Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018.
Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisikiliza maelezo mbalimbali kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza ,mara baada ya kuwasili katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018.
Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari Mkoani Iringa wakinasa kumbukumbu muhimu kwa ajili ya kuhabarisha wananchi juu ya ziara ya Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko mkoani humo, Leo 19 Februari 2018.
Umati mkubwa wa wachimbaji wadogo katika mgodi wa mgodi wa Nyakavangala uliopo katika Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa wakisikiliza hatma ya mgodi huo kutoka kwa Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika , Leo 19 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko aakikagua mashimo mbalimbali kabla ya kuzungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018.
Na Mathias Canal,
Iringa
Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko
ameagiza kufunguliwa ndani ya wiki mbili mgodi wa Nyakavangala uliopo katika
Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa ili kuwarahisishia huduma
wachimbaji wadogo za kujiingizia kipato chao.
Mhe Biteko ameyasema hayo Leo 19 Februari 2018 wakati
akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara Mara baada ya
kuwasili mgodini hapo kukagua hatua za kiusalama zilizofikiwa tangu kufungwa
kwa mgodi huo 12 Februari 2018 kufuatia matukio matatu ya ajali ambayo
yalipelekea vifo vya wachimbaji wanne.
Mhe Biteko akiwa ameambatana na Mkuu Wa Mkoa Wa Iringa Mhe Amina
Masenza, Kamati za ulinzi na usalama Wilaya na Mkoa wa Iringa, Mkuu Wa Wilaya
ya Iringa Mhe Richard Kasesela na wataalamu Wa Madini kutoka Wizara ya Madini
ameagiza kuchukuliwa hatua za haraka za kujiridhisha uhakika Wa usalama Wa
wachimbaji kuanzia Leo 19 Februari 2018 hadi kufikia 5 Februari 2018 mgodi uwe
umeanza uchimbaji.
Alisema kuwa kufunguliwa kwa mgodi huo kutaongeza kipato cha
wachimbaji hao huku akisisitiza wachimbaji hao pindi mgodi utakapofunguliwa
kuzingatia taratibu za usalama mgodini na kulipa kodi stahiki za serikali.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imekusudia
kuwanufaisha wananchi kupitia rasilimali zao ikiwemo Madini ambapo Tanzania ni
nchi yenye fursa nyingi kwa uchimbaji Madini ilihali wananchi hawanufaiki
ipasavyo na rasilimali hiyo.
Mhe Rais Magufuli ametuagiza kuwalea na kuwasimamia wachimbaji
wadogo nchini ili kutoka kwenye uchimbaji mdogo na kuwa wachimbaji wa kati na
hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa ili uchumi wa nchi ushikwe na watanzania
wenyewe.
Alisema kuwa wachimbaji hao wanapaswa kushirikiana na serikali
kuwafichua waovu wanaoiibia serikali rasilimali Madini kwa kuyatorosha kwenda
sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi pasina kulipa kodi.
"Jichungeni na kujilinda wenyewe ili kila kinachopatikana
serikali ijue imepata kiasi gani na wachimbaji wameingiza kiasi gani na kisemwe
hadharani, ndugu zangu Rais anahangaika kuona kila eneo ambalo lina wachimbaji
wadogo wana rasimishwa na hatimaye wananufaika na madini yao, lakini bado kuna
watu wanatorosha madini" Aliongea kwa msisitizo Mhe Biteko na kuongeza kuwa
"Na Mimi nataka niwaambieni wale wote wanaofikiri katika
serikali hii inayoongozwa na Rais Magufuli wanaweza kupenya na dhahabu watafute
jambo jingine la kufanya maana jambo hilo limepitwa na wakati"
Alisisitiza kuwa wamiliki wa leseni kote nchini wanapaswa
kutunza kumbukumbu za biashara nzima ya madini ikiwemo mapato na matumizi kwa
muda usiopungua miaka mitano kinyume na hapo kwa mujibu wa sheria watatozwa
faini ama kifungo jela
Kwa upande wake Mhe Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza
alisema kuwa wachimbaji hao wanapaswa kutofanya kazi kwa mazoea huku
akisisitiza wachimbaji hao kuwa na ushirikiano na kupendana.
Sambamba na hayo pia aliwasihi kuwa makini na kutofanya ngono
zembe kwani matokeo yake ni kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI jambo
litakalopelekea kupoteza nguvu kazi katika familia na Taifa kwa ujumla.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment