Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akihutubia mamia
ya wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji
cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari
2018. Picha zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua maeneo
ya uchimbaji baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha
Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua maeneo
ya wachimbaji wadogo wa chama cha ushirika cha Kasi Mpya Gold Mine katika Kijiji cha
Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akihutubia mamia ya wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua maeneo ya wachimbaji wadogo wa chama cha ushirika cha Kasi Mpya Gold Mine katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018
Na Mathias Canal,
Shinyanga
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ametatua mgogoro
wa leseni uliodumu kwa takribani miaka kumi kwa kuamuru kupitia haraka eneo la
leseni ya uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo wa chama cha ushirika cha
Kasi Mpya Gold Mine.
Mhe Biteko ametoa agizo hilo Jana 3 Februari 2018 wakati
akihutubia mamia ya wachimbaji wadogo waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama
kufuatia malalamiko ya Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe Ezekiel Maige sambamba na
malalamiko ya wachimbaji wadogo waliyoyawasilisha Wizara ya Madini Mjini Dodoma
Januari 26, 2018.
Alisema kuwa wananchi walifunga safari mpaka ofisi za madini kwa
ajili ya kupata uhalali wa kupimiwa eneo lao kwa kutumia GPS lakini Kaimu Afisa
madini mkazi Wilaya ya Kahama akawabadilishia Nukta (Coordinator) ambazo
baadaye zilionekana kuwa za eneo jingine ambalo ni mbuga isiyokuwa na madini
huku eneo hilo likihamishiwa kwa ntu mwingine.
Mhe Biteko amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya madini Prof
Simion Msanjila kumchukulia hatua za haraka za kinidhamu aliyekuwa Kaimu Afisa
madini mkazi Wilaya ya Kahama aliyehusika na upotoshaji wa leseni na kuzua
mgogoro wa usumbufu usiokuwa na sababu dhidi ya wananchi na serikali.
Alisema kuwa hakuna sababu ya Wizara ya Madini
kukumbatia mgogoro huo wa leseni uliodumu kwa miaka kumi kwa sababu ya
eneo ambalo lilipotoshwa na baadhi ya watendaji wa Wizara ya madini kwani
jukumu la serikali ni kuwatumikia wananchi ikiwemo utatuzi wa kadhia mbalimbali
zinazowakabili katika jamii.
Mhe Biteko kwa msisitizo mkubwa amewataka wachimbaji wadogo kuwa
waaminifu na kufichua baadhi ya wachimbaji wanaoficha madini kwa kutorosha bila
kulipa kodi kwani kufanya hivyo itakuwa njia pekee ya kuisaidia serikali na
kuinusuru katika mtego wa wizi wa rasilimali hizo.
Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli haitawafumbia macho
wamiliki wa leseni hizo ambao leseni zao zimedumu kwa muda mrefu bila
kuzifanyia kazi kwani hawazalishi ajira yoyote wala kulipa kodi Hivyo serikali
imekusudia kuzifuta na kuwapa watu wengine ambao watazifanyia kazi haraka
iwezekanavyo ili kuongeza tija kwa sekta ya madini katika uchangiaji wa pato la
Taifa.
Akitoa mfano katika eneo la Kahama kuna leseni 249 lakini
zinazofanyiwa kazi ni 18 tu huku wenye leseni zisizofanya kazi wakisubiri
wachimbaji wadogo wavumbue madini kisha huja kuwaondoa kwa kisingizio cha
umiliki wa leseni. Leseni hizo zikiwa zimedumu kwa muda mrefu bila
kuendelezwa.
Aidha, alisema kuwa kuna maeneo makubwa manne ambayo
yameshaamuliwa na serikali kutengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo ikiwemo eneo
la Nyang'wale lenye hekari 996, eneo la Nyangarata lenye hekari 1074, Eneo la
Buzwagi kilometa za mraba 53.4 na eneo la Kinamyuba kilomita za mraba 33.3
Alisema kuwa jukumu la serikali ni kutatua kero za wananchi sio
kuwaongezea kero wananchi hivyo watendaji wote wa serikali wanapaswa kutimiza
ndoto ya Rais Magufuli kwa kuwatumikia wananchi kwa imani na matendo imara kwa
kuwanufaisha watumishi na rasilimali zao.
Sambamba na hayo Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko
amewataka wananchi kuendelea na uchimbaji wakati taratibu zikifuatwa
kukamilisha kumaliza mgogoro huo huku akiwahakikishia kutoondolewa tena na
endapo kama watakuwa wanahitaji maeneo mengine yaliyotengwa kwa ajili ya
wachimbaji wadogo wanapaswa kufuata taratibu za kisheria zilizoainishwa.
Awali mbunge wa Msalala Mhe. Ezekiel Maige alimweleza Mhe. Naibu
Waziri kuwa watu wake wameonewa kwa muda mrefu na yeye akifuatilia mgogoro huo
bila mafanikio.
"Ni kwasababu ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na
Rais Magufuli kwa kimbilio la wanyonge, mheshimiwa Naibu Waziri nilikua
nimekata tamaa" Alikaririwa Mhe Maige aliyekuwa akizungumza kwa hisia huku
akishangiliwa na mamia ya wachimbaji wadogo waliokisanyika kwenye mkutano huo.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment