Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akimuomba Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi ,Isack Kamwelwe kutatua changamoto ambayo imeendelea kuwepo kwenye baadhi ya maeneo katika Mkoa huo. |
Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi ,Isack Kamwelwe akikagua baadhi ya miradi ya maji kwenye kijiji cha imalabupina wilayani chato. |
Na,Joel Maduka,Geita.
Waziri wa
maji na Umwagiliaji Mhandisi ,Isack
Kamwelwe amewataka wakandarasi wa miradi mbalimbali ya maji kukamilisha miradi
hiyo kwa wakati ili kuwaondolea wananchi changamoto ya
ukosekanaji maji ambayo imeendelea
kuwakabili kwa muda mrefu .
Mhandisi Kamwelwe ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani Chato Mkoani Geita iliyokuwa na lengo la
kukagua miradi ya maji inayotekelezwa wilayani
humo.
Akizungumza
na wananchi wa Kata ya Katoro na Buseresere amesema matatizo ya maji katika
miji ya Muganza, Buzirayombo na Buseresere yataanza kufanyiwa kazi na pindi tu
usanifu wa mradi huu utakapokuwa tayari miradi hiyo itaanza kutekelezwa ili
kumaliza kero kubwa ya maji.
Isack Saimon
ambaye ni mkazi wa Buseresere amemuomba waziri kuharakisha zaidi mradi huo
ambao ametoa ahadi kwa wananchi hao kwani kwasasa wameendelea kupata shida
kubwa ya kupata maji na kwamba wamekuwa wakinunua ndoo ya maji kwa shilingi
elfu moja hali ambayo inasababisha wasio na uwezo kushindwa.
Mkuu wa Mkoa
wa Geita,Mhandisi Gabriel Luhumbi amewasisitiza wakandarasi wote wa miradi ya maji kutumia vibarua kwa
wananchi wa maeneo husika ambapo miradi hiyo inatekelezwa.
Katika Wilaya ya Chato jumla ya wananchi ambao
wamekuwa wakuipata maji safi na salama ni ni asilimia 41.
0 comments:
Post a Comment