Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Iringa umemaliza salama kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa. Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Comred Kenani Kihongosi
Akitoa nasaa na salamu za Chama katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Christopher Magala alisema kuwa Vijana ni Viongozi wa sasa na baadae Vijana ndiyo jeuri ya Chama hivyo amewaasa Vijana kufuata sana miongozo ya Chama kwa maana ya Katibu ya CCM na Kanuni ya Umoja wa Vijana kusiwe na muingiliano na mgongano katika kutekeleza majukumu ya kila siku.
Nae Kihongosi aliwaasa Viongozi kuwa hii awamu ni yakazi tu ni lazima Vijana/Viongozi tujipambanue katika kuwasemea Vijana, kuwatumikia Vijana wa makundi yote kwa mfano Machinga, madereva wa bodaboda Bajaji, Madereva wa Daladala Vijana wa Mijini na Vijijini Vijana wasomi na wasiowasomi kwa ujumla alisisitiza kuwa UVCCM iwe ndiyo kimbilio na sauti ya Vijana wote bila kujali dini zao rangi au ukabila.
"Kwenye uongozi wangu sitomvumilia mtu yeyote yule atakae ivuruga jumuiya kwa maslahi yake binafsi" Alisema Kihongosi
Maana wapo Vijana au Viongozi wachache wanaoichafua Jumuiya kwa kuwa ombaomba kutumia mgongo wa Jumuiya hivyo vitendo sasa havikubaliki alisema Kihongosi wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza.
Baraza hili pia lilifanya Uchaguzi wa kamati ya Utekelazi ya Mkoa na kuwapata wajumbe hao watatu ambao ni:
NANCE NYALUSI
FREDY CHALAMILA
FREDY NDANZI
Ambao wote walipigiwa kuwa na kushinda kwa kishindo kati ya watu sita waliokuwa wamejitokeza kuomba nafasi hii.
Kupitia kikao hiki pia Baraza liliweza kumthibitisha
Kuwa katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Mkoa wa Iringa ambapo uteuzi wake ulifanya na Kamati ya Utekelezaji ya Mkoa iliyochaguliwa leo. Baada ya kumpata katibu hamasa na chipukizi wa UVCCM Mkoa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa
Kenani aliwashukuru wajumbe kwa mahudhurio yao mazuri na aliwasisitiza sana viongozi kwenda kufanya kazi, kwani awamu hii ni yakazi tu kama kauli mbiu ya Mwenyekiti wetu wa CCM na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Joseph pombe Magufuli ya hapa Kazi Tu.
Alisisitiza pia Upendo, Umoja na Mshikamo ili Jumuiya ya Vijana iwe mfano kwa Chama na Taifa kwa ujumla
Mwisho kabisa alisema Kila kiongozi akatimize wajibu wake. Na baada ya kusema hayo aliahirisha kikao hadi siku nyingine.
TUKUTANE KAZINI
"KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI"
Imetolewa na:
James D. Mgego
Katibu UVCCM Mkoa wa Iringa
0753 738 553
0 comments:
Post a Comment