katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa Elisha Mwampashi wa pili
kulia akiwa na katibu mkuu wa UVCCM
Taifa Bw Sixtus Mapunda
na fredy mgunda,iringa
Akizungumza na mtandao huu katibu wa uvccm mkoa wa iringa ELISHA MWAMPASHE alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wakibweteka kwa kutojituma kufanya kazi na kuendelea kuilaumu serikali.“Eti asubuhi unawakuta vijana wamekaa kwenye vijiwe wakizungumza siasa na kucheza mabao wakati hawajui mchana watakula wapi na jioni watarudi na nini nyumbani”alisema ELISHA MWAMPASHEELISHA MWAMPASHE ameendelea kuwaomba vijana wengi wenye fursa ya kurudi au kuingia shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi wengi kutokana na mabadiliko...