Monday, November 30, 2015

Rais Magufuli kaamua Bilioni zilizokua zitumike sherehe za uhuru 9 Dec matumizi yake yawe kama ifuatavyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika tarehe 09 Desemba 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami.

Tayari fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara hapa nchini TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo, linalopaswa kuanza mara moja
Akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi PATRICK MFUGALE Ikulu Jijini Dar es Salaam, Dkt. Magufuli ametaka ujenzi wa barabara hiyo uanze haraka ili kukabiliana na adha ya msongamano wa magari katika barabara hiyo

Kujengwa kwa njia hizo kutaifanya barabara ya Morroco hadi Mwenge kuwa na njia tano.
 
Wakati huo huo, Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba Ikulu Jijini Dar es salaam.

Katika Mazungumzo hayo Prof. Lipumba amempongeza Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kwa kutoa hotuba nzuri ya uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokonga nyoyo za Watanzania.

Kwa Upande wake Rais Magufuli amempongeza Prof. Lipumba kwa msimamo wake thabiti wa kupinga ufisadi na amemtakia heri katika shughuli zake.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es Salaam.
30 Novemba,2015

MBUNGE COSATO CHUMI KUTATUA TATIZO LA MAJI KATIKA MJI WA MAFINGA LILOTUDUMI KWA MUDA MREFU.

 mbunge wa mafinga mjini cosato chumi akikagua chanzo maji cha ikangafu wakati wa ziara yake ya kutembelea vyanzo vya maji na matanki ya kuhifadhia maji
 mbunge wa mafinga mjini cosato chumi akikagua moja ya tanki la kuhifadhia maji

 mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa mafinga shaibu nnunduma kulia akiwa mbunge cosato chumi wakijali jambo kwenye moja ya matank waliyokuwa wanayakagua.
kushoto ni bw uhaula ,bw shaibu nnunduma mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa mafinga wakijadili jambo baada ya kukagua baadi ya vyanzo hivyo vya maji.

mbunge wa jimbo la mafinga mjini cosato chumi amefanya ziara ya kuangalia jinsi gani anaweza kutatua tatizo la maji katika jimbo hilo.

leo mapema mbunge huyo aliongozana na wataalamu wa maji na mkurugenzi wa maji wa mafinga walifanya ziara kwenye vyanzo vya maji kwa lengo la kutatua tatizo la maji ambalo limedumu kwa kipindi kilefu.

akizungumza katika ziara hiyo chumi amesema kuwa ameamua kufanya ziara katika eneo hilo kwa lengo la kujua nini tatizo linalosababisha miji wa mafinga kuwa na uhaba wa maji.

"huwezi kutatua tatizo bila kulijua tatizo lenyewe hivyo nimelazimika kufanya ziara na kufika huku ili nijionee mwenye nini tatizo na nianze kuangalia na kupanga mikakati ya kulitatua tatizo hilo ambalo limekuwa sugu katika mji huo" alisema chumi

aidha mh chumi alisema kuwa mji wa mafinga unahitaji maendeleo hivyo moja ya mambo yanayosababisha maendeleo ni maji hivyo ni lazima kulitatua tatizo hilo mapema ili wananchi waendelee kufanya kazi na kuacha kulifikilia tatizo hilo ambalo limekuwa likiwagharimu muda mwingi wa kwenda kutafuta maji.

"leo nimekuja na wataalamu wa maji wa mji wa mafinga ili wanieleze nini tatizo kitaalamu na tutumie njia gani kulitatua tatizo hilo ndio maana unaniona nipo na hawa wataalm lengo langu ni kulimaliza kabisa tatizo la maji katika mji huu wa mafinga" alisema chumi

pia chumi amewahakikishia wananchi wa jimbo la mafinga mjini kuwa atahakikisha anatatua tatizo hilo kwa kuwa ili kuwa moja ya sera yake wakati wa kuomba kura kwa wananchi hivyo lazima atimize ahadi aliyoihaidi.

chumi amemalizia kwa kuwaomba wananchi wa jimbo hilo kumpa ushirikiano kwa jambo lolote lile analolifanya la maendeleo katika jimbo hilo na kuwaomba wawe na subira wakati anapanga mikakati ya kutengeleza ahadi zake alizozitoa wakati wa kuomba kura.

CCM yakanusha Zilizosambaa Kwamba Imekubali Kumkabidhi Maalim Seif Ikulu

Chama cha Mapinduzi CCM kimekanusha Taarifa iliyozagaa katika Mitandao ya Kijamii kwamba Chama hicho kimeridhia aliyekuwa Mgombea wa Urais wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akabidhie nchi kuiongoza kwa miaka mitano. 

Akikanusha Taarifa hiyo mbele ya Waandishi wa Habari Afisini kwake Kisiwandui Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai amesema taarifa hiyo ni uzushi uliotungwa ili kuwatia taharuki WanaCCM na Wananchi kwa Ujumla. 

Amesema toka kusambaa kwa Taarifa hiyo Jana amekuwa akipigiwa simu na Watu mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kujua ukweli wa Taarifa hiyo hasa ikizingatiwa kuwa ilidaiwa kusainiwa na Naibu huyo. “Huu ni Uzushi Mkubwa na kwamba unafaa kupuuzwa maana hauna lengo jingine zaidi ya kuwagawa WanaCCM” Alismema Vuai. 

Amesema kilichopo nikwamba CCM inajiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa Marejeo kama ambavyo Tume ya Uchaguzi ilitangaza kuufuta Uchaguzi na hivyo kurudiwa upya. Aidha Vuai amesema kuwa tayari wamewasiliana na Wanasheria wao pamoja na wataalamu mbalimbali ili kuwabaini waliohusika kusambaza Taarifa hizo na kuwapeleka katika Vyombo vya Sheria. 

“Tumeshafanya mawasiliano na Wataalam wetu na tukiwabaini Sheria ya Makosa ya mtandao itachukua nafasi yake” Alisema Vuai. 

Katika taarifa hiyo iliyosambaa na kudai kusainiwa na Vuai Ali Vuai ilisema kuwa Chama cha mapinduzi kimeridhia na kukubali kumpa nchi Maalim Seif Sharif kupitia chama chake cha Cuf kuwa ndio rais wa uchaguzi ulopita,na yeye ndio atakayeongoza serikali ya umoja wa kitaifa. 

Taarifa hiyo ilieleza kuwa CCM imekubali kushirikiana na maalim Seif katika kuongoza nchi chini ya serikali ya umoja wa kitaifa na kukubali kutoa makamo wa kwanza wa rais na nusu ya mawaziri. 
 
Vuai amerejea kauli yake kuwa mazungumzo yanayofanywa na Viongozi wa Kitaifa kwa kushirikiana na Viongozi Rais Wastaafu wa Zanzibar hayawezi kubatilisha maamuzi ya Tume ya kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita. 

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

Njia 10 Zinazotumika Kukwepa Kodi Bandari ya Dar es Salaam

Wakati Serikali ikikunjua makucha yake dhidi ya wote waliohusika katika kashfa ya kupitisha makontena 349 kwenye Bandari ya Dar es Salaam bila ya kuyalipia kodi, imefahamika kuwa idadi hiyo ya makontena ni sehemu ndogo tu ya mamia ya mizigo yanayovushwa kinyemela kila uchao na kuikosesha serikali mabilioni ya fedha.

Hata hivyo, wakati serikali ya Rais Magufuli na Waziri Mkuu wake, Kassim Majaliwa, ikiendelea kutafuta suluhu ya kudumu kuhusiana na ukwepaji kodi, imebainika kuwa kazi hiyo siyo lelemama kwani zipo njia zaidi ya tisa zinazotumiwa kukwepa kodi katika Bandari ya Dar es Salaam.

Mosi, ni kupitia mwanya utokanao na mfumo wa zamani wa malipo usiohusisha ule wa sasa wa kielektroniki, maarufu kama ‘E-Payment’. 
  
Kwamba, wafanyabiashara wengi hutumia mfumo huo wa zamani unaohusisha matumizi ya karatasi zilizojazwa kwa mkono na hivyo kuwezesha ujanja wa kubadili taarifa kwa manufaa ya mitandao ya wakwepaji wa kodi.

“Tatizo lililopo ni kwamba mfumo wa E-Payment ni mpya (umeanza Julai) na umefungwa kwenye benki moja tu iliyopo ndani ya eneo la Bandari… ule wa zamani unaendelea kutumiwa na wajanja hucheza na maandishi ya kujaza kwa mkono kuhujumu mapato ya serikali,” chanzo kimeeleza.

Njia ya pili ya kuhujumu mapato bandarini hapo, imetajwa kuwa ni ya kushirikiana na maafisa wa benki. Hii ina uhusiano mkubwa na njia ya kwanza inayohusisha matumizi ya mfumo wa malipo wa zamani usiokuwa wa kielektroniki. 
  
Mfanyabiashara anaweza kuandikiwa kodi sahihi anayotakiwa kulipa, lakini anashirikiana na wafanyakazi wa benki anayokwenda kuweka fedha kwa kuhakikisha kuwa baada ya kufanikiwa kuondoa kontena bandarini, maafisa wa benki husika husitisha malipo hayo kwa kuondoa fedha husika kwa madai kuwa fedha ziliingizwa kwenye akaunti husika kimakosa.

“Huwa kuna ushirikiano wa karibu kati ya maafisa wa benki na mfanyabiashara husika. Baada ya kontena kutolewa bandarini, hamisho la fedha (transaction) huondolewa katika mfumo kwa maelezo kuwa halikuwa sahihi,” chanzo kimedai, huku kikisisitiza kuwa ushirikiano huo huhusisha pia watu wa Bandari na TRA ambao mwishowe hugawana malipo kadri wanavyokubaliana.

Tatu, ni mwanya wa uvushaji wa makontena yenyewe yasiyolipiwa ushuru kupitia mageti maalum yanayofahamika kwa kazi hiyo, hasa geti Namba 3 ambalo chanzo kimedai ndilo linaongoza kupitisha mizigo ya ‘dili’.

“Kwa ujumla yapo mageti matano ya kupitisha bidhaa mbalimbali, baadhi yakiwa ni ya kupitihia mafuta, nafaka na magari. 
  
"Hili Namba 3 ndiyo hutumika kupitisha makontena ya bidhaa zenye thamani kubwa na wengi wasiolipa kodi hulitumia hili,” chanzo kilieleza kabla ya kufafanua kuwa awali, hilo geti Namba 3 halikuwa na mfumo wowote wa kuangalia kama kontena husika limelipiwa au la na ndiyo maana lilikuwa likitumika zaidi kupitisha makontena yasiyolipiwa kodi.

Njia ya nne ya kuhujumu kodi ya mapato ni ya kuwatumia watu wanaoendesha bandari kavu (ICD’s). Inaelezwa kuwa hivi sasa kuna bandari kavu 12, ambazo kila meli inapoingia hujulikana kila mzigo husika unapelekwa kwenye bandari ipi kati ya hizo. 
  
Hata hivyo, inaelezwa kuwa kinachofanyika ni kwa baadhi ya makontena yanayotolewa bandarini ili yapelekwe bandari kavu kabla ya kukombolewa na wahusika huishia kupelekwa kwa wafanyabiashara wenye makontena na hivyo kuikosesha mapato serikali.

“Awali kwenye ICD’s kulikuwa na askari wa mmiliki wa ICD’s na siyo wa TPA… huyu alikuwa akiangalia malipo ya bosi wake tu ambayo ni gharama za kuhifadhi mzigo na hivyo TPA na TRA huambulia patupu,”chanzi kimeeleza, kikiongeza kuwa hivi sasa walau kuna nafuu kwani kwenye ICD’s kuna walinzi wa TPA lakini hilo limefanyika baada ya watu kuwa tayari wameshaiba sana.

Njia ya tano inayotumiwa kukwepa kodi ni ya kubadili taarifa, hasa kupitia watu wenye wajibu wa kufanya tathmini. Kwamba, badala ya mzigo kukadirwaa kodi kwa kiwango sahihi, wahusika ambao zaidi huwa ni watu wa TRA hukadiria fedha kidogo baada ya kujihakikishia kuwa nao wanapewa mgawo na wafanyabiashara.

“Hapo utakuta kontena la kodi ya milioni 80, mteja anaambiwa alipe milioni 40 tu … na wakati mwingine kiasi hicho pia hakiandikwi balki huandikwa cha chini zaidi kama milioni 5 tu…hii ni njia nyingine inayoligharimu taifa mabilioni ya fedha,” chanzo kimeeleza.

Njia ya sita inayofanikisha ukwepaji kodi ni mtandao mpana wa baadhi ya vigogo wa maeneo mbalimbali Bandarini na TRA, ambao hawa huhakikisha kuwa wanakuwa na timu ya vijana wao wa kazi karibu katika kila eneo ili kufanikisha mipango yao.

“Hii ndiyo njia kubwa ya hujuma. Kama utakumbuka aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, alisambaratisha baadhi ya mitandao kwa kuwagusa vigogo 27…  ile ilikuwa kuvunja mtandao uliokuwapo. Hilo lilisaidia kiasi, lakini sasa ipo pia mitandao mingine ambayo uchunguzi ukifanyika utabaini kuwa mambo yameanza kurudi kama zamani,” imeelezwa.

Njia ya saba ya ukwepaji kodi ni kwa baadhi ya vigogo wa Bandari na TRA kuanzisha kampuni zao za uondoaji mizigo bandarini. Inaelezwa kuwa hizi hutumiwa sana kufanikisha ‘dili’ za ukwepaji kodi na ndiyo maana haishangazi kusikia kuwa kuna makontena zaidi ya 300 hayaonekani kwenye kumbukumbu za TRA.

Njia ya nane ya ukwepaji kodi ni kuonyesha kuwa kontena linapelekwa nje ya nchi, kwa mfano Malawi, wakati ukweli ni kwamba huishia hapahapa nchini.

“Utakuta kontena linadaiwa kupelekwa Malawi, lakini linachukuliwa na gari kukuu linaloonekana wazi kuwa haliwezi kufika hata Kibaha… njia hii pia hutumiwa sana kuikosesha serikali mapato,” chanzo kingine kilisema

Njia ya tisa ya ukwepaji kodi  ni ucheleweshaji wa makusudi wa utoaji makontena. Kwamba, mteja anapotaka kutoa mzigo wake kwa kufuata njia halali zilizopo, huishia kuzungushwa kila uchao ili akubali kutoa rushwa na mwishowe kulipishwa kiwango pungufu cha kodi au kulipa fedha zisizoingia kabisa kwenye mikono ya TRA.

Njia ya kumi ni ubabaishaji unaofanyika katika kuorodhesha idadi ya makontena inayotolewa bandarini kwenda kwenye bandari kavu. Hapa, kama makontena yanayotolewa ni 12, basi huandikwa kuwa ni 10 na mengine mawili huishia kuondolewa bila ya kuwa na kumbukumbu zake kwa ajili ya kulipiwa kodi.

Pamoja na kuwapo kwa njia zote hizo, chanzo kimedai kuwa sababu kubwa ya kufanikiwa kwa ukwepaji kodi ni mtandao mpana unaoundwa na vigogo mbalimbali na ndiyo maana taarifa mbalimbali za wakaguzi wa ndani na wa nje katika Bandari ya Dar es Salaam huishia kubaki kwenye makabrasha bila ya kuwapo kwa utekelezaji wowote wa vitendo juu ya yale yanayopendekezwa na wataalamu.

Chanzo: Nipashe

Sheikh Ponda Aachiwa Huru

Mahakama ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia

 Historia ya kesi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda.

Hati ya Mashitaka ya Kesi hiyo ilikuwa na jumla ya Mashitaka matatu  lakini Julai 22 mwaka 2015, Hakimu Mkazi Mary Moyo  alitoa  uamuzi wa kumfutia shitaka la kwanza kwasababu lilishatolewa uamuzi na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na hivyo mahakama hiyo ya Morogoro siku hiyo ilitoa uamuzi wa kumuona ana kesi ya kujibu  katika mashitaka mawili yaliyosalia ambalo ni kosa la pili na la tatu .

Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro  ilimfungia dhamana Sheikh Ponda baada ya kukubaliana na hati ya aliyekuwa  Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), wakati huo Dk.Eliezer Feleshi ambaye kwasasa ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam liloomba Mahakama hiyo imfungie dhamana mshitakiwa huyo chini ya Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai ya Mwaka 2002.

Hatua hiyo ya kufunguliwa kesi katika Mkoa wa Morogoro ilikuja ikiwa ni muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Agosti 19 Mwaka 2013 saa Tatu asubuhi,  kumfutia kesi ya jinai  Na.144/2013 katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano baada ya DPP kudai kuwa hana nia ya kuendelea kumshitaki katika kesi hiyo No.144/2013  kwa mujibu wa kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.

Hata hivyo baada ya hakimu Liwa kumwachilia huru,Ponda ambaye aliletwa mahakamani hapo saa 12 asubuhi na wanausalama wa polisi na magereza chini ya ulinzi mkali, alikamatwa tena na kupakizwa kwenye magari ya wanausalama hao ambapo baadhi ya wanausalama hao walisema kuwa wanampeleka Ponda mkoani Morogoro kwaajili ya kumfunguliwa makosa matatu ya uchochezi, kufanya mkusanyiko haramu na kisha akarejeshwa gereza la Segerea Dar es Salaam , lakini baadae Uongozi wa Jeshi la Magereza uliamua kumuamisha Ponda kutoka Gereza la Segerea na kumuamishia Katika Gereza Moja Mkoani Morogoro.

Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, baada ya kuwasili kwa helikopta ya Jeshi la Polisi katika uwanja wa gofu mjini Morogoro.

Akisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro, Richard Kabate, Mwanasheria Kiongozi  wa Serikali, Bernard Kongola, alidai  kuwa Agosti 10, mwaka 2013, katika eneo la Uwanja wa Ndege, Manispaa ya Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.

Alidai kuwa Sheikh Ponda ambaye anatetewa  na wakili wa kujitegemea Juma Nassor aliwaagiza waumini hao kuwa endapo watu hao watajitokeza kwao na kujitabulisha kwamba ni kamati za ulinzi na usalama za misikiti, wafunge milango na madirisha wawapige.

Ilielezwa kuwa kauli hiyo ni kinyume cha agizo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyotolewa na Hakimu Victoria Nongwa Mei 9, mwaka 2010, ambayo ilimtaka Ponda ndani ya mwaka mzima kuhubiri amani na Kuwa Raia Mwema.

Katika shitaka la pili, Kongola alidai kuwa Agosti 10, mwaka huu, katika eneo la Uwanja wa Ndege, Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu kuwa serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi ili kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi hao ni Waislamu.

Kwamba, Ponda aliwaambia wafuasi wake kuwa serikali haikufanya hivyo kwa wananchi wa Loliondo walipokataa Mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa huko ni Wakristu.

Shitaka la tatu ambalo linafafana na lile la pili, ambalo nalo linadaiwa kutendwa Agosti 10, mwaka huu, ambapo kauli ya Ponda inadaiwa kuumiza imani za watu wengine kinyume cha kifungu cha sheria namba 390 na kanuni ya adhabu namba 35 cha mwaka 2002.

Oktoba 18 mwaka 2012, Ponda na wenzie 49 walifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa Mara ya kwanza   wakikabiliwa na makosa matano, kosa la kwanza ni la kula njama, kujimilikisha mali, kuingia kwa jinai katika kiwanja cha Chang'ombe  Markas,wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh. Milioni 59 na kosa la uchochezi ambapo katika kesi hiyo Jamhuri ilikuwa ikiwakilishwa na wakili Mwandamizi wa Serikali , Tumaini Kweka .
 
Mahakama pia iliwafunga dhamana ya Ponda na mshitakiwa wa pili tangu 0ktoba 18 Mwaka 2012 hadi siku Kesi hiyo iliyotolewa hukumu Mei 9 Mwaka 2013.

Mei 9 mwaka 2013 Hakimu Mkazi Victoria  Nongwa akitoa hukumu yake katika kesi hiyo ya Ponda na wenzake alisema anawaachiria huru washitakiwa 49  kwasababu upande wa jamhuri  umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi yao na kwamba anamtia hatiani Ponda kwa kosa moja tu  la kuingia kwa jinai na kwamba na anamuachiria huru katika makosa manne yaliyosalia kwasababu pia jamhuri ilishindwa kuthibitisha mashitaka hayo dhidi ya Ponda.

Sheikh Ponda alikata rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mei 9 mwaka 2013 ambapo alishinda rufaa yake.

Hata hivyo siku Chache baada ya Kufungwa Kifungo hicho cha nje Mei 9 mwaka 2013, Ponda alikwenda Mkoani Morogoro na kufanya mkutano ambao alidai wa Kutenda makosa ya jinai ambao alikamtwa  Agosti Mwaka 2013 na kuwekwa chini ya ulinzi na kufunguliwa Kesi Mahakama ya Kisutu Na.144/2013 ikafutwa na DPP na ndipo akafunguliwa kesi hiyo Mkoani Morogoro ambayo imetolewa hukumu Leo na kuachiwa huru.

COSATO CHUMI KESHO KUTIMIZA KAULI MBIU YA HAPA KAZI TU KATIKA JIMBO LA MAFINGA MJINI

 hivi ni baadhi ya vifaa atakavyokabidhi mbuge wa jimbo hilo cosato chumi katika jimbo la mafinga mjini siku ya kesho.
 hili ni gari likishusha vifaa hivyo na baadhi ya watumishi wakisaidia kuvishusha 
 huyu ni mmoja ya wafanyakzi katika hospitali ya mafinga akiwa ameshusha kiti cha wagonjwa akipeleka sehemu inayotakiwa.

Mbunge wa jimbo la mafinga mjini cosato chumi ameanza kutimiza ahadi zake alizo waahidi wakazi wa jimbo hilo na kutekeleza kauli mbiu ya rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania dr john pombe magufuli ya hapa kazi tu.

Akizungumza na blog hii mbunge huyo amesema kesho anatarajia kutoa vifaa ya hospitali ili viweze kuwasaidia wakazi wa jimbo na kuboresha afya za wananchi wake kwa kuwa usipokuwa na afya huwezi kufanya kazi na kutimiza malengo ya kuleta maendeleo kwa kasi kubwa.

“Unajua afya ni kila kitu katika maisha ya binadamu hivyo lazima nitekeleze ahadi zangu nilizotoa wakati wa kampeni na wanachi lazima tufanye kazi kwa kujituma ili tumuunge mkono rais wetu ambaye ananiaya ya kutuletea maendeleo “aliyasema hayo wakati akiwashukuru wananchi wake mapema tu baada ya kutangazwa kuwa ni mshindi katika uchaguzi huu.

chumi amewaomba wananchi wa jimbo hilo kuunga mkono kwa kufanya kazi kwa nguvu zote ili walete maendeleo kwa pamoja maana akifanya kazi pekee yake bila wao hawezi kuleta maendeleo pekee yake.

Viongozi wa serikali katika ngazi mbalimbali wametakiwa kujituma kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza azma yao ya kuleta maendeleo katika jimbo hilo.


Kesho natajia kukabidhi vifaa ambavyo vitawasaidia wagonjwa kupata huduma inayostahili.

Chadema Yateua Meya Manispaa ya Kinondoni

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Konondoni, kimempitisha Diwani mteule wa Ubungo, Boniface Jacob (Chadema), kuwa mgombea umeya wa Manispaa ya Kinondoni, huku akiwakilisha mwamvuli wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Mgombea huyo alikuwa akiwania nafasi hiyo huku akipambana na diwani mwenzake mteule wa Kata ya Mbweni, Abdunel Elibariki (Chadema) ambaye alishindwa kutamba.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa uchaguzi huo Venus Kimei ,  alisema Jacob alishinda kwa kura 20 kati ya kura 28 zilizopigwa.

“Wagombea walikuwa wanne lakini watatu ndio ambao walikidhi vigezo, hata hivyo waliopigiwa kura ni wawili kutokana na mgombea mmoja Ndeshukurwa Tungaraza ambaye ni Diwani mteule wa Kata ya Makongo kujitoa katika hatua za mwisho,” alisema.

Akizungumza baada ya kutangazwa kushinda kinyang’anyiro hicho, Jacob alisema ana imani atashinda katika uchaguzi utakaowajumuisha wagombea wa vyama vingine kikiwamo Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Nitasimamia kwa vitendo sera ya elimu ambayo chama chetu iliisimamia katika kampeni na jambo zuri ni kwamba hata Rais Dk. John Magufuli amesisitiza kwamba watoto wasome bure kuanzia msingi hadi sekondari.

“Hivyo ninaamini hilo linawezekana endapo tutasimamia mapato ya ndani kwa umakini nataka Manispaa Kinondoni iwe mfano katika hili ambayo tutahakikisha tunaboresha maslahi ya walimu na kuondoa kabisa michango ya aina zote,” alisema.

Alisema atasimamia kwa kuzingatia sera ya utatu akijumuisha wananchi, wanasiasa na wataalam bila kuwabagua kwani kwa pamoja watainua maendeleo ya manispaa hiyo.

Kwa upande wa Chama cha Wananchi (CUF), ambacho ni mshirika wa Ukawa, kinatarajia kumsimamishwa Diwani mteule wa Kata ya Tandale, Jumanne Mbunju (CUF) ili awanie nafasi ya unaibu meya wa manispaa hiyo.

Katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni yenye majimbo manne, Chadema imenyakua majimbo matatu ambayo ni Ubungo, Kawe na Kibamba, huku jimbo moja la Kinondoni likienda CUF.

Kata zinazounda halmashauri hiyo ni 34 ambapo Chadema ilishinda kata 18 na kupata madiwani wa viti maalumu 7, CCM kata 11 na viti maalumu 4 na CUF ikishinda kata 5 na viti maalumu 2.

Lowassa, Mbowe Watua Alipouawa Alphonce Mawazo

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe  na aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho Mhe. Edward Lowassa pamoja na viongozi mbalimbali wakitazama eneo ambalo Alphonce Mawazo alifanyiwa kitendo ya kinyama cha kukatwakatwa mapanga na watu wanaosemekana ni wafuasi wa CCM ikiwa ni umbali mchache kutoka kutuo cha polisi na ofisi za CCM katika barabara kuu inayoelekea Geita kutokea Busanda.
Umati mkubwa wa wakazi wa Jimbo la Busanda waliojitokeza kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mgombea ubunge na M/kiti wa Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.
Mwili wa Marehemu Alphonce mawazo ukipokelewa na wakazi wa jimbo la Busanda ambako alikuwa akiwania Ubunge katika jimbo hilo

Waziri Mkuu: Tumedhamiria Kuwatumikia Watanzania...Tutahakikisha Mapato Ya Taifa Yanatumika Kwa Maslahi ya Watanzania Wote

WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kila kinachokusanywa kama mapato ya nchi kinatumika kwa maslahi ya Watanzania wote na si kwa manufaa ya wachache. Alitoa kauli hiyo jana mchana (Jumapili, Novemba 29, 2015) wakati akifunga maadhimisho ya miaka 20 ya Dayosisi ya Pwani ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Serikali imeanza kukabiliana na upotevu wa mapato ya Serikali na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za umma. Nia yetu ni kuhakikisha kila kinachopaswa kukusanywa kama mapato ya nchi, kikusanywe na kitumike kwa masuala ya msingi kwa ustawi wa Watanzania wote na si kwa watu wachache,” alisema.

Akifunga maadhimisho hayo kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kupambana na maovu yote na kuondoa kero zinazowaumiza wananchi wa kawaida.
 “Wako watu wanaoamini kwamba hatuwezi, nawaomba waondoe hiyo dhana. Wako watu wanaodhani kwamba kwamba utawala huu ni wa watu wapole, nao pia waondoe hiyo dhana,” alisema huku akishangiliwa na mamia ya waumini waliohudhuria sherehe hizo zilizoanza Novemba 27, 2015. 

“Tunawaomba Watanzania wote mtuunge mkono kwenye vita hii na mtuwezeshe kuifanya kazi hiyo. Tunaomba waumini wote mtuombee katika sala zenu za kila siku ili tuweze kuongoza kwa haki na kuwaletea Watanzania wote maendeleo,”
aliongeza.

Akinukuu kitabu cha Mithali sura ya 29 mstari wa pili, Waziri Mkuu alisema: “Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi, bali mwovu atawalapo, watu huugua. Mtuombee viongozi wenu tuwe waadilifu na wenye kutenda haki. Nasi tutaendelea kuwa waadilifu ili watu wetu wasigue,” alisema.

Aliwataka viongozi wa kanisa hilo waendelee kuisaidia Serikali katika kujenga kundi la watu wenye maadili mema ili walisaidie Taifa kuwa na watu waadilifu na hivyo kupunguza kero nyingi zinazoikabili jamii.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na waumini wa kanisa la hilo kutoka mikoa mbalimbali, Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT, Askofu Silas Kezakubi alisema Kanisa hilo litaendelea kumuombea Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake ili wawe na afya njema, wawe na hekima na kuahidi kwamba wataendelea kuwaweka chini ya ulinzi wa Mungu siku zote.

Alisema wao kama kanisa wanaamini kwamba Serikali ya awamu ya tano ina nia ya kuwatumikia wananchi kwa bidii na uadilifu lakini akasisitiza kuwa siri ya bidii na uadilifu inapatikana kwenye neno la Mungu.

Akisoma risala ya kanisa hilo, Askofu wa AICT Dayosisi ya Kibaha, Askofu Charles Salalah alisema kanisa halina budi kushirikiana na Serikali kwa sababu wote wanawahudumia watu walewale isipokuwa katika malengo tofauti. 

Alisema kanisa hilo linahubiri maadili mema na bidii katika kazi kwa vile linaamini kuwa maendeleo hayadondoki kutoka juu wala hayaoti kama uyoga bali yanapatikana kwa watu kufanya kazi. 
Akisisitiza kuhusu uadilifu, aliwataka wazazi kudumisha ndoa zao ili watoto wapate malezi mema kutoka kwa baba na mama na kwamba baba na mama wasipokaa vizuri, watoto hawawezi kuwa waadilifu.
 
“Wazazi tunao wajibu wa kupanda mbegu bora ya uzalendo kwa watoto wetu. Endapo tutapanda mbegu mbaya ya kuwagawa watoto wetu kwa itikadi tofauti, ni lazima tujue kuwa tutavuna tunachopanda.”

“Tukumbuke kuwa tunalo Taifa moja tu la Tanzania. Hata kama watoto wetu watakuwa na upenzi na vyama vyao, ni lazima tuwalee katika misingi ili wakue wakijua Taifa letu ni moja tu. Ndiyo maana tunaweka mkazo kwenye familia kwa sababu maadili mema yanaanzia nyumbani,”
alisisitiza.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMAPILI, NOVEMBA 29, 2015.


Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 ya Kanisa la Africa Inland Church Dayosi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015


Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akiwa meza kuu na viongozi wa kanisa la Africa Inland Church wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015.

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim majaliwa akiwasha moja ya pikipiki tatu ili kuashiria mkakati wa kueneza injili wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 ya kanisa la Africa Inland Church Dayosisi ya Pwani kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere, Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Magazeti ya Leo Jumatatu ya Leo Tarehe 30 Novemba

Sunday, November 29, 2015

HAPA KAZI TU” YAWAWEKA SAWA WAFANYAKAZI WA DAWASCO.

 Ofisa Mtendaji wa Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasco), Mhandisi Cyprian Luhemeja, akizungumza katika mkutano na wafanyakazi uliofanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Dawasco jijini Dar es Salaam kuhusu utendaji kazi wa kazi.
 Wafanyakazi wa Dawasco wakimsikiliza Ofisa Mtendaji 
Mkuu wao.


Na Mwandishi, Maalumu

Ule usemi maaarufu wa Hapa kazi tu” 

unaendelea kuimbwa na kufanyiwa kazi na watanzazia wengi hususani watumishi wa Umma na serikali ili kuendana na kasi ya awamu ya Tano ya Raisi Magufuli. Kauli mbiu hiyo imekumbushwa tena na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Eng Cyprian Luhemeja wakati wa kikao cha pamoja na  wafanyakazi wa shirika hilo mapema wiki hii.

“lazima tuendane na kasi na speed ya Mheshimiwa Rais, tabia ya kufanya kazi kwa mazoea, kutojali malalamiko ya Wateja sasa ni mwisho” aliongeza Luhemeja

Aliwataka wafanyakazi kujali muda wao wa Kazi kwa kutenda yale ambayo yataondoa kero ya Maji kwa Wateja hususani kuziba mivujo ya Maji katika maeneo mengi ya Jiji pamoja na kupambana na wizi wa Maji ili kila mwananchi apate huduma ya Maji kihalali.

Alimalizia kwa kuwataka wafanyakazi wa DAWASCO kutekeleza kauli ya Rais aliyoitoa mapema wakati akifungua Bunge katika sekta ya Maji pale aliposema “LAZIMA TUWATUE KINA MAMA NDOO KICHWANI” kwa kuhakikisha huduma ya Maji inamfikia mwananchi na kuondokana na malalamiko ya upatikanaji huduma hiyo kwa maeneo stahili.
 

Katibu Wa Wizara ambaye ni Goigoi Ajiondoe Mapema

Joto la utawala wa Rais John Magufuli limebadili utendaji kazi wa makatibu wakuu wa wizara mbalimbali waliozoea kukaa ofisini na sasa wanafanya kazi nje ya ofisi na kusikiliza kero za wananchi kwenye maeneo yao.

Wakati hilo likifanyika, Ikulu jijini Dar es Salaam imesema katibu mkuu au mtumishi yeyote wa umma atakayeshindwa kwenda na kasi na mabadiliko ya utendaji kazi katika serikali ya awamu ya tano ajiondoe.

Tamko hilo linalotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alipohojiwa jana  kuhusu kutokuwapo kwa makatibu wakuu wa wizara kadhaa kwenye ofisini zao wiki iliyopita. 
 
Makatibu wakuu wa Wizara kadhaa wamelazimika kuzifunga ofisi zao na kuelekea mikoani kusikiliza kero za wananchi.

Hali ya viongozi hao kuhama jiji na kwenda mikoani imeleta mabadiliko ya utendaji kazi wao baada ya miaka ya nyuma kuzoeleka kutumia muda mwingi ofisini na kuacha kazi za nje kufanywa na waziri, naibu au watendaji wengine.

Baadhi ya wizara ambazo zilitembelewa na kukuta ofisi za katibu mkuu zikiwa zimefungwa ni Uchukuzi, Tamisemi, Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano na Ujenzi.

Baadhi ya wafanyakazi wa wizara hizo ambao hawakutaka majina yao yatajwe, walisema mabosi wao kwa sasa inakuwa nadra kuonekana ofisini wakifanya kazi kwa kuogopa kuonekana wazembe.

"Hatujawahi kuona katibu anakwenda mikoani kama ilivyo sasa, kila siku anakwenda huku na kule kuangalia miradi na kero za wananchi," alisema mmoja wa wafanyakazi wa moja ya wizara  hizo.

Hatuna Muda na Katibu Mkuu Goigoi-Sefue
Akitoa kauli ya serikali, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema kuanzia sasa katibu Mkuu na mtendaji wa serikali ambaye anafanya kazi kwa kusuasua ajiondoe mwenyewe.

Alisema tayari amefanya kikao na makatibu wote kuwaeleza suala hilo na atakayerudi nyuma hatakuwa na nafasi katika serikali ya awamu ya tano.

"Jambo hilo tumekubaliana kwenye kikao, serikali ya awamu ya tano haitakuwa na utani kwa wale watakaoonekana hawaendi na kasi ya Rais, sasa wanatakiwa kuchagua kama wanataka kuendelea na nafasi  zao au la," alisema Sefue

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More