Askofu
mkuu wa kanisa la hofan ministry hope for all natins Dr. Charles Jangalason
akizungumza na waumini wa kanisa la hofan mjini mafinga mara baada ya kufanyika
kwa ufunguzi rasmi.
NA OLIVER MOTTO
SERIKALI ya awamu ya tano imetakiwa kutowavumilia viongozi wa dini ambao wanakiuka maadili na sheria za nchi, kwa kufanya mambo yao
binafsi- kwa madai kuwa viongozi wa aina hiyo ni mbegu chafu yenye nia ya kupandikiza
uovu katika jamii.
Rai hiyo
imetolewa na askofu mkuu wa kanisa la kipentekoste la Hofan Ministry Hope For All Nations Tanzania Dr.
Charles Jangalasoni, katika uzinduzi wa kanisa la Hofan la mjini Mafinga Iringa,
ambapo Dr. Jangalasoni amesema rais Magufuli ameonyesha nia njema kwa kudhibiti tabia ya Ushoga nchini.
Aidha
Askofu Jangalasoni amesema anakerwa na baadhi ya viongozi wa dini
wanaobariki uchafu huo wa kutaka watu wa jinsia moja kuoana, na kuwa
viongozi wa dini wanapaswa kuwa mstari a mbele katika kupiga vita uovu
wa ndani na nje ya makanisa yao.
Jangalason
amesema kuwafumbia macho viongozi wa dini waovu
kunaliangamiza Taifa, na kuwa serikali ya Tanzania inapaswa kupongezwa
kwa msimamo wake huo wa kudhibiti ushoga na viashiria vyovyote vyenye
nia ya kupandikiza tabia hiyo ya ushoga ambayo ni chukizo hata mbele ya
uso wa Mungu.
Aidha
Askofu
Jangalasoni amesema serikali ya awamu ya tano imeamua kuzikataa tabia za
kimagharibi hasa ikiwemo tabia ya Ushoga, na kuwa yeye anamuunga mkono
rais Magufuli kwa ujasiri huo ambao umelenga kuliponya Taifa..
Pia
Askofu Jangalasoni amewataka viongozi wa dini kutowafumbia macho
manabii wa uongo na wale wote wanaoibuka kwa
njia za kiroho wakieneza mambo machafu yanayolichafua kanisa na Taifa,
mambo ambayo yapo nje ya maagizo ya Mungu, kwa madai kuwa viongozi hawa
wanakuja kwa njia ya kujipachika vyeo vya unabii na Utume ili
kujijengea kuaminiwa katika jamii.
Amesema
kufumbia mamcho uovu kunasababisha kuibuka kwa mitume na manabii wa
uongo akiwemo mtu aliyejiita "Nabii Tito" alikuwa na lengo lake
binafsi -ambapo askofu Dr. Jangalason ameipongeza pia serikali kwa hatua
ya haraka ya kumkamata Nabii Tito kwa madai kuwa mtu huyo alikuwa na
nia mbaya ya kuupandikiza uovu katika Taifa la Mungu.
Askofu
Jangalason amewataka maaskofu wote kuwa mstari wa mbele kukemea mambo
machafu pasipo kupoteza muda, kwakuwa mambo hayo ni chukizo mbele ya
Mwenyezi Mungu, na kuwa baadhi ya maaskofu na wachungaji hawaifanyi kwa
weredi na kusababisha kukua kwa mbegu ya uovu duniani.
Akizungumzia suala
la ujenzi- Baraka Kolowoga katibu wa kanisa la Hofan Mafinga amesema ujenzi wa kanisa la
Hofan umegharimu fedha zaidi ya shilingi Milioni 100, ambazo zilichangwa na
waumini wa kanisa hilo na hawana mkopo wala deni mahala popote juu ya ujenzi
huo.
Baraka
amesema kanisa la Hofan Ministry Hope for all Nations mjini Mafinga
ujenzi wake ulianza mnamo mwaka 2007 baada ya mchungaji Ntumigwa
Ambakisye kununua kiwanja na kujenga kanisa la Mbao ambapo ujenzi wa
kanisa la kisasa ulinza mnamo mwaka 2014 kwa nguvu ya washirika na
mchungaji huyo.
Barakla
amesema mpaka kukamilika kwa ujenzi huo wa kanisa la Hofan Mafinga,
hawana deni katika benki yoyote wala kwa mtu binafsi jambo linalowapa
nguvu ya kuitenda kazi ya Mungu kwa kuwa na imani waumini wao kupenda
neno la Mungu.
Pamoja
na mambo mengine askofu mkuu Dr. Charles Jangalasoni ameweza kumweka
wakfu kwa kumpaka mafuta ya baraka mchungaji Ntumigwa Ambakisye kuwa
Askofu, ambapo askofu Jangalason amemtaka askofu Ambakisye kujitoa
kimwili na roho kumtumikia Mungu.
2 comments:
Mungu wa Mbinguni aendelee kumtia nguvu ktk kuitete haki ya kristo Yesu.
Asikofu hongera sana ukweli usemwe
Post a Comment