Thursday, May 5, 2016

WATOTO OMBAOMBA JIJINI MWANZA WABUNI NJIA YA KUJIPATIA KIPATO.

Watoto wanaoishi Mitaani Jijini Mwanza wakiwa katika shughuli ya kufuta magari na kuomba pesa.


Wanapitia wakati mgumu Mitaani. Wanakosa malezi bora na fursa muhimu kama vile kupata elimu. Hakika wanahitaji mpango mkakati ili kunusuru ndoto zao ambazo zinapotelea mitaani. Wapo wenye ndoto za kuwa Wachezaji bora duniani, watangazaji na waandishi bora wa habari, waalimu na taaluma nyingine kede wa kede. Swali ni je; ndoto hizo zitatimia vipi?

Nawazungumzia Watoto wanaoishi Mitaani ambao wamekuwa wakionekana katika Miji na Majiji mbalimbali hapa nchini ikwemo Jijini Mwanza, wakirandaranda mitaani na hata kuishi mitaani.

Wana makwao, japo ukiwauliza kwa nini wamekimbilia mitaani, wanasema wametoroka mateso na manyanyaso kutoka kwa ndugu na walezi wao baada ya wazazi kufariki ama kutengana katika ndoa.

Wachache pia wamekuwa wakitumiwa na wazazi ama walezi wao kama sehemu ya familia kujipatia kipato kupitia shughuli ya kuombaomba mitaani.

Jijini Mwanza kasi ya ongezeko la Watoto wa Mitaani inazidi kuongezeka maradufu. Jamii mara kadhaa imekuwa ikihimizwa kutowapa watoto hao pesa kwa kuwa hali hiyo huwafanya kuona maisha ya mitaani ni matamu zaidi. Lakini hiyo si hoja tena, watoto hao sasa wamebuni njia ya kujipatia kipato ambapo wengi wao hukaa eneo la Mataa, Nyerere Road na kufanya shughuli ya kusafisha na kufuta vuti katika magari kwa minajiri ya kupata kipato.

Binagi Blog inashauri, Mkakati zaidi ufanyike ili kunusuru vipaji vya watoto hawa walio mitaani. Watoto hawa wana makwao, wakamatwe na kurudishwa walikotoka, ikishindikana katika hilo, vituo vya kulelea watoto hao vitimize wajibu wa kuwalea. Mwisho kabisa, Magereza za watoto zitumike kuwapa malezi wale watakaoonekana kichwa ngumu katika kutii moja ya mkakati utakaokuwa umepewa kipaumbele katika utekelezaji.
Watoto wanaoishi Mitaani Jijini Mwanza wakiwa katika shughuli ya kufuta magari na kuomba pesa
Imeandaliwa na BMG

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More