Jeshi
la Polisi nchini limetoa wito kwa wamiliki wa silahi kujitokeza na
kuhakiki silaha zao katika Wilaya wanazoishi kabla ya kumalizika kwa
zoezi hilo mnamo Juni 30 mwaka huu.
Hayo
yalisemwa na Msemaji wa Jeshi hilo Kamishna Msaidizi Advera Bulimba
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
“Serikali
imetoa muda wa miezi mitatu kukamilisha zoezi hili muhimu na tayari
miezi miwili imepita hivyo wale ambao bado hawajahakiki silaha zao
kuzikakiki sasa kabla ya Juni 30 ili kuepukana na usumbufu” alisema
Kamshna Msaidizi Bulimba na kuongeza kuwa:
“Natoa
wito kwa watu wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria kusalimisha
silaha hizo katika vituo vya polisi, ofisi za serikali na kwenye nyumba
za ibada na watakaofanya hivyo ndani ya muda ulipangwa hawatachukuliwa
hatua zozote za kisheria”.
Aliongeza
kuwa baada ya muda ulipangwa na Serikali kupita na wamiliki
hawajahakiki silaha zao Jeshi la Polisi nchini litaendesha operesheni
kali kuwakamata wale ambao hawakujitokeza katika zoezi la uhakiki na
hatua kali zitachukuliwa ikiwemo kufutiwa leseni na silaha zao
kutaifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Aliwaomba
ndugu wa wale walikuwa wakimiliki silaha ambao wamefariki au ni
wagonjwa wasalimishe silaha hizo katika vituo vya Polisi kwa niaba ya
ndugu zao ndani ya kipindi cha uhakiki wa silaha.
Zoezi
la uhakiki wa silaha lilianza Machi 21 mwaka huu kufuatana na sheria ya
usimamizi wa silaha na risasi ya mwaka 2015, ambapo kifungu cha 66 cha
sheria hiyo kinamtaka kila mmiliki kuhakiki kumbukumbu za silaha yake au
risasi pale anapoamriwa na mamlaka.
Lengo
la kuhakiki kumbukumbu za wamiliki wa silaha ni kupata taarifa sahihi
za wamiliki hao zitakazosaidia kubaini wale wote wanaomiliki kinyume na
sheria, kuwafahamu wamiliki waliohama na kuhamia makazi mapya,
kuwafahamu wamiliki waliofariki ili kuzuia vitendo vya uhalifu na
uvunjwaji wa amani nchini.
0 comments:
Post a Comment