Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa,ambae pia ni Mnec wa Mkoa wa wa Iiringa Salim Asas akimkabidhi Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kilolo, kiasi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa UWT wilayani humo.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taiga ( NEC)Salim Asas akikabidhi kiasi cha shilingi milioni 5 mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kilolo kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa UWT
Asas akipongezwa kwa mchango wake
Na Fredy Mgunda,Kilolo
MJUMBE wa
halmashauri kuu ya CCM Taifa anayewakilisha Mkoa wa Iringa Salim Asas ameichangia
jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi ( UWT) wilaya ya Kilolo kiasi cha
shilingi milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa mikutano ya
hadhara
Asas ametoa pesa hizo Leo wakati akifungua kikao cha baraza kuu la UWT Wilaya ya kilolo.
Alisema kuwa
lengo la kusaidia jumuiya hiyo ni kuitaka ijitegemee pia kuwa na miradi yake.
Kwani alisema
ameona ni vema kuiwezesha jumuiya hiyo kupata ndoano kuliko kuipa samaki na
kuwa kwa kipindi chake chote cha miaka mitano atakayokuwepo madarakani ataichangia
jumuiya hiyo kiasi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya ujenzi huo
"Ahadi yangu
nitapaswa kuiweka katika maandishi ili familia yangu ijue pale nitakapo
tangulia mbele za Haki ahadi hii iweze kutekelezwa na familia maana hatujui la
kesho"
Hata hivyo
alipongeza jitihada za UWT wilaya ya Kilolo kwa kuwa na mipango ya kimaendeleo
kwa jamii tofauti na vyama vya upinzani ambavyo mipango yao ni maandamano na
vurugu.
0 comments:
Post a Comment