Tuesday, June 17, 2025

TFS YAJIDHATITI KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO MSITUNI

Baadhi ya vijana wakipewa mafunzo ya utimamamu wa mwili kwa ajili ya kulinda na kuzuia mtoto usiharibu miti ya mashamba ya miti Sao Hill.Baadhi ya vijana wakipewa mafunzo ya utimamamu wa mwili kwa ajili ya kulinda na kuzuia mtoto usiharibu miti ya mashamba ya miti Sao Hill.Baadhi ya vijana wakipewa mafunzo ya utimamamu wa mwili kwa ajili ya kulinda na kuzuia mtoto usiharibu miti ya mashamba ya miti Sao Hill.





Na Fredy Mgunda,Mufindi

Ikiwa ni kuelekea msimu wa kipindi cha kiangazi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill umeendesha zoezi la usahili kwa watumishi wa muda watakaounda kikosi maalumu kwa  ajili ya kupambana na kudhibiti majanga ya moto katika maeneo yanayolizunguka Shamba.


Zoezi hilo limefanyika leo Juni 16, 2025 katika viwanja vya Shamba la Miti Sao Hill likishirikisha wahifadhi wa Shamba, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Jeshi la Polisi, likilenga kupata vikosi vitakavyohudumu katika Makao Makuu ya Shamba pamoja na Tarafa ya II ya Shamba Ihefu.


Akizungumza katika zoezi hilo Mhifadhi Mwandamizi anayesimamia Utumishi na Utawala Felista Bayo amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 Shamba linatarajia kuajiri watumishi wa muda 192 kwa ajili ya kukabiliana na kupambana na majanga ya moto kwa kipindi chote cha kiangazi.


Ameongeza kuwa licha ya maombi kuwa mengi kulinganisha na nafasi zilizotajwa, Shamba la Miti Sao aaHill lina shughuli nyingine zinazoendelea katika vituo vyake vyote ikiwa ni pamoja shughuli za bustani na usafi wa mashamba, hivyo wanaokosa nafasi katika vikosi hivyo wanapata fursa ya kuendelea na shuguli nyingine za Shamba.


Kwa upande wake Mhifadhi anayesimamia Kitengo cha Ulinzi wa Msitu dhidi ya moto Murya Sawa amesema kuwa baada ya kukamilisha zoezi hili ni matarajio ya TFS kupitia Shamba la Miti SaoHill kuwa watumshi hawa muda  waliopata nafasi watafanya kazi hiyo kwa weledi kwa kutanguliza uzalendo huku akihimiza ushirikiano baina ya wananchi wote wanaoishi karibu na maeneo ya hifadhi katika kulinda rasilimali za misitu.


Naye Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Mufindi Ashery Kitundu amesema kuwa lengo mama la jeshi la zimamoto ni kuhakikisha matukio ya moto hayatokei kwa kutoa elimu, na kuyadhibiti pindi yanapotokea hivyo ni watumishi hawa wa muda watakuwa mabalozi wazuri katika maeneo yao waliyotoka kwa kushirikiana na jeshi la zimamoto katika kutoa elimu ya kuepuka na kukabilina na majanga ya moto.


Usaihili huo unatarijiwa kuendelea hapo kesho katika Tarafa ya Kwanza ya  Shamba Irundi kisha Tarafa ya Tatu Ihalimba, na Tarafa ya Nne Mgololo.

Thursday, June 12, 2025

VIJANA FANYENI MAZOEZI MARA KWA MARA KUIMARISHA AFYA

Katika ulimwengu wa leo unaokumbwa na changamoto nyingi za kiafya, viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Lindi wametoa wito maalum kwa vijana na wananchi wote kufanya mazoezi mara kwa mara kama njia ya kuimarisha afya na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza. Wito huo umetolewa wakati wa maonyesho ya madini yanayoendelea katika viwanja vya madini wilayani Ruangwa.Katika ulimwengu wa leo unaokumbwa na changamoto nyingi za kiafya, viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Lindi wametoa wito maalum kwa vijana na wananchi wote kufanya mazoezi mara kwa mara kama njia ya kuimarisha afya na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza. Wito huo umetolewa wakati wa maonyesho ya madini yanayoendelea katika viwanja vya madini wilayani Ruangwa.Katika ulimwengu wa leo unaokumbwa na changamoto nyingi za kiafya, viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Lindi wametoa wito maalum kwa vijana na wananchi wote kufanya mazoezi mara kwa mara kama njia ya kuimarisha afya na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza. Wito huo umetolewa wakati wa maonyesho ya madini yanayoendelea katika viwanja vya madini wilayani Ruangwa.



Na Fredy Mgunda,Lindi.

Katika ulimwengu wa leo unaokumbwa na changamoto nyingi za kiafya, viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Lindi wametoa wito maalum kwa vijana na wananchi wote kufanya mazoezi mara kwa mara kama njia ya kuimarisha afya na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza. Wito huo umetolewa wakati wa maonyesho ya madini yanayoendelea katika viwanja vya madini wilayani Ruangwa.

Viongozi hao wamebainisha kuwa afya njema siyo tu msingi wa maisha bora, bali pia ni mtaji muhimu kwa maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla.

“Afya bora ndiyo msingi wa maisha na maendeleo ya mtu binafsi na taifa. Tunapaswa kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi kila wakati ili kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali,” walisisitiza viongozi hao.

Mazoezi ya mwili yameelezwa kuwa na faida lukuki ikiwa ni pamoja na kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo, kisukari, shinikizo la damu na unene uliopitiliza. 

Kwa vijana, mazoezi husaidia katika kujenga miili imara, kuimarisha uwezo wa kujifunza na kujiamini, na pia kupunguza msongo wa mawazo.

Pamoja na kutoa wito wa mazoezi, viongozi hao waliwahamasisha wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi katika maonyesho ya madini yanayoendelea, kwani yameleta fursa nyingi za kiuchumi na kielimu kwa wakazi wa Lindi na maeneo jirani.

 Maonyesho hayo yanalenga kuinua sekta ya madini kwa kuonesha teknolojia mpya, mbinu za usindikaji, pamoja na fursa za uwekezaji katika rasilimali za madini.

Kwa kuzingatia mchango mkubwa wa vijana katika maendeleo ya taifa, viongozi hao wamehimiza kuwa ni muhimu kwa vijana kuwekeza katika afya zao kupitia mazoezi na pia kutumia fursa kama hizi za maonyesho kupata maarifa yatakayowasaidia kuinua maisha yao na ya jamii kwa ujumla.

Mazoezi ya mwili ni njia rahisi na ya gharama nafuu ya kujilinda dhidi ya maradhi na kuimarisha afya. Viongozi wa Mkoa wa Lindi wameweka wazi kuwa ni wajibu wa kila mmoja, hasa vijana, kuchukua hatua na kuwa mabalozi wa afya bora kupitia mazoezi ya mara kwa mara. 

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI ZANZIBAR AZINDUA MAONYESHO YA MADINI LINDI

Waziri wa Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Shaibu Hassan Kaduara, amezindua rasmi awamu ya pili ya Maonyesho ya Madini (Lindi Mining Expo) mkoani Lindi, yakilenga kuvutia wawekezaji na kutangaza fursa mbalimbali za rasilimali madini zinazopatikana mkoani humo.
Waziri wa Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Shaibu Hassan Kaduara, amezindua rasmi awamu ya pili ya Maonyesho ya Madini (Lindi Mining Expo) mkoani Lindi, yakilenga kuvutia wawekezaji na kutangaza fursa mbalimbali za rasilimali madini zinazopatikana mkoani humo.
Waziri wa Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Shaibu Hassan Kaduara, amezindua rasmi awamu ya pili ya Maonyesho ya Madini (Lindi Mining Expo) mkoani Lindi, yakilenga kuvutia wawekezaji na kutangaza fursa mbalimbali za rasilimali madini zinazopatikana mkoani humo.
Waziri wa Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Shaibu Hassan Kaduara, amezindua rasmi awamu ya pili ya Maonyesho ya Madini (Lindi Mining Expo) mkoani Lindi, yakilenga kuvutia wawekezaji na kutangaza fursa mbalimbali za rasilimali madini zinazopatikana mkoani humo.

Na Fredy Mgunda, Ruangwa, Lindi.


Waziri wa Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Shaibu Hassan Kaduara, amezindua rasmi awamu ya pili ya Maonyesho ya Madini (Lindi Mining Expo) mkoani Lindi, yakilenga kuvutia wawekezaji na kutangaza fursa mbalimbali za rasilimali madini zinazopatikana mkoani humo.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Kaduara alisema thamani ya dhahabu imeendelea kupanda katika soko la dunia kutokana na athari za vita kati ya Urusi na Ukraine, ambako dhahabu inayozalishwa na Urusi imewekewa vikwazo kuingia katika masoko ya kimataifa.


"Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya 1996, pamoja na Sera ya Maendeleo ya Viwanda ya 1996–2020 na ile ya Viwanda Vidogo ya mwaka 2003, zipo kwenye mchakato wa kupitia upya kwa lengo la kuendana na mahitaji ya sasa ya maendeleo ya kimkakati," alisema Kaduara.


Waziri huyo alibainisha kuwa miradi ya madini ni miongoni mwa miradi ya kimkakati nchini, ambayo inaendelea kufanyiwa tathmini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sera mpya itakayowezesha Watanzania kunufaika zaidi na sekta hiyo.


Lindi Yajitokeza Kama Kitovu cha Madini Nchini

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Zainab Telack, alisema mkoa huo umebarikiwa kuwa na rasilimali kubwa za madini ambazo tayari zimeanza kuwanufaisha wananchi moja kwa moja.


“Maonyesho haya yanafungua milango kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Yanachochea uchumi wa eneo hili na kuongeza thamani ya madini tunayochimba,” alisema RC Telack.


Aliongeza kuwa maonyesho ya awamu ya kwanza mwaka 2023 yalivutia wageni kutoka mataifa 14 na zaidi ya watu 6,000 walihudhuria, jambo lililoongeza hadhi ya Lindi kama eneo la kimkakati kwa shughuli za madini nchini.


“Kwa sasa tunaona ongezeko la wawekezaji, uboreshaji wa miundombinu na fursa za ajira, hali inayodhihirisha kuwa Lindi ni sehemu muhimu katika ajenda ya maendeleo ya taifa,” aliongeza.


Ongezeko la Wachimbaji na Teknolojia ya Uchimbaji

Kwa mujibu wa Mratibu wa Maonyesho hayo, Bw. Mwinjuma Mkungu, ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi mkoani Lindi, idadi ya wachimbaji imeongezeka kutoka 2,265 hadi 2,948 baada ya maonyesho ya kwanza, huku mitambo ya kisasa ya uchimbaji ikiongezeka pia.


“Tumeona ongezeko kubwa la wawekezaji na mapato ya serikali yameongezeka kwa asilimia 10.1 baada ya maonyesho ya awali. Hii inaonyesha mchango wa moja kwa moja wa maonyesho haya kwa uchumi wa taifa,” alisema Mkungu.


Alfred Chilumba, mchimbaji mdogo, alishuhudia mabadiliko makubwa baada ya kupata elimu kupitia maonyesho ya awali.


“Tulikuwa hatujui kama tunaweza kutumia mitambo ya kisasa. Maonyesho haya yametufungua macho,” alisema.


Anna Milanzi, mama lishe anayehudumu kwenye maonyesho hayo, alisema ametumia fursa ya ongezeko la wageni kuongeza kipato chake.


“Kwa siku za kawaida napika kilo 5 za unga, lakini leo nimepika kilo 15. Biashara imenoga,” alisema kwa furaha.


Maonyesho Yadumu kwa Siku Kadhaa

Maonyesho hayo ya siku kadhaa yanahusisha maonesho ya bidhaa za madini, teknolojia mpya za uchimbaji, warsha za kitaalamu, na majadiliano baina ya serikali, wawekezaji na wachimbaji wadogo.


Yamebeba kauli mbiu: “Madini na Uwekezaji wa Fursa za Kiuchumi Lindi – Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025”, yakisisitiza uhusiano kati ya maendeleo ya sekta ya madini na ushiriki wa wananchi katika mustakabali wa taifa.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More