Na,Joel Maduka,Chato.
Mkazi wa
kijiji cha Minkoto Wilaya ya Chato Mkoani Geita Bw Hoja Kasumbakabo ( 25)
anatuhumiwa kumuua mke wake Spensioza Petro (22) kwa kumchoma na kitu chenye
ncha kali mwilini na kisha kumnyonga mtoto Brison Hoja mwenye umri wa miezi mitatu
kisha kutokomea kusikojulikana.
Mwenyekiti
wa kijiji hicho Bw Leo Nkwabi amesema tukio hilo limetokea tarehe 24 mwezi januari
kuamkia tarehe 25 kwenye kijiji hicho ambapo ilibainika miili kuonekana chini
ya Sakafu ndani ya chumba walichokuwa wanaishi huku mwili wa mwanamke huyo
ukiwa na majeraha sehemu ya kooni, mgongoni na tumboni huku utumbo ukiwa nje.
Mzazi wa
marehemu Mzee Petro Lusaga ameelezea kusikitisha na tukio hilo na kwamba hakuwahai
kuwaona marehemu na mumewe wakiwa na ugomvi kwani kwa kipindi chote walikuwa
wakiishi kwa amani bila ya kuwa na
malumbano wala kelele zozote ndani ya familia yao.
Bi,Judy
Masanja ambaye ni jirani wa karibu wa familia hiyo alisema na yeye ameshangazwa
na kifo hicho kwani hawakuwai kuwa na ugomvi na siku hiyo walikuwa wamekaa nje
na walikuwa wakizungumza vizuri tu hivyo hata yeye kifo kimekuacha na maswali mengi ya
kujiuliza.
Kwa upande
wake Diwani wa Kata hiyo, Bw Geroge Magezi amewataka wananchi kuimarisha ulinzi na kuisaidia serikali
kumtafuta mtuhumiwa huku akisisitiza wanaume kuacha mauaji ya namna hiyo.
Dr Masanja
Mchanganya anayetokea kituo cha afya cha Bwanga amethibitisha tukio hilo ambapo
katika uchunguzi walioufanya wamegundua kuwa marehemu alikuwa na majerahaa
matatu makubwa
0 comments:
Post a Comment