Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa uchimbaji
madini ya dhahabu wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya wakati wa ziara ya kikazi
Mkoani Mbeya, Jana 21 Februari 2018. Picha
Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko akizungumza kwa ukali na baadhi ya viongozi wa Mgodi wa uchimbaji
madini ya dhahabu wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya wakati wa ziara ya kikazi
Mkoani Mbeya, Jana 21 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko akizungumza kwa ukali na mmoja wa kiongozi wa Mgodi wa uchimbaji
madini ya dhahabu wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya wakati wa ziara ya kikazi
Mkoani Mbeya, Jana 21 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Mbeya
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko amekerwa na usiri wa mapato na matumizi ya muwekezaji wa
mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
Mhe Biteko ameonyesha masikitiko
makubwa wakati akizungumza na uongozi wa mgodi huo mara baada ya uongozi wa
mgodi huo kushindwa kumpatia taarifa ya mapato na matumizi wakati akiwa
katika ziara ya kikazi Mkoani humo kukagua shughuli za uchimbaji Madini.
Kumbukumbu hizo zimekosekana
kufuatia viongozi wa ngazi ya juu ya mgodi kutokuwepo kwenye kikao hicho pamoja
na kukiri kupokea taarifa ya ujio wake kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Chunya.
Alisema kuwa viongozi hao kukosekana
pamoja na kuwa na taarifa ya muda mrefu juu ya ziara hiyo ni utovu mkubwa na nidhamu kwa serikali
ya awamu tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt
John Pombe Magufuli.
Alisema kuwa pamoja na kutokuwepo
kwao lakini taarifa zilitakiwa kuwepo ofisini kwani ni kosa kisheria kukosekana
kwa taarifa za mgodi ilihali sheria ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2017 inaeleza vyema kuwa mmiliki wa leseni ya Madini
anatakiwa kutunza kumbukumbu za mapato na matumizi kwa miaka mitano.
"Endapo atashindwa kufanya
hivyo serikali itamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kifungo cha
mwaka mmoja jela ama faini ya shilingi Milioni 50 mpaka milioni 150"
Alisema Naibu Waziri huyo
Mhe Biteko akizungumza huku
akionyesha kukerwa na baadhi ya viongozi ambao walikuwepo katika eneo la ofisi
ya mgodi huo huku wakishindwa kuhudhuria katika kikao hicho cha kazi
alisisitiza kuwa muwekezaji wa mgodi huo anapaswa kuzingatia na kufuata sheria,
taratibu na kanuni za nchi.
Sambamba na hayo pia Mhe Biteko
aliutaka uongozi wa mgodi huo kutoa taarifa sahihi za uwepo wa mashapu katika
mgodi waliyokuwa wakichimba au kama mashapu katika mgodi huo yameisha wafuate
taratibu za kisheria za ufungaji wa mgodi ikiwemo kuyarudisha mazingira katika
halo take ya kawaida.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment