NAIBU
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula,
ametaka wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika mikoa
yote washindanishwe kujua utendaji kazi wao.
Waziri
Mabula, alitoa kauli hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati
akifungua kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa shirika hilo
kilichokuwa kikijadili mipango na makisio ya mapato na matumizi ya
wizara hiyo kwa mwaka 2016/17 kabla ya kuwasilishwa bungeni.
Alisema hatua hiyo itasaidia kutambua wakurugenzi ambao wanasubiri kubebwa na wenzao kwa kushindwa kufanya kazi kwa weledi.
Alisema ujenzi na ununuzi wa nyumba unahitaji fedha nyingi, wananchi hununua nyumba kupitia mikopo kutoka benki.
"Serikali
inatambua umuhimu wa taasisi za fedha katika kusaidia ukuaji wa sekta
ya nyumba jambo ambalo hufanywa duniani kote, "alisema.
Alisema
Serikali inatambua bado kuna changamoto ya riba kubwa ya mikopo ya
nyumba inayotozwa na benki ambayo sasa ni kati ya asilimia 18 hadi 25.
Alisema
Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwamo Benki Kuu
ya Tanzania (BoT) ili kuona namna bora ya kuwezesha benki kupunguza riba
katika mikopo ya nyumba.
“Serikali
itahakikisha benki zote zinashiriki kukopesha wananchi waweze
kununua nyumba, kufanya hivi kutachochea ukuaji wa uchumi na wananchi
watatumia nyumba zao kupata mikopo ya benki kwa ajili ya kuanzisha
miradi yao ya maendeleo."
Mkurugenzi
Mkuu NHC, Nehemia Mchechu, alisema moja ya majukumu ya baraza hilo
ni kujadili mipango na makisio ya mapato na matumizi ya wizara kabla
ya kuwasilishwa bungeni.
“Serikali
imeweka msisitizo zaidi katika ukusanyaji wa mapato, kupitia kikao
hiki tutapata maoni na mikakati ya kuboresha ukusanyaji wa kodi za
ardhi,” alisema.
0 comments:
Post a Comment