Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (Kushoto) akimkabidhi Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Prof Ratlan Pardede Mwongozo wa uwekezaji Mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (Kulia) akifurahia jambo na Muwakilishi Mkaazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi Jacqurline Mahon.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (Kulia) akisalimiana na Balozi wa Ireland nchini Tanzania H.E Ambassador Paul Sherlock ofisini kwake Jijini Dar es salaam.
Na Mathias Canal, Wazo
Huru Blog
Balozi wa Ireland nchini Tanzania H.E Ambassador Paul Sherlock amemuahidi
Mkuu wa Mkoa wa simiyu Mhe Antony Mtaka kuendeleza ushirikiano na Mkoa wa
Simiyu ili kuboresha sekta ya Afya kupitia Irish Aid.
Balozi huyo ameyasema hayo wakati wa mazungumzo ya pamoja na Mhe Mtaka ambapo tayari kwa pamoja wamekubaliana kuanza kutekelezwa
wa kusudio hilo tarehe 6 Februari 2018 kwa kuanza na timu ya wataalamu kufika Mkoani
humo ili kuanza haraka shughuli hiyo.
Balozi H.E Ambassador Paul Sherlock amemuahidi Mhe Mtaka kuwa tayari
nchi yake ya Ireland imekusudia kwa dhati kushirikiana vyema na Mkoa huo huku
akisisitiza kuendelea kushirikiana zaidi pia katika utekelezaji wa miradi ya
Maendeleo kwenye sekta ya Mifugo, Kilimo na Utalii.
Balozi wa Ireland nchini Tanzania H.E Ambassador Paul Sherlock ametoa
kauli hiyo ya kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka za
kutoka kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo uwekezaji wakati alipokutana na
kufanya mazungumzo leo 2 Februari 2018 katika.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka amemshukuru Balozi
Sherlock kwa ubalozi wa Ireland kukubali kuwezesha safari ya mafunzo kwa wataalamu
wawili kutoka Mkoani Simiyu kwenda nchini Ireland kuanzia Februari 12 mpaka 16
Machi 2018 kwa ajili ya kupata mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
hasa kwenye upande wa uhifadhi wa Data za Mkoa.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa wa Simiyu Mhe Mtaka alikutana
na kufanya mazungumzo na Muwakilishi Mkaazi wa shirika la Umoja wa Mataifa
linalohusika na Idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi Jacqurline Mahon ambapo pamoja
na mambo mengine Shirika hilo limetoa zaidi Bilioni 3 kwa ajili ya kukarabati
vituo vya afya na upasuaji ndani ya Halmashauri zote za Mkoa wa Simiyu.
Pia UNFPA imeahidi kutoa magari kwa Halmashauri 6 za Mkoa wa
Simiyu kwa ajili ya kuboresha huduma za afya, ambapo tayari UNFPA wameamua kujenga
ofisi yao ndogo ndani ya Mkoa wa Simiyu itakayoratibu shughuli mbalimbali za
shirika hilo kwa mikoa yote ya kanda ya ziwa.
Wakati huo huo Mhe Mtaka amekutana na Balozi wa Indonesia nchini
Tanzania Prof Ratlan Pardede ambaye pamoja na mambo mengine amekubali
kutembelea Mkoa wa Simiyu mwezi Macih mwaka huu 2018 huku akiwaalika wataalamu
wa Mkoa wa Simiyu nchini Indonesia mwezi Aprili mwaka huu.
Aidha, Balozi huyo Prof Pardede alisema kuwa pia sekta rasmi ya
Indonesia itazuru Mkoani Simiyu ili kuona uwezekano wa kujenga kiwanda
kitakachosaidia kuongeza thamani ya zao la pamba, kuboresha mkoa dada wa
Indonesia na Simiyu katika mazao ya Mpunga na pamba pamoja na kualika
wawekezaji wa Indonesia kuwekeza Mkoani Simiyu kwa kuzingatia Mwongozo wa
uwekezaji wa Mkoa wa Mkoa huo (Simiyu Investment Guide) ambao ameusifia kwamba
ni wa kipekee na alipouona mwongozo huo kupitia mtandao wa Youtube aliona ukiwa
umeitangaza sana Tanzania na wafanyabiashara wa Indonesia walihamasika sana
kuuona na kuusoma katika Tovuti hiyo.
0 comments:
Post a Comment