Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa amewahakikishia wananchi wa Monduli kuwa bado yupo nao katika kuwaletea maendeleo.
Lowassa
ambaye alikuwa mbunge wa Jimbo la Monduli karibu miongo miwili enzi
akiwa mwanachama wa CCM, alisema juzi kuwa bado atashirikiana na
wananchi wa jimbo hilo.
Lowassa alihamia Chadema na kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana.
Akizungumza
katika mahafali ya shule ya sekondari ya Irkisongo iliyopo wilayani
humo juzi, Lowassa alielezea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika
wilayani humo kwa kushirikiana na wananchi.
Alitaja
baadhi ya miradi hiyo kama maji ya kutosha mpaka miaka 20 ijayo na
hospitali kubwa ya kisasa ambayo itawafanya wananchi wengi kupata huduma
za afya bila kulazimika kwenda mjini Arusha.
Mafanikio
mengine ni pamoja na kukubaliana kuhifadhi shule za sekondari za
wasichana zilizopo Monduli ambazo ni Masai, Enyorata,Irkisongo na
Kipok.
"Bado
nitaendelea kuyahifadhi mambo ya Monduli, ntashirikiana na mbunge si
kumwangusha bali kuhakikisha maendeleo ya Monduli yanabaki palepale." Alisema
Aliwataka wazazi kuhakikisha wanaendelea kuwasomesha watoto wao licha ya kuwapo kwa shida kubwa ya ajira
Alisema wanafunzi hao na wengine wanamaliza masomo yao wakati mgumu,dunia ikiwa imebadilika.
"Wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne, cha sita na vyuo vikuu hawakutani na ajira, Ajira imekuwa tatizo kubwa."Alisema
Alisema pamoja na ukubwa wa tatizo hilo, silaha pekee wanayoweza kuwapatia watoto wao ni elimu.
"Hizi fedha, nyumba na magari yataisha na kupotea,lakini elimu itabaki vichwani."Alisema
0 comments:
Post a Comment