Mwenyekiti wa chama cha mapindizi (CCM) manispaa ya Iringa Said Rubeya akimkabidhi TV na king'amuzi mwenyekiti wa masoko ya manispaa ya iringa Starmi Mathew akiwa sambamba na viongozi na wanachama wa chama hicho
Mwenyekiti wa chama cha mapindizi (CCM) manispaa ya Iringa Said Rubeya akimkabidhi king'amuzi mwenyekiti wa masoko ya manispaa ya iringa Starmi Mathew akiwa sambamba na viongozi na wanachama wa chama hicho
Mbunge wa viti maalumu ritta Kabati akiwa na diwani wa kata ya Mshindo Ngwada pamoja na matha walipokuwa wakikabidhi TV na king'amuzi cha Azam kwa viongozi wa soko kuu la manispaa ya Iringa
Wananchama wa chama cha mapinduzi pamoja na baadhi ya wafanyabiashara walipohudhuria hafla ya kukabidhiwa kwa TV na king'amuzi cha Azam TV kwa viongozi wa soko kuu manispaa ya Iringa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
CHAMA cha mapindizi (CCM) manispaa ya Iringa kimetekeleza ahadi ilikuwa imeahidiwa na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wakati wa kampeni za mwaka 2015 ya kuwatafutia TV wafanyabiashara wa soko kuu la manispaa ya Iringa chini ya mgombea wake wa ubunge mchungaji Petter Msigwa ambaye kwa sasa ndio mbunge wa jimbo la Iringa mjini
Hayo
yamesemwa na mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya alipokuwa anakabidhi
TV nchi 58 na king’amuzi kwa kiongozi wa masoko hapa manispaa.
Rubeya
alisema kuwa wametoa TV hiyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa wananchi na
wafanyabiashara wa soko hilo wanapata habari kwa wakati.
“Mimi
nimekuja jana hapa mkaniambia kero hii nikaichuklua na chama change kimeifanyia
kazi haraka iwezekanavyo na saizi tumekuja kukabidhi” alisema Rubeya
Rubeya
alisema kuwa chama cha mapinduzi kinaamini kwenye utendaji na sio kulalamika na
kuandamana hivyo kuna tumia vizuri falsafa ya Rais Dr John Pombe Magufuli ya
hapa kazi tu ndio maana tupo hapa kufanya kazi kwa vitendo kwa wananchi.
“Chama
cha mapinduzi manispaa ya Iringa kinafanya kazi kwa vitendo pale tunaposikia
kero za wananchi tunatafuta njia za kutatua changamoto hizo ndio maana leo
tunaleta hii TV na king’amuzi ili wafanyabiasha mpate habari mkiwa hapa kazini”
alisema Rubeya
Rubeya
alisema kuwa alipokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiasha ya kutekelezwa kwa
ahadi ambazo zilizotelewa na mbunge wakati kampeni na imepita miaka mingi
haijatekelezwa hivyo wakaamua kuichua na kuitatua ili kuwapa haki wananchi na
wafanyabishara wa soko hilo.
“CCM
tukitoa ahadi tunatekeleza kwa wakati lakini wenzetu wamekuwa wanapiga
propaganda tu za maneno hivyo wananchi mnatakiwa kuchagua viongozi ambao
wanaweza kutekeleza ahadi zao kwa maendeleo ya wananchi wanaowangoza” alisema
Rubeya
Kwa
upande wake mbunge wa viti maalumu ritta Kabati alisema kuwa kitendo cha leo
walichokifanya chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa kinaonesha kuwa chama
hicho ni chama cha wananchi wote ndio maana leo wametoa TV na king’amuzi kwa
ajili ya kupata habari kwa wananchi wanaopata huduma katika soko hilo.
“Kupata
habari ni haki ya kila mwananchi wa mtanzania anapata habari kwa wakati hivyo
kutoa TV hii kutasaidia kuongeza wigo kwa wananchi kupata habari kwa wakati”
alisema Kabati
Kabati
aliwataka viongozi wa soko hili kuandaa mkutano wa kusikiza kero ili
kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuendelea kukuza uchumi na kuleta maendeleo
kwa haraka zaidi na kuendana na kasi ya Rais wa awamu ya tano Dr Johh Pombe
Magufuli.
“Mwenyekiti
naomba mniandalie mkutano nije kuwasikiliza kero zenu kwa kuwa ni haki yenu na
msipofanya hivyo mtakuwa mnajinyima haki yenu ya msingi ya kutatuliwa kero
zenu” alisema Kabati
Naye
mwenyekiti wa masoko ya manispaa ya iringa Starmi Mathew aliwashukuru chama cha
mapinduzi kwa msaada walioutoa kwa kuwa wamerahisisha wafanyabiashara kupata
habari wakiwa kazini.
Mathew
alikiomba chama hicho kuongezea nguvu kwenye masoko mwengine ya manipsaa ya
Iringa kupata hata TV ndogo hata kama sio kuwa kama ambayo imetolewa leo katika
soko kuu la manispaa ya Iringa
“Naomba
nimbe kama hapo mbe mtapa nguvu nyingine basi tunaomba mtukumbuke tena maana
kuna soko hilo hapo chini nalo linahitaji kuwa na Tv nao wewe kupata habari
kama haki yao ya msingi kujia nini kinaendelea duniani” alisema Mathew
Aidha
Mathew akawamba viongozi wa chama cha mapinduzi kuwasidia kuiomba SUMATRA kutengeneza
njia ya daladala ipite katika soko hilo ili kuongeza mzunguko wa kibiashara
kama ilivyo mikoa mingi hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment