MBUNGE
wa jimbo la Iramba mkoani Singida Mwigulu Nchemba anakusudia
kuzindua mashindano ya kombe la Mwigulu 2016 litakaloshindaniwa na
vijana katika jimbo lake .
Nchemba ambae ni mmoja kati ya
mashabiki nguli wa timu ya Yanga alisema kuwa upo uwezekano
mkubwa wa michezo kuendelea kutoa ajira kwa vijana iwapo
watajituma zaidi katika mashindano hayo ambayo yataanzishwa jimboni
mwake kwa vijiji vyote kushiriki .
Akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu
mbali mbali za vijiji 8 vya jimbo la Iramba vikiwemo vijiji vya
Mingela,Tulia ,Dolomoni ,Ntwike na vingine wakati wa ziara yake ya
kuwashukuru wapiga kura wake ,alisema amekuwa akifanya hivyo kila
mwaka lengo ni kukuza vipaji vya vijana ila kutoa burudani baada ya
kazi.
Nchemba alisema wilaya ya Iramba na
mkoa wa Singida ni mmoja kati ya maeneo ambayo yanahistoria kubwa
katika soka la Tanzania na kuwa wapo baadhi ya vijana wanachezea
timu ya Simba wakiwa wametokea jimboni mwake na hivyo upo uwezekano
wa timu ya Singida United ambayo imepanda daraja kuweza kupata
wachezaji wazuri zaidi kutoka katika mashindano hayo.
Kwani alisema kila kijiji
kitashiriki mashindano hayo ya Mwigulu Cup na kuwa wakati wa
mashindano wachezaji wazuri kutoka kila kijiji watateuliwa ili
kuunda timu ya wilaya kabla ya kupata mchujo wa wachezaji
watakaochezea timu ya mkoa na nje ya mkoa pale inapowezekana.
Hata hivyo alishauri wachezaji
kucheza kwa nidhamu na kuacha kugombana wakati wote wa mashindano hayo
na wakubali kucheza uwanja wa nyumbani na nje . |
0 comments:
Post a Comment