Social Media Administrator wa MultiChoice (DSTV) Tanzania, Shumbana Walwa akiwa katika pozi wakati wa hafla hiyo ya siku ya Afrika ambapo wadau mbalimbali walijumuika kwa pamoja kusheherekea siku hiyo iliyofanyika usiku wa Mei 27. Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Fedha wa kampuni ya Multichoice Tanzania, Bw. Francis Senguji akiwa katika pozi wakati wa hafla hiyo ya siku ya Afrika ambapo wadau mbalimbali walijumuika kwa pamoja kusheherekea siku hiyo iliyofanyika usiku wa Mei 27. Jijini Dar es Salaam
Msanii Richie Richie akimtangaza mshindi wa DSTV
Mwanablog ya Fullshangwe, John Bukuku akishangilia baada ya kutangaza kushinda zawadi ya dikoda ya DSTV
Mwanablog ya Fullshangwe, John Bukuku akipokea dikoda yake
Mke wa msanii Sheta, Leila Yusuph 'Mama Quila' akisoma jina la mshindi
Mmiliki wa mtandao wa Wananchi, Bw. William Malecela 'Lemutuz' akitangaza jina la mshindi
Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo akikabidhi zawadi
Baadhi ya staff wa DSTV
Othuman Michuzi wa blog ya Mtaa kwa Mtaa akipokea zawadi yake wakati wa hafla hiyo ya usiku wa Afrika na DSTV.
Wadau wakisakata rhumba.
Wasanii wa kundi la NIMUJO Edutaiment wakicheza ngoma za makabila mbalimbali wakati wa hafla hiyo. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).
Kampuni
ya MultiChoice Tanzania wasambazaji wa bidhaa za DStv nchini usiku wa
Mei 26 wameweza kujumuika kwa pamoja katika kusheherekea siku ya Afrika
kwa kukutana na wadau wake Jijini Dar es Salaam na kufurahia paamoja
fahari ya Afrika.
Wadau
hao ni pamoja na wanahabari, Waendesha vipindi vya televisheni na
radio, wasanii na baadhi ya wateja ambao walijumuika kwa pamoja usiku
maalum ambao pia walipata kula na kunywa pamoja na kubadilishana mwazo.
Awali
wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo maalum, Meneja Uhusiano na Masoko wa
MultiAChoice Tanzania, Bi. Furaha Samalu alieleza kuwa, MultiChoice
wanajisikia fahari katika ushiriki wao wa kuleta mabadiliko na maendeleo
tangu kuanzishwa hapa Barani Afrika miaka 20 iliyopit huku ldngo kuu ni
kuwa na maudhui ya kila siku ya kiafrika.
Aidha,
Bi. Furaha Sumalu alibainisha kuwa, kwa kuthamini Afrika, hata chaneli
wameweka zinazolenga Afrika zikiwemo: Africa Magic, Maisha Magic Bongo,
Maisha Magic East ambapo ndani ya chaneli hizo zimekuwa na mtazamo
tofauti kuhusu Afrika hivyo watanzania na waafrika kwa ujumla ni wakati
wa kuchangamkia bidhaa bora za DSTV ilikufurahia uhondo huo wa Kiafrika
na mambo mbalimbali yanayotokea ndani ya Afrika nan je ya Afrika.
0 comments:
Post a Comment