Katibu tawala wa Mkoa wa Geita,Celestine Gesimba akimkaribisha mkuu wa mkoa kuzungumza na waandishi wa habari juu ya utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi. |
Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Douglas Masanja akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari Mkoani humo. |
Na,Consolata Evarist,Geita
Wananchi
Mkoa wa Geita wametakiwa kutoa ushirikiano kwenye zoezi la utafiti wa mapato na
matumizi kwenye Kaya binafsi ili kutoa takwimu za hali ya umasikini
zitakazosaidia serikali na wadau wengine kutathimini hatua zilizofikiwa katika
kutimiza malengo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
Miongoni mwa
Malengo hayo ni pamoja na yale yaliyoainishwa katika mpango wa pili wa
maendeleo ya miaka mitano pamoja na maendeleo endelevu.
Kata,
Vijiji, Mitaa na vitongoji 34 mkoani humo vinatarajia kufanyiwa utafiti huo ili
kupata taarifa zinazohusu Kaya na wanakaya, Uzazi na unyonyeshaji, elimu, afya,
uraia, uhamiaji, ulemavu, bima, hali ya ajira, biashara na mapato ya kaya na
makazi ya kaya.
Mkuu wa Mkoa
wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi alisema utafiti huo utasaidia kuweka misingi
katika kutambua viashiria vya kiuchumi, ajira na ustawi wa jamii
vitakavyofuatiliwa kwa kipindi husika na kupata makadirio ya jumla ya mwenendo
wa matumzi ya kaya ili kuandaa fahirisi za bei.
“Napende
kuwahakkisa wananchi wa mkoa wetu kuwa katika kutekeleza maagizo ya serikali
,uongozi wa mkoa umeendelea kuhimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii na maarifa
ili kutimiza azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi
ya viwanda na yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025”Alisema Luhumbi.
Amendelea
kusema madhumuni ya utafiti huu wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania
Bara wa mwaka 2017/18 ni kutoa takwimu za hali ya umasikini na takwimu nyingine
ili kusaidia serikali na wadau wengine kutathmini hatua zilizofikiwa katika
kutimiza malengo mbali mbali ya kitaifa na kimataifa yakiwemo yale
yaliyoanishwa katika mpango wa pili wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano
(2016/17-2020/21) na malengo wa maendeleo endelevu.
Mtakwimu
Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Douglas Masanja alisema azma ya
serikali ni taifa kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 hivyo kutokana na
misingi hiyo zinatakiwa ziwepo taarirfa sahihi kutoka kwa wananchi.
Zoezi la
utafiti ambalo linafanyika nchi nzima limeanza Desemba Mosi mwaka jana na
linatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment