Serikali Mkoani Geita imeeleza kusikitishwa na uendeshwaji wa
miradi ya mgodi wa dhahabu wa Geita, (GGM) kwa kutozingatia sheria ya
ushirikishaji kwa Halmashauri zilizopo mkoani humo na kushindwa kujulikana kwa
gharama za miradi ya jamii inayotekelezwa na mgodi huo.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku
chache baada ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kukabidhi mradi wa Maendeleo ya uchumi kwa
Vijana na Wanawake ulipo Mtaa wa Magogo Kata ya Bombambili Halmashauri ya Mji
wa Geita.
Hali hiyo ilimlazimu Mkuu wa mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert
Luhumbi kuzulu kwenye mradi wa vijana na wanawake uliopo
kata ya Bomba mbili ,mtaa wa magogo kwa lengo la kujiridhisha baadhi ya vifaa
ambavyo vilitakiwa kuwepo kwenye mradi huo na hata hivyo amebaini kuwepo kwa
udanganyifu mkubwa kwenye vifaa ambavyo vilitakiwa kuwepo kwenye mradi huo.
Luhumbi alisema
baadhi ya watumishi kutoka serikalini
na baadhi yao kutoka GGM wameendelea kushirikiana kwa pamoja
kuhujumu miradi mingi ambayo
imekuwa ikilenga kuleta chachu ya maendeleo kwa wakazi wa Geita ambao
wamezungukwa na Mgodi huo na kufuatia hatua hiyo ameagiza uchunguzi wa kina
ufanyike ili kuwabaini wale wote ambao wameshiriki kuchakachua fedha za miradi
hiyo.
“Sasa katika miradi yote ishirini na sita (26) ambayo imekwenda
yote ina matatizo na ajabu mwaka huu
niliambiwa kuna fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya CSR ya mwaka huu nilikagua
baadhi ya miradi kuna mradi mmoja nilikuta ni wa bilioni moja nukta sita
lakini mimi siwezi kuficha hata tukitumia fedha vibaya kidogo tunaweza kutumia
milioni mia tatu (300) lakini bilioni moja
nukta tatu inapotea na watu kutoka ofisi
zetu walikwenda mgodini wakaa na kuweka mkataba wakurugenzi hawakuwepo mkuu wa wilaya afahamu baadae
tunaambiwa fedha ipo tayari kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo nimesema sisi
kama mkoa hatubariki miradi hiyo
kabisa”Alisema Luhumbi.
Hata hivyo kutokana na kuonekana upungufu kwenye miradi ya jamii
Mhandisi Luhumbi amewakataa maafisa mahusiano ya jamii wa mgodi wa GGM kutokana
na kushindwa kufanya shughuli zao kwa
weledi kwenye maeneo waliyopangiwa na mgodi huo.
Na pia ameviagiza vyombo vyote vya sheria kuhakikisha wanaingia
kwa undani zaidi na kufanya uchunguzi wa kutosha na ndani ya wiki moja endapo
kuna mtumishi wa serikali atakayebainika
kuhujumu basi sheria ichukuliwe dhidi yake ikiwa ni pamoja na kumwajibisha.
Afisa sheria wa Mkoa huo Bi Sarah Mwangole alisema mradi wa
Magogo ambao umekabidhiwa hivi karibuni umefanyika bila ya makubaliano baina ya
Halmashauri na mgodi wa GGM hivyo pia wameshauri vyombo vya sheria kuingilia na
kufanya uchunguzi na kwamba hadi sasa ofisini kwao hawajapata nyaraka zozote za
mradi huo licha ya kuzihitaji.
Mtandao huu umezungumza
na Msimamizi wa
kitengo cha mahusiano kwenye mgodi wa GGM Bw Joseph
Mangilima ambaye alisema mengi ya mambo
yaliyozungumziwa hawezi kuyazungumzia yeye kwa kuwa hayahusiani na kitengo
chake moja kwa moja na kwamba kazi iliyompeleka kwenye mradi huo ni kupeleka
funguo za majengo baada ya kusikia mkuu wa mkoa anautembelea mradi huo.
0 comments:
Post a Comment