NA SAMIA CHANDE,
SUMBAWANGA
KITUO cha kufua umeme mkoani Rukwa kimepata jenereta ya
kufua umeme yenye uwezo wakuzalisha MegawatI 10 zitakazoimarisha
uzalishaji wa umeme mkoani humo.
Akizungumzia ujio wa jenereta hiyo, Meneja wa TANESCO Mkoani
Rukwa Bw.Herini Muhina, alisema, hali ya uzalishaji umeme itakuwa bora zaidi
na hivyo kufanya upatikanaji wa umeme katika wilaya za Sumbawanga, Laila,
Kalambo na Nkasi kuwa bora zaidi.
“Nimatumaini yetu kuwa ongezeko hilo la umeme, litasaidia kwenda sambamba na mipango ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda kwani umeme wa uhakika utakuwepo na hivyo kufanya Mkoa wa Rukwa kuwa sehemu nzuri ya kuwekeza kwenye sekta hiyo ya viwanda.” Alitoa hakikisho Bw. Muhidin.

Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali Watu wa TANESCO Makao Makuu, Bw. Nathan Daimon (watatu kushoto), akipta maelezo kutoka kwa mdhibiti na mwendeshaji mifumo ya umeme wa Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO), kituo cha Sumbawanga Mkoani Rukwa Bw.Halfan R. Seba
kuhusu jenereta ujio wa jenereta yenye uwezo wa kuzalisha umeme Megawati
10 kwenye kituo hicho.
Bw. Daimon akipewa maelezo zaidi ya uendeshaji shughuli za TANESCO mkoani Rukwa. |
0 comments:
Post a Comment