Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Jackline Msongozi juzi jioni alinusurika
kipigo kutoka kwa wabunge wanawake wa UKAWA baada ya kuwaeleza kuwa
upande huo una wabunge wawili tu wenye michango ya maana ambao ni Upendo
Peneza (Viti Maalumu Chadema) na Magdalena Sakaya (Kaliua - CUF).
Akichangia
mjadala wa bajeti kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Msongozi aliishambulia kambi ya upinzani akieleza kuwa kuna mlevi mmoja
amechangia upande wa upinzani kuhusu uuzwaji wa nyumba za Serikali
wakati waliohusika na uuzwaji huo wamehamia upinzani ambao ni Waziri
Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.
Msongozi alisema hakuna mke
mwenza anayeweza kumsifia mwenzake, hivyo upinzani hauwezi kuisifia CCM
kutokana na kazi wanayoifanya.
Baada ya kusema maneno hayo na
wabunge wengine kuchangia, Bunge lilipoahirishwa wabunge wanawake wa
upinzani wakiongozwa na Sabrina Sungura na Ester Matiko walimfuata
Msongozi wakitaka kumshambulia, lakini aliondoka moja kwa moja pasipo
kusimama popote.
Sungura alipoulizwa alisema kuwa mbunge huyo angesimama wangemshughulikia.
0 comments:
Post a Comment