Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Julian Raphael Banzi, akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha kwa waandishi wa habafri za Uchumi, Biashara na Fedha, mkoani Mtwara leo Februari 5, 2018.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mtwara
WAANDISHI
wa Habari za uchumi na Fedha, wameaswa kutumia kalamu zao vema ili kuongeza
tija katika jitihada za serikali za kujenga uchumi wa viwanda nchini ifikapo
mwaka 2025, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt.Julian Raphael Banzi
amesema leo Februari 5, 2018 wakati akifungua semina ya waandishi wa habari za
Uchumi, Biashara na Fedha kwenye ukumbi wa BoT , mkoani Mtwara.
“Waandishi
mnao wajibu wa kuamsha ari ya uelewa kwa wananchi kuwaelimisha nini serikali
inafanya kwa ajili ya nini na kwa utaratibu upi.” Alisema Dkt. Banzi na kuwaasa
badala ya waandishi kutumia muda mwingi kuandika maswala ambayo hayasaidii sana
katika kusaidia ujenzi wa uchumi, ni vema sasa wakaangazia katika kuelimisha
umma juu ya jitihada za serikali wakati huu ambapo kuna utekelezaji wa miradi
mbali mbali ya kiuchumi kama vile jenzi wa reli ya kisasa, (SGR).
Naibu
Gavana pia amewataka waandisjhi wa habari kuwafichua wale wanaokatisha tama au
kukwamisha uwekezaji nchini kwani kwa kutofanya hivyo waandishi wa habari watakuwa
hawawatendei haki wananchi na umma kwa ujumla.
Alisema
kuwa BoT inaposema pato la taifa limeongezeka, haimaanishi kwamba wananchi wanajazwa
pesa mfukoni lakini pia mwananchi inabidi ajiulize yeye mwenyewe anashiriki
vipi katika ujenzi wa uchumi ili kuweza kufaidika na pato lenyewe.
“Kwa
msingi huo elimu mtakayopata hapa katika kipindi cha siku tano, itawaongezea
uwezo wa kufanya uchambuzi wa kina mnapoandika makala ze uchumi, biashara na
fedha ili ziweze kuufikia umma kwa usahihi na kuepuka upotoshaji.” Alisema Dkt.
Banzi.
Kwa
upande wake, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Itifaki cha BoT, Bi. Zalia Mbeo,
alisema semina hii ni ya tano ambazo BoT imekuwa ikifanya kila mwaka, ili
kujenga uelewa kwa waandishi kuweza kuandika kwa usahihi shughuli za BoT.
“Tumezidi
kuona mafanikio makubwa tangu tuanze kutoa semina kwa waandishi wa habari kwa
waandishi wamekuwa wakijitahidi kuandika kwa usahihi taarifa za BoT.” Alisema.
Bi
Mbeo pia alisema katika semina ya mwaka huu, waandishi watapata fursa ya
kuelimishwa mambo mbalimbali kutoka Kurugenzi ya sera na tafiti za uchumi,
kurugenzi ya masoko ya fedha, kurugenzi ya usimamizi wa ,mabenki, kurugenzi ya
huduma za kibenki na kurugenzi ya mifumo ya malipo, na pia kuna ushiriki kutoka
kurugenzi ya bima ya amana.
“Mwaka
huu tuna kurugenzi ya Katibu wa Boadi ambayo itaelezea dawati ambalo linashughulikia
matatizo ya watu wanayoyapata katika huduma mbalimbali za kibenki, na kwa
kupitia waandishi wa habari, tunategemea wataelimisha umma kuhusu dawati hili.”
Alisema Bi. Mbeo.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Julian Raphael Banzi, akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha kwa waandishi wa habafri za Uchumi, Biashara na Fedha, mkoani Mtwara leo Februari 5, 2018. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Itifaki, Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Zalia Mbeo na Mwenyekiti w aSemina, Bw. Ezekiel Kamwaga,
Baadhi ya waandishi wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye warshan hiyo
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Itifaki, BoT, Bi. Zalia Mbeo, akielezea maudhui ya semina hiyo ambayo itafanyika kwa siku tano kuanzia leo Februari 5, 2017.
Meneja wa tawi la Benki Kuu ya Tanzania Mkoani Mtwara, Bw.Lucas Mwimo, akitoa hotuba ya ukaribisho
Bi.Vicky Msina, kutoka Kitengo cha Uhusiano na Itifaki BoT. akizunguzma mapema wakati wa ufunbguzi wa warsha hiyo.
Bi.Vicky Msina, kutoka Kitengo cha Uhusiano na Itifaki BoT. akizunguzma mapema wakati wa ufunbguzi wa warsha hiyo.
Baadhi ya washiriki
Mwenyekiti wa Warsha hiyo, Bw. Ezekiel Kamwaga akitoa hotuba yake.
Dkt. Banzi akipeana mikono na Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Uchumi BoT, Bw, Johnson Nyella
Dkt. Banzi, (katikati), Bi Zalie, na Bw.Mwimo
Maafisa waandamizi wa BoT.
Mkurugenzi wa Uchumi BoT, Bw, Johnson Nyella, akitoa Mada
ya Mabadiliko ya mfumo wa kuandaa sera ya fedha, ambapo pa,moja na mambo mengine alisema pato la taifa ni mjmuiko wa thamani ya vitu vyote vilivyozalishwa katika uchumi kwa kipindi husika.
Meza kuu
0 comments:
Post a Comment