Thursday, January 25, 2018

RC MASENZA: WATENDAJI ACHENI SIASA KAZINI FANYENI KAZI ZA KIMAENDELEO

 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina masenza akiongea na maafisa watendaji wa wilaya ya kilolo kwa lengo la kuhimiza ufanyaji kazi wao kwa kutatua changamoto za wananchi na hatimaye wapate maendeleo
pichani ni baadhi ya maafisa watendaji wa vijiji,kata na tarafa waliohudhuria kikao hicho cha mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza



Na Fredy Mgunda, Iringa.

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amewataka watendaji wote wa serikali kuacha kufanya kazi kwa mihemuko ya kisiasa kwa kuwa linarudisha maendeleo nyuma.
 
Onyo hilo limetolewa wakati wa kikao na maafisa watendaji wa wilaya ya Kilolo,Masenza alisema kuwa imebuka tabia ya viongozi wa serikali kujihusisha na siasa wakati wa utendaji wao wa kazi hivyo kuanzia saizi zitaki kusikia siasa wakati wa kazi.

“Haiwezekani kila siku mnafanya siasa tu huko vijijini badala ya kutengeneza mpango kazi wa kimaendeleo ambao utakuwa na faida kwa taifa na wananchi wote hivyo kuanzia leo sitaki kusikia tena hiyo tabia” alisema Masenza

Masenza alisema serikali ya awamu ya tano inataka watu wafanye kazi hivyo wakati siasa hakuna tena kama kuna viongozi wanataka siasa wasubili wakati ukifika watafanya hizo siasa.

“Jamani rais wetu ameshasema kuwa huu sio wakati wa porojo za kisiasa huko makazini hivyo mnapaswa kufanya kazi na sio kupiga siasa fanyeni kazi kwa nguvu zote kuhakikisha mnatatua kero za wananchi katika maeneo yenu husika” alisema Masenza

Masenza alisema kama kuna mtendaji wa serikali anataka kufanya kazi za kisiasa basi hana budi kuachia nafasi yake ya kazi ili akaendelee kufanya kazi ya siasa na nafasi yake itajazwa na viongozi ambao wapo tayari kufanya kazi na serikali ya awamu ya tano.

Aidha Masenza aliwaagiza wakurugenzi wote mkoani Iringa kuwachukulia hatua za kisheria mara moja viongozi wa serikali watakuwa wanajishughulisha na maswala ya kisiasa la sivyo wao ndio watachukuliwa hatua kwa kufuata miongozo ya kiserikali inavyoagiza.

“ wakurugenzi mnawajua sana hawa watendaji hivyo ni lazima muwadhibiti kufanya siasa wakati wa kazi na mnatakiwa kuwa wakali pindi mtakapogundua kuwa wanafanya siasa makazini” alisema Masenza

Naye katibu tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu alisema kuwa ameshatoa walaka unaonyesha majukumu ya watendaji wa serikali hivyo hategemee kuona kiongozi wa serikali akifanya siasa kazini.

“Jamani nimetuma na kuwa walaka wa majukumu yenu hivyo sitegemie mnakiuka la sivyo nitaanza kuwa sughulikia kiongozi mmoja mmoja ili nikomeshe tatizo la siasa makazini” alisema Ayubu

Ayubu aliwataka makatibu wa wilaya kufanya kazi kwa kufuata miongozo ya serikali la sivyo serikali haitafikia malengo ya kuleta maendeleo kwa wananchi kama ambavyo wamejipangia hivyo inapaswa  kila mmoja anafanye majukumu yake kikamilifu ili kutimiza malengo ya serikali.

“Rais wa awamu ya tano DR John Pombe Magufuli hataki tufanye kazi kimazoea kama ambavyo ili kuwa awali saizi ni kazi tu hivyo ni lazima kufanya hivyo” alisema Ayubu

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More