Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) mkoa wa Iringa Nikolina Lulandala akiongea na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi vifaa tiba kwa uongozi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa akiwa sambamba na viongozi wengine wa umoja huo
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) mkoa wa Iringa Nikolina Lulandala akimkabidhi vifaa tiba afisa muuguzi msaidizi wa hospital hiyo Victory Ntara
Baadhi ya makada wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani Iringa wakielekea hodini kukawa zawadi kwa wagonjwa
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) mkoa wa Iringa Nikolina Lulandala akiongea na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi vifaa tiba kwa uongozi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa akiwa sambamba na viongozi wengine wa umoja huoNa Fredy Mgunda,Iringa.
UMOJA wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) mkoa wa Iringa wametoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni nane laki tatu na themanini na tano (8,385,000) katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa kwa lengo la kusaidia kutatua changamoto za afya.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vifaa tiba mwenyekiti wa umoja huo Nikolina Lulandala alisema kuwa wameamua kutoa
msaada wa vifaa tiba kutokana na upungufu uliopo katika hospital hiyo.
“Tumeamua
kufanya hivi kwa lengo la kuboresha sekta ya afya kwa kuwa tumegundua kuwa hapa
kuna changamoto nyingi hivyo sisi ni wanawake ndio maana tumeamua kutafuta
wadau watusaidie kwa kuokoa maisha ya wagonjwa wanaokuja kutibiwa hapa” alisema
Lulandala
Lulandala
alisema kuwa walifanya utafiti kwanza kabla ya kununua vifaa tiba ambavyo
wamevitoa msaada ili kuweza kutatua changamoto kwenye maeneo ambayo ndio
yanakumbana na changamoto husika.
“Nashukuru
tulikuja hapa kimya kimya na tulifanya utafiti na ndio tukaenda kwa wadau
mbalimbali ambao wametusaidia na kutuwezesha kutoa msadaa huu ambao utachangia
kuokoa maisha ya watanzania wanaotibiwa katika hospital yetu hii” alisema
Lulandala
Alivitaja vifaa tiba
ambavyo wamekabidhi hospitalini hapo kuwa ni Injection Gentramicin, boksi 1000, Nabulaiza 1, Injection
Ampiliciline vipande 1000,Suction Mashine 2, box za sabuni, mafuta ya kupaka
watoto na biskuti.
lulandala
alisema kuwa anaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kufanya kazi kwa
kuwafikia wananchi wa chini hasa wale wanyonge kwa kutimiza kile ambacho
kilikuwa kimeahidiwa wakati wa kuomba kura za kuongoza nchi.
“Kiukweli
naomba nichukue nafasi hii kumpongeza sana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kuwa
anafanya kazi kubwa sana kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua ya kimaendeleo
hivyo ni lazima tuonge mkono juhudi hizi” alisema lulandala
lulandala
alisema kuwa serikali imefanikisha kuleta mabadiliko ya haraka katika sekta ya
afya tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea
kufanya kazi kwa kujituma ili kuunga mkono juhudi hizi.
“Najua
kuwa mnaona kwa macho yenu kiasi gani serikali ya wamu ya tano jinsi gani
huduma za afya zilivyo boreshwa na lazima tujivunie hiki kinachofanywa na Rais
wetu,mimi binafsi naunga mkono juhudi hizi na ninaomba wananchi nao waunge
mkono juhudi hizi” alisema lulandala
lulandala
alisema kuwa kuongezaka kwa hospital za rufaa kwenye mikoa,vituo vya afya
kwenye kata au tarafa, zahanati kwenye vijiji na mitaa ni hatua kubwa ya
kimaendeleo hivyo ndio serikali ya awamu hii inavyotekeleza vilivyo ilani ya
chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi 2020.
“Nyie
ni mashaidi kuwa zamani tulikuwa tunaishia kuwa na hospitali za mikoa tu lakini
kwa sasa mambo yamebadilika kila kitu kinazidi kuwa kwenye ubora unaostahili
kuwahudumia wananchi waliotuweka madarakani” alisema lulandala
Lakini
sio afya tu hata ukiangalia saizi tunapata elimu bure ambayo inamwezesha kila
mwanafunzi kusoma bure na kuhakikisha tunapunguza wimbi la wanafunzi kukosa
elimu ambapo inasaidia kuwa nakizazi cha wasomi hapo baadae.
Naye afisa muuguzi msaidizi wa hospital hiyo Victory
Ntara aliwashukuru viongozi hao wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi
(UWT) mkoa wa Iringa kwa kuwatembelea na kufanya usafi na zawadi walizozitoa
kwa watumishi na wagonjwa waliokuwepo muda huo.
“Tunaomba
mtufikishe salamu kwa Rais wa serikali ya awamu ya tano kwa kazi kubwa
anayoifanya kwa kuboresha sekta ya afya kwa kuwa hali ya sasa kila kitu
kinaenda kwa wakati” alisema Ntara
0 comments:
Post a Comment