Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa katika ziara
ya kukagua miradi inayofanywa na wanufaika wa Mfuko wa kusaidia kaya masikini
(TASAF) akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdalah na viongozi wengine wa halshauri ya wilaya ya Kilolo
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa katika ziara ya kukagua miradi inayofanywa na wanufaika wa Mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASAF) wakiwa kwenye moja ya nyumba ya mnufaika upande wa kushoto ndio nyumba mpya iliyojengwa na upande wa kulia nyumba ambayo mnufaika anaishi
Nyumba ya kushoto inayoonekana ndio nyumba inajengwa na mnufaika na hii ya kulia ndio nyumba anayoishi mnufaika wa TASAF wilayani kilolo
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa katika ziara ya kukagua miradi inayofanywa na wanufaika wa Mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASAF) akiwa kwa mnufaika wa TASAF kukagua anafanya nini baada ya kupata pesa za TASAF
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa katika ziara ya kukagua miradi inayofanywa na wanufaika wa Mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASAF) akiwa kwenye moja ya nyumba za mnufaika wa TASAF
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa katika ziara ya kukagua miradi inayofanywa na wanufaika wa Mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASAF) akiwa na viongozi wa wilaya ya Mufindi wakati wa kuwa tembelea wananchi wanaonufaika na mfuko wa TASAF
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilya ya Mufundi Daud Yassin alikuwepo kwenye ziara ya kukagua miradi ya TASAF jinsi gani inawanufaisha wananchi
Nyumba ya juu ndio nyumba iliyojengwa kwa kutumia pesa za mfuko wa TASAF na nyumba ya chini ndio nyumba aliyokuwa anaishi mnufaika wa TASAF
Na
Fredy Mgunda, Iringa.
MKUU
wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amemaliza ziara ya kukagua miradi inayofanywa
na wanufaika wa Mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASAF) kwa kujionea changamoto
zilizopo na mafaikio makubwa ambayo wanufaida wamepata katika wilaya zote za
mkoa wa Iringa.
Akizungumza
wakati wa ziara hizo Masenza aliwapongeza wanufaika kwa juhudi kubwa
wanazozifanya kuhakikisha kuwa wanatumia vizuri pesa wanazipata kwa kufanyia
vitu vya kimaendeleo.
“Nimeona
juhudi zenu za kazi mnavyofanya na nimeamini kuwa TASAF imeinua maisha ya
wananchi walikuwa na kipato cha chini na imani yangu kuwa biashara mnazozifanya
zitakuwa na faida hapo baadae” alisema Masenza
Masenza
aliongeza kuwa wanufaika wa TASAF wamejenga nyumba nzuri tofauti na walipokuwa
wanaishi hapo awali naomba juhudi hizo ziendelee maana hapo watakuwa wamejiokoa
kwenye swala la kuwa na makazi bora tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
“Jamini
kweli maisha ya wanufaika yanabadilika angalia nyumba walikuwa wanaishi awali
nah ii ya sasa hapa ndio ambapo hata Rais wetu akiona hivi atafurahi sana maana
anaona matunda ya pesa anayoitoa kwa wananchi wake” alisema masenza
Aidha
Masenza aliwapongeza wanufaika wote ambao wanafuga mifugo mbalimbali ya
kibiashara kwa kuwa hiyo inatakuwa njia mbadala kwa maisha ya baadae hasa
kipindi ambacho serikali itaacha kuttoa tena hizo pesa.
“Nawaomba
endeleeni kufanya biashara,kulima na kufuga hiyo itakuwa njia nzuri ya
kujiongezea kipata kwa maisha yenu na vizazi vyenu hivyo msikate taama kabisa
kina mtu anaanzia chini na kwenda juu hivyo naomba mpambane kuhakikisha mnaishi
maisha bora” alisema Masenza
Lakini
Masenza aliwataka wataalam kufika kwa wanufaika na kuwapa elimu ya juu miradi
wanayoifanya ya kimaendeleo kwa ajili ya kuboresha kipata cha kaya yao.
Nao
wanufaika wa mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASAF) mkoani iringa wameipongeza
serikali kwa kuinua maisha kwa kuendelea kuwasaidia kwa kuwapa elimu ya
ujasiliamali na kujua kutuzitumia vizuri pesa wanazozipata kwa kufanyia biashara.
Wakizungumza
na blog hii wanufaika wa TASAF wamesema kuwa pesa ya TASAF imewasidia kufanya
biashara mbalimbali ambazo zimewasidia kujikwamua kiuchumi
Nao
baadhi ya wanafunzi wanaonufaika na TASAF
wameishukuru serikali kwa kufanikisha kuwasomesha kwa kupata mahitaji
yote yanayohitajika shuleni.
MASENZA
amewataka wanufaika kuitumia vizuri pesa wanayoipata kutoka TASAF kwa kuifanyia
biashara kwa faida ya maisha ya baadae.
0 comments:
Post a Comment