Katika
kile kinachoonekana amedhamiria kuendelea kubana matumizi ya serikali,
Rais John Magufuli amekataa ombi la kuongeza fedha za ununuzi wa magari
kwa wabunge pamoja na fedha za mfuko wa bunge.
Baada
ya kuchaguliwa, wabunge walipatiwa milioni 90 za mkopo kwa ajili ya
ununuzi wa magari, lakini baadhi yao walieleza kutoridhishwa na kiasi
hicho, wakidai hakitoshelezi na kutaka kiongezwe hadi sh. milioni 120.
Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa wabunge waliwasilisha ombi kwa Rais Magufuli kuongezwa fedha lakini ombi hilo limekataliwa.
Chanzo
cha kuamini kimedokeza kuwa mmoja wa wabunge wa CCM alimkumbushia Rais
Magufuli ombi hilo wakati wa kikao cha chakula cha jioni, kilichofanyika
wiki iliyopita mjini Dodoma.
Chanzo hicho kilieleza kuwa Rais Magufuli alikataa kuwaongezea wabunge fungu hilo kwa madai kuwa serikali yake haina fedha.
Kilieleza
pia kuwa Rais Magufuli alikataa kuongeza fungu la mfuko wa jimbo kwa
kuwa serikali haina fedha huku akiwataka wabunge kufanya kazi kwa bidii.
"Rais
alisema kwa sasa hali si nzuri, amekumbana na changamoto mbalimbali na
kutuahidi kulichukua ombi letu, endapo hali itatengemaa atatuangalia kwa
sababu hata yeye analitambua hilo kwa sababu alikuwa mbunge."Kilisema chanzo hicho
0 comments:
Post a Comment