mwenyekiti wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) manispaa ya Iringa Ashura Jongo akiwa na viongozi wengi wameazimisha miaka arobain na moja (41) kwa kufanya usafi katika kituo cha afya cha ngome pamoja na kugawa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa
Huyu ni mmoja ya wanawake wa umoja wa chama cha mapinduzi CCM waliokuwa wakitoa zawadi kwenye kituo cha afya cha Ngome kata ya Kihesa manispaa ya Iringa
Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) manispaa ya Iringa wameazimisha miaka arobain na moja (41) kwa kufanya usafi katika kituo cha afya cha ngome pamoja na kugawa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa ambalo wamelazwa katika kituo hicho kwa lengo la kuwafikia na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi
Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) manispaa ya Iringa wameazimisha miaka arobain na moja (41) kwa kufanya usafi katika kituo cha afya cha ngome pamoja na kugawa zawadi mbalimbali
Na Fredy Mgunda,Iringa.
UMOJA
wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) manispaa ya Iringa wameazimisha miaka
arobain na moja (41) kwa kufanya usafi katika kituo cha afya cha ngome pamoja
na kugawa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa ambalo wamelazwa katika kituo hicho
kwa lengo la kuwafikia na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.
Akizungumza
wakati wa kufanya usafi na kugawa zawadi,mwenyekiti wa umoja huo Ashura Jongo
alisema kuwa anaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kufanya kazi kwa
kuwafikia wananchi wa chini hasa wale wanyonge kwa kutimiza kile ambacho
kilikuwa kimeahidiwa wakati wa kuomba kura za kuongoza nchi.
“Kiukweli
naomba nichukue nafasi hii kumpongeza sana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kuwa
anafanya kazi kubwa sana kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua ya kimaendeleo
hivyo ni lazima tuonge mkono juhudi hizi” alisema Jongo
Jongo
alisema kuwa serikali imefanikisha kuleta mabadiliko ya haraka katika sekta ya
afya tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea
kufanya kazi kwa kujituma ili kuunga mkono juhudi hizi.
“Najua
kuwa mnaona kwa macho yenu kiasi gani serikali ya wamu ya tano jinsi gani
huduma za afya zilivyo boreshwa na lazima tujivunie hiki kinachofanywa na Rais
wetu,mimi binafsi naunga mkono juhudi hizi na ninaomba wananchi nao waunge
mkono juhudi hizi” alsema Jongo
Jongo alisema kuwa kuongezaka kwa hospital za
rufaa kwenye mikoa,vituo vya afya kwenye kata au tarafa, zahanati kwenye vijiji
na mitaa ni hatua kubwa ya kimaendeleo hivyo ndio serikali ya awamu hii
inavyotekeleza vilivyo ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi 2020.
“Nyie
ni mashaidi kuwa zamani tulikuwa tunaishia kuwa na hospitali za mikoa tu lakini
kwa sasa mambo yamebadilika kila kitu kinazidi kuwa kwenye ubora unaostahili
kuwahudumia wananchi waliotuweka madarakani” alisema Jongo
Lakini
sio afya tu hata ukiangalia saizi tunapata elimu bure ambayo inamwezesha kila
mwanafunzi kusoma bure na kuhakikisha tunapunguza wimbi la wanafunzi kukosa
elimu ambapo inasaidia kuwa nakizazi cha wasomi hapo baadae.
Naye
mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa umoja huo Devota Chaula alisema kuwa
wanawake wengi wanakumbuna na changamoto mbalimbali hasa kukosa mikopo midogo
midogo hivyo serikali ya awamu ya tano hivyo inatakiwa kuangalia kwa jicho la
tatu kutusaidia kupata mikopo hiyo.
“Wanawake
wanafanya kazi kwa umoja sana hivyo kukosa mikopo kuasababisha kuduma kwa
kipato cha kukuza uchumi wa mtu moja moja na taifa kwa ujumla hivyo ukifanikiwa
kumweza mwanamke basi umewawezesha wananchi wote hapa nchi” alisema Chaula
Chaula
alisema kuwa watanzania wanatakiwa kubadili kwa kuacha kuishi kimazoea hivyo
wanatakiwa kuendana na kasi ya serikali ya awmu ya tano kwa kufanya kazi kwa
kujituma ili kukuza vipato vyao.
Kwa
upande mratibu wa afya ya uzazi na mtoto Sezalia Endru aliwashukuru viongozi
hao wa umoja wa wanawake wa ccm manispaa ya Iringa kwa kuwatembelea na kufanya
usafi na zawadi walizozitoa kwa watumishi na wagonjwa waliokuwepo muda huo.
“Tunaomba
mtufikishe salamu kwa Rais wa serikali ya awamu ya tano kwa kazi kubwa
anayoifanya kwa kuboresha sekta ya afya kwa kuwa hali ya sasa kila kitu
kinaenda kwa wakati” alisema Endru
0 comments:
Post a Comment