Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe
Mkoani Geita akisisitiza jambo wakati akihutubia mamia ya wanachama kwenye
maadhimisho ya miaka 41 ya CCM yaliyofanyika Kimkoa katika eneo la Ukumbi wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliopo Kijijini Mtambala Kata ya Katente, Wilayani
Bukombe, Leo 4 Februari 2018. Picha Zote
Na Mathias Canal
Viongozi
mbalimbali wakiwa meza kuu wakati wa maadhimisho ya miaka 41 ya CCM
yaliyofanyika Kimkoa katika eneo la Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliopo
Kijijini Mtambala Kata ya Katente, Wilayani Bukombe, Leo 4 Februari 2018.
Baadhi ya
wananchi wakifatilia kwa makini Mkoani Geita wakifatilia kwa makini maadhimisho
ya miaka 41 ya CCM yaliyofanyika Kimkoa katika eneo la Ukumbi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) uliopo Kijijini Mtambala Kata ya Katente, Wilayani Bukombe, Leo
4 Februari 2018.
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe
akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel wakati wa maadhimisho
ya miaka 41 ya CCM yaliyofanyika Kimkoa katika eneo la Ukumbi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) uliopo Kijijini Mtambala Kata ya Katente, Wilayani Bukombe, Leo
4 Februari 2018.
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe
akimualika aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye kwa sasa ni Mkuu wa
Wilaya ya Iramba Mhe Emmanuely Lwehahula kuwasabahi wanachama wa CCM wakati wa maadhimisho
ya miaka 41 ya CCM yaliyofanyika Kimkoa katika eneo la Ukumbi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) uliopo Kijijini Mtambala Kata ya Katente, Wilayani Bukombe, Leo
4 Februari 2018.
Baadhi ya wananchi wakifatilia kwa makini Mkoani Geita wakifatilia kwa makini maadhimisho ya miaka 41 ya CCM yaliyofanyika Kimkoa katika eneo la Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliopo Kijijini Mtambala Kata ya Katente, Wilayani Bukombe, Leo 4 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Geita
Wafuasi wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) Februari 4 kila mwaka huadhimisha kumbukizi ya
kuzaliwa kwa Chama hicho kutokana na kuvunjwa kwa vyama vya Tanganyika African
National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) Februari 5 mwaka 1977.
Kutokana na
umuhimu wa maadhimisho hayo Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamehimizwa
kuwa na ujasiri wa kuisimamia vyema serikali ili kutatua matatizo
yanayowakabili wananchi katika jamii ili kuakisi mkataba wa wananchi na CCM
kupitia ilani ya ushindi ya mwaka 2015-2020.
Kauli hiyo
imetolewa leo 4 Februari 2018 na Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita wakati akihutubia mamia
ya wanachama waliohudhuria maadhimisho hayo yaliyofanyika Kimkoa katika eneo la
Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliopo Kijijini Mtambala Kata ya Katente.
Mhe Biteko
alisema kuwa kumekuwa na undumilakuwi kwa baadhi ya viongozi wengi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) unaotokana na kujisahau na kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo
linachochea hisia kali kwa wananchi dhidi ya serikali yao kutokana na watendaji
wachache waliopewa dhamana kutotekeleza vyema majukumu yao.
Akizungumza
kwa hisia chanya Naibu waziri huyo alisema kuwa maadhimisho ya CCM ni muhimu
katika Taifa kwani Tendo hilo la kihistoria ni maalumu kwa ajili ya kuendeleza
utamaduni uliokuwa umeanza huko nyuma wa kuunganisha nguvu kwa lengo la
kujiimarisha katika mapambano. Kwa mfano, ASP kwa upande wa Zanzibar ilitokana
na kuungana kwa African Association (AA) na Shirazi Association (SA), tendo
ambalo liliunganisha nguvu za wanyonge katika mapambano ya kuundoa usultani na
utawala wa kikoloni wa Kiingereza.
Alisema kuwa
kwa upande wa Tanzania Bara, TANU ilitokana na kujibadilisha kwa Tanganyika
African Association (TAA) kutoka jumuiya ya kutetea maslahi ya kijamii na kuwa
chama cha siasa ambapo muunganiko wake uliibua mapambano ya ukombozi katika
Afrika na kote duniani kujenga Tanganyika na Zanzibar huru kiuchumi na kijamii
na kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa.
Aidha,
alisiitiza kuwa wananchama wanapaswa kuvunja makundi mbalimbali yanayoibua
hisia hasi za utengano ambazo zinatokana na chuki dhidi ya wananchama wengine, chuki
dhidi ya viongozi wa chama na serikali, badala yake kukiri kwa kauli moja kuwa
Umoja ni Nguvu na Utengano ni udhaifu hivyo kutokuwa na chuki za daima kwani
katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu.
Alisema
kuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi wote wanapaswa kuunga mkono
juhudi za Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ndiye kiongozi mkuu wa serikali, Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwani amekiwezesha
Chama Cha Mapinduzi kuwa Chama chenye nguvu, imara na madhubuti, hivyo kuwa
Chama cha siasa pekee chenye uwezo wa hali ya juu wa kuwaunganisha Watanzania.
Mhe
Mashaka Doto Biteko Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Naibu Waziri wa Madini, alisema
kuwa Rais Magufuli ameiwezesha CCM kuwaongoza wananchi katika mapambano ya
kitaifa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kufuatana na mabadiliko mbalimbali
yanayojitokeza ndani na nje ya nchi.
Sambamba
na hayo pia Mhe Biteko amesifu juhudi hizo za Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe Dkt
John Pombe Magufuli kwa kukiongoza vyema Chama hicho na hatimaye kuendelea kuungwa
mkono na CCM kuendelea kupewa dhamana na wananchi ya kuunda serikali na
kukamata dola tangu 1977 chini ya mfumo wa demokrasia ya chama kimoja hadi sasa
katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, kufuatia mageuzi yaliyoidhinishwa na
marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania Juni 1992.
Maadhimisho
ya miaka 41 ya CCM Mkoani Geita yamehudhuriwa na Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Mkoani Geita Alhaji Said Karidushi ambaye ndiye aliyekuwa mgeni
rasmi katika maadhimisho hayo, Katibu wa CCM Mkoa wa Geita Ndg Adam Ngalawa,
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel, na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha
Mapinduzi na serikali ngazi ya Mkoa, na Wilaya.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment