Timu ya Lipuli ya mkoani Iringa imepata pigo baada ya mjumbe
wa Kamati ya Utendaji kutangaza kujivua uachama wa klabu hiyo na kuachia ngazi vyeo
alivyokuwa navyo ndani ya klabu hiyo
Akizungumza na blog hii Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Devotha Chaula alisema kuwa ameamua
kujivua uanachama na uongozi kutokana na kutoelewana na viongozi wa klabu hiyo
kujali maslai yao binafsi
“kujiuzuru uongozi na kujivua uanachama ndani ya klabu ya
mpira wa miguu ya lipuli kutokana na kutokukubali mambo yanayoendelea ndani ya
klabu” alisema Chaula
Chaula alisema kuwa kwasasa hawezi kuongelea mambo mengi
yanayoendelea ndani ya klabu ila viongozi wa lipuli wasipo sema ukweli ya nini
kinaendelea ndani ya timu basi ataweka wazi kila kitu kwa umma
“Mwandishi naomba niache kidogo kwanza nipumzike maana nina
hasira sana nisije ropoka mambo ambayo yataigharimu timu wewe niache hadi
baadae nikwambia kila kitu” alisema Chaula
Bi, DEVOTHA T.
CHAULA,
+255 754531183,
S. L.
P. 600,
IRINGA TZ,
22 - 02 – 2018.
MWENYEKITI WA KLABU YA
MPIRA WA MIGUU YA LIPULI,
S.
L. P. 1149/817,
IRINGA
TZ.
Barua pepe; lipulifc2014@gmail.com
YAH; KUJIUZURU
UONGOZI NA KUJIVUA UANACHAMA NDANI YA KLABU
YA
MPIRA WA MIGUU YA LIPULI.
Husika kichwa cha barua hapo
juu, Mimi Devotha Chaula mwanachama namba LF
00000037 natangaza kujiuzuru uongozi
wangu niliokuwa nao kama Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji na uanachama wangu ndani ya klabu ya Lipuli kuanzia leo
tarehe 22/02/2018 kutokana na sababu
zilizoko nje ya uwezo wangu kama vile matatizo na majukumu ya kifamilia.
WENU
KATIKA KUINUA NA KUKUZA MICHEZO.
Bi,
Devotha .T. Chaula.
0 comments:
Post a Comment