo kuwa yenye ubora unaostahili na kuwa kivutio kwa wananfunzi
wengine kukimbia kusoma katika shule hizo.
“Kweli mnafanya vizuri sana
lakini naombeni muongeze bidii kuhakikisha shule hizi za sekondari za jimbo la
Ismani zinakuwa za mfano kwa kutoa elimu bora na mkifanya hivyo mbunge wenu
mnanijua nitakikisha nawatafutia zawadi nzuri kwa maendeleo ya kwenu na
wanafunzi mnaowafundisha” alisema Lukuvi
Aidha Lukuvi alimpongeza rais
wa Jamhuri ya Muungano kwa kazi kubwa anaifanya ya kuhakikisha kuwa wananchi
wanaofanya kazi wanapata kile wanachostahili na kuondoa dhana ya kuishi
kimazoea kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
“Saizi usipofanya kazi huwezi
pata chochote kile hivyo nilazima kila mwananchi awajibike kwenye maeneo yake
kwa kufanya kazi ili apate kipata la sivyo wataishia kulalamika kila siku
nawaambieni ukweli” alisema Lukuvi
Lukuvi aliongeza kuwa
ataendelea kutafuta pesa kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa majengo ya shule
hizo kadri atakavyokuwa amepata fursa hiyo ila akawaomba wananchi na viongozi
kutunza miundombinu ambayo inakuwa imejengwa na wafadhili ili itumike kwa miaka
mingi.
Nao baadhi ya wakuu wa shule ya
sekondari ya Ilambilole na Ismani walimshukuru mbunge huyo kwa kazi kubwa
anayoifanya kuhakikisha anaboresha sekta ya elimu.
“Angekuwa mbunge mwingine
asingehangaika kuhakikisha anaboresha sekta hii lakini huyu mbunge wetu Lukuvi
amekuwa msaada sana kwa walimu kwa kutoa misaada mbalimbali hivyo tunamuombea
kwa mungu amjalie aendele kuwa na afya
njema” walisema walimu
0 comments:
Post a Comment