Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza na vijana wa kanisa la kikatoriki parokia ya kihesa (UVIKAI) wakati wa kufunga kongamano la vijana hao
Baadhi ya vijana wa kanisa la kikatoriki parokia ya Kihesa wakimsikiliza mbunge wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakatika wa kufnga kongamano hilo.
Na Fredy Mgunda,Iringa
UMOJA wa vijana wa kanisa la
kikatoroki parokia ya Kihesa wamemwangukia mbunge wa viti maalum Ritta Kabati
kuhusu ukosefu wa ajira ambao unaongeza umaskini katika kaya mbalimbali hapa
nchini.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi
mwenyekiti wa umoja wa vijana wa kanisa la kikatoriki kihesa (UVIKAI) Mussa
Kihwele alisema kuwa vijana wengi kwa sasa hawana ajira za kudumu kutokana na
kukoseka kwa nafasi za kazi hivyo kupelekea vijana wengi kuwa wadhurulaji.
“Mgeni rasmi ukipita mtaani
utakutana na kilio kikubwa kwa vijana ni kukosekana kwa ajira na ndio maana
kuna baadhi ya maeneo vibaka wengi wameongeza hasa pita maeneo ya stand yoyote
ile utagundua hilo” alisema Kihwele
Kihwele aliongeza kuwa
kukosekana na kwa miradi mingi ya kudumu nako kunachangia kukosekana kwa ajira
hivyo tunaishauri serikali kuwa na miradi ya kudumu ili kuwa na ajira za kudumu
ambazo zitapunguza ongezeko la vijana wa mitaani.
“Serikali ikiweka mikakati
madhubuti ya kuhakikisha kuna miradi mingi nay a kudumu utaona upungufu wa
vijana mitaani hivyo tunaishauri serikali kufanya hivyo kwa kushirikiana na
sekta binafsi ambazo zinanafasi kubwa katika maendeleo hapa nchini” alisema
Kihwele
Aidha Kihwele alisema
kukosekana kwa ajira kunasababisha kupunguza muamko wa vijana kushiriki katika
makongamano mbalimbali ya kidini kwa
kukosa ada ya kulipia kushiriki kwenye kambi ambazo zinakuwa zimeandaliwa na
umoja huo.
“Ndugu mgeni ukiangalia hapa
unaona idadi imepungua ya vijana kushiriki katika makongamano ya makanisa hasa
hapa tulipo mwaka jana kulikuwa na washiriki wengi tofauti na hali ilivyo hivi
sasa yote hiyo ni kukosekana na ada ya ushiriki” alisema Kihwele
Lakini licha ya kuwa na
changamoto hizo bado tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli anafanya kazi kubwa
kuhakikisha kuna kuwa na ongezeko la ajira kwa vijana na wananchi wengine na
ndio maana saizi anawaajiri vijana wengi kwenye vitengo mbalimbali vya
serikali.
Kwa upande wake mgeni rasmi
katika kongamano hilo mbunge wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM)
Ritta Kabati alisema kuwa anawachangia shilingi laki tano (500,000) kwa ajili
ya kubuni mradi wa kufanya maendeleo ya kudumu.
“Naanza kwa kuwachangia hiki
kidogo kwa ajili ya kuwawezesha kubuni kitu cha kufanya ila mungu akinijalia
nitaongeza kwa mungu na kuongeza ajira kwa wananchi na vijana ambao
wanalalamika ukosefu wa ajira” alisema Kabati
Kabati alisema kuwa atawasaidia
kuwaletea wataalamu wa kufundisha ujasiliamali ambao utasaidia jamii kujiajiri
na kuacha kutegemea ajira kutoka serikali au kwenye sekta binafsi.
“Haya mambo ya kutegemea
kuajiriwa serikali inatakiwa watanzania tuondokane na kasumba hiyo hivyo ni
lazima tujtengenezee mazingira ya kujiajiri kuliko kutegemea kuajiriwa na
serikali” alisema Kabati
Lakini Kabati aliwataka vijana
kujipendekeza kwa mungu kuliko kujipendekeza kwa watu ambao hawana faida katika
maisha ya sasa.
0 comments:
Post a Comment