Mkazi wa Kijiji cha Natambiso, Kata ya Natta wilayani Serengeti Mkoa wa Mara,
Christopher Nyamasagi ameswekwa mahabusu kwa tuhuma za kutoa taarifa ya
uongo kuwa mjumbe mmoja mwanamke aliombwa rushwa ya ngono ili wapate
mikopo ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Alitoa madai hayo
katika mkutano wa hadhara uliofanyika Shule ya Msingi Natta Mbisso mbele
ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo.
Kabla ya kukamatwa,
Nyamasagi aliyekuwa na bahasha ya kero mkononi, alidai kuwa walichanga
fedha ili waanzishe Saccos ya kukopeshwa fedha na NSSF Mkoa wa Mara.
“Mkuu
wa Mkoa tulikamilisha vigezo vya usajili, baada ya kuchangia zaidi ya
Sh11 milioni, wakatoa elimu namna ya uendeshaji na baadaye tukafungua
akaunti mwaka 2014, tukaanza kufuatilia mikopo, tulisumbuliwa sana na
kufikia hatua ya kutuambia kama tunataka mkopo, mjumbe mmoja mwanamke
atoe rushwa ya ngono ili tupatiwe,” alidai Nyamasagi.
Wakati
mkuu huyo wa mkoa akishangazwa na madai hayo, alisimama mwanamke mmoja
wa kijiji hicho na kukanusha huku akitaka Nyamasagi awaombe radhi
wanawake kwa taarifa yake ya uongo inayolenga kuwadhalilisha.
Ndipo
Mulongo alimuagiza kamanda wa polisi wilayani hapo amkamate Nyamasagi
na kumuweka mahabusu kwa tuhuma za kudanganya. Alisema kikao hicho
kililenga kujadili kero na siyo kudhalilishana.
0 comments:
Post a Comment