kushoto ni meneja wa hoteli ya star com iliyoko kilolo mkoani iringa wakiwana na wafanyakazi wa hoteli hiyo wakizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani baada ya hoteli hiyo kusitisha huduma zake kwa muda
NA RAYMOND MINJA IRINGA
Wakazi na wafanyabiashara zaidi ya 2500 wanaofanya kazi ya kuuza mazao ya mbogamboga katika hotel Star Com iliyoko Kitonga wilayani kilolo mkoani Iringa wameiyomba halimashauri ya wilaya hiyo kuweza
kuifungulia hoteli hiyo kwa kile wanachodai familia zao zinakufa na njaaa huku wakiziona .
Wafanyabiashara hao wanadai hotel hiyo imefungiwa kutokana na fitina za kibiashara huku zikichochewawa kiasi kikubwa na viongozi wa halimashauri hiyo kuendekeza swala la udini linaloonekana kuitafuna
halimashauri hiyo.
Wakizungumza na wandishi wa habari waliokwenda kujionea halihalisi huku machozi yakiwatoka nje ya hoteli hiyo mmoja wa wafanyabiashara wanaofanya biashara ya mazao ya mbogamboga Shaibu Daudi anasema kuwa
wamekuwa wakitesaka kwa kukosa chakula na mahitaji ya kila siku kwa familia zao kutokana na hoteli hiyo kufungiwa
Daudi alisema kuwa kufungiwa kwa hoteli hiyo kunatokana na fitina chafu za kibiashara zinazofanywa na wafanyabiasha wanaofanya biashara inayofanana na hiyo kwani hakukuwa na sababu ya kuifungia hoteli hiyo
kwani wangeweza kufanya marekebisho waliyosema huku huduma nyingine zikiwa zinaendelea
“Huuu ni uonevu wa hali ya juu kwani katika barua waliyotuletea ni kurekebisha tails sehemu ya jiko na kupaka rangi lakinieti wanafunga biashara na kutoa notisi ya siku tano tuache kuonenana bwana familia zetu zinakufa njaa kutokana na watu wachache wanaondekeza udini tunamuomba raisi magufuli aje kutumbua hili jipu la udini linalotesa halimashauri ya kilolo kwani sisi wengine tunaonekana kama hatuna haki ”alisema daidi
Alisema kuwa ni jambo la kushangaza kuzuiwa kwa diwani wa kata hiyo na mtendaji kuingia katika kikao kilichokuwa kikijadili hatima ya kufunguliwa kwa hoteli hiyo huku viongozi wa kata ya ruaha mbuyuni ambako ndiko aliko mpinzani wao wa kibiashara wao wakiruhusiwa kuingia katika kikao hicho ili kumkandamiza kibiashara mmiliki wa hoteli hiyo
Catherine Msigwa mama wa watoto sita anayeendesha maisha yake kwa kufanya biashara ya vitungu katika hoteli hiyo anasema ni siku 5 sasa zimepita kwa familia yake kula mlo mmoja kwa siku kutokana na kukosa hela ya kununua mahitaji ya nyumbani kutokana na mali aliyonunua kuharibika kutokana na magari kushindwa kusimama katika hoteli hiyo
Msigwa alisema kuwa ni jambo la busara kwa uongozi wa wilaya hiyo kuweza kuifunulia hoteli hiyo kwani marekebisho yaliyokuwa yakitakiwa kufanyika ni madogo mno ambayo yangeweza kufanyika huku huduma nyingine zikiendelea kama kawaidaa
“Mimi sina mume watoto wananitegemea mama yangu naye ananitegemea mume wangu ndiyo hii biashara laki ndio tumefungiwa wanangu wanakula mlo mmoja kwa siku Raisi wangu Magufuli tulikuchagua ukasema utatutetea
sisi wanyonge ukuwapi babaaa tunatesekaaa mzeee njooo mzeee utukomboe” alisema
Akizungumzia sababu ya kufungiwa kwa hoteli hiyo mkurugenzi wa Star Com Henry Vegele Alisema kuwa walipokea barua ya notisi ya siku 5 kutoka katika Halimashauri hiyo ikawataka kufanya marekeisho katika
maeneo mbalimbali ikiwemo kupaka rangi katika eneo la jiko ,kuweka tails katika eneo la jiko pamoja na rekebisha miondombinu ya mitaro ya maji jambo ambalo tayari wamekwisha kulifanya .
Vegule alisema kuwa marekebisho aliyokuwa akitakiwa kuyafanya ni marekebisho ya kawaida katika hoteli yoyote na hakukuwa na sababu kubwa ya kufunga kwa hoteli hiyo kwani wamepata hasara kubwa huku wafanyabisha wadogowadogo wakishindwa kuendesha biashara zao
“Tayari tumewisha kufanya marekebisho kadogo madogo waliyotuandikia katika barua yao sasa tunasubiri wakaguzi kutoka halimashauri kuja kukagua ili kuturuhusi kuendelea na biasha kwani watu unaowaona hapa wanataka hata kuandamana lakini tumewasihi wasifanye hivyo kwa kuheshimu sheria na mamlaka husika .
Hata hivyo Vegele aliwataka wateja waliokuwa wanapata huduma katika hoteli hiyo kuwa hoteli hiyo eteendelea kutoa huduma bora na nzuri kwa wateja wake kama ilivyokuwa hapo awali .
0 comments:
Post a Comment