Na Fredy Mgunda, Iringa
MBUNGE
wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamud Mgimwa amemwokoa mtoto wa kike
ambaye ni mlemavu wa viungo kwa kumpeleka shule baada ya wazazi wake
kushindwa gharama za masomo.
Mtoto
huyo Rosemary Lutego ambaye ana umri wa miaka 15 alichaguliwa kujiunga
na kidato cha kwanza katika shule yawasichana Iringa lakini alishindwa
gharama za masomo na matumizi shuleni baada ya wazazi wake kukimbia
jukumu la kumpeleka shule.
Mbunge
Mgimwa baada ya kugundua changamoto inayomkabili binti huyo licha ya
kufaulu na kushindwa kujiunga na wenzake kuanza masomo ya kidato cha
kwanza ndipo alipoamua kumsomesha katika shule maalum ya Wasichana
Iringa ambayo ni mchanganyiko.
Mwanafunzi
huyo alijulikana kama yuko nyumbani baada ya ziara ya kikazi aliyofanya
mbunge Mahamud Mgimwa katika kata mbalimbali na kubaini uwepo wa
mwanafunzi ambaye alikosa vifaa mbalimbali vya shule na kuamua kuchukua
jukumu la kumsomesha hadi anamaliza shule.
Mara
baada ya kupata taarifa za mwanafunzi huyo,Mgimwa alizungumza na wazazi
na walimu katika shule ya Msingi Ikweha na kuwataka uongozi wa kijiji
cha Ikweha kuwatafuta wazazi hao na kuwapeleka katika vyombo vya sheria
huku akichukua jukumu la kumnunulia vifaa vyote vinavyohitajika shuleni
hapo.
Aidha
aliwataka wazazi wote ambayo wana tabia ya kuwazuia watoto waliofaulu
kujitokeza haraka kabla ya msako kuanza popote pale katika jimbo la
Mufundi Kaskazini ambapo wawapeleke shule kutokana na sasa hakuna ada
wala mchango katika shule za serikali.
Aidha
aliwataka wazazi kuacha tabia ya kuwafundisha watoto wao tabia ya
kujifelisha katika mitihani ili waweza kuolewa wakati uwezo wa kufaulu
upo kwa mtoto husika.
Akizungumza
mara baada ya kupata msaada huo mtoto Rosemary Lutego alisema kuwa
ndoto yake ya kupata elimu na kuweza kuja kuwasaidia wazazi wakeimeanza
kupata mwanga kwani alidhani ndoto zake zimeishia darasa la saba.
alimshukuru
sana mbunge Mgimwa msaada huo mkubwa wa kufanikisha masomo yake kwani
itakuwa mfano mkubwa wa wazazi wengine ambayo hawataki mtoto wa kike
aende shule.
Aliongeza
kuwa wazazi wake walimwambia kuwa wanaenda kutafuta fedha za kununulia
vifaa lakini hadi sasa hawakuweza kufanikisha hali iliyomlazimu abaki
nyumbani wakati wanafunzi wengine wakiendelea na masomo.
"Namshukuru
sana mbunge kwa kusikia na kuamua kugharamia masomo yangu ya sekondari
nitahakikisha nasoma kwa bidii licha ya ulemavu wangu ili kuweza
kuikomboa familia yangu katika umaskini." alisema
0 comments:
Post a Comment