Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina
Masenza ameipongeza kampuni ya Asas ya mkoani Iringa akiwa kwenye moja ya shule ya sekondari wakati wa ziara yake ya kimkati ya kutatua changamoto za shule.
Na Fredy Mgunda,Iringa
MKUU wa mkoa wa Iringa Amina
Masenza ameipongeza kampuni ya Asas ya mkoani Iringa kwa kufanya kazi ya
kusaidia kutatua changamoto za miundo mbinu na majengo katika maeneo ya taasisi
hata maeneo ambayo serikali imeshindwa kutekeleza.
Hayo yamesemwa wakati wa ziara
aliyofanya katika baadhi ya meneo ya mkoa huu,Masenza alisema kuwa kampuni ya
Asas imekuwa ikitolea kufanya kazi za wananchi na kusaidia kutatua kero za
wananchi pale inapopaswa kufanya hivyo.
“Iringa tuna kampuni nyingi ambazo
zinafanya biashara hapa lakini mchango wa kampuni ya Asas imekuwa ikijitoa sana
katika shughuli za kimaendeleo hivyo ni lazima niipongeze kwa kazi kubwa
inayofanya kutatua kero za wananchi na kutoa misaada mbalimbali” alisema
Masenza
Masenza alisema kuwa amefakiwa
kufanya ziara kwenye baadhi ya maeneo na amekutana na kazi zilizofanywa na
viongozi wa kampuni hii ya Asas mfano wa Iringa mjini Salim Asas amejitolea
mifuko mia mbili hivi karibu licha kuwa anafanya kazi nyingi za kimaendeleo
katika manispaa ya Iringa.
“Salim Asas amefanya mambo
makubwa sana hapa Iringa mfono kwa uchache tu amesaidia mambo mengi jeshi la
polisi,amesaidia sekta ya afya kwa kujenga baadhi ya mahodi katika hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Iringa,amekarabati majengo mengi hapa manispaa,mimi nasema
kuwa nitaendelea kumpongeza kwa kazi kubwa anaifanya hapa” alisema Masenza
Aidha Masenza alisema kuwa
alipokuwa kwenye ziara katika shule ya sekondari ya Ilambilole amekutana na
mchango wa ujenzi wa jingo la madarasa ambalo limejengwa na kampuni hiyo
kupitia mwenyekiti wa bodi wa shule hiyo ndugu Feisal Asas,lakini wamejenga
hodi katika kituo cha Afya cha kising’a ambacho kipo kata ya kising’a.
“Nichukue nafasi hii kumpongeza
Fesail Asas kwa kazi anayoifanya katika wilaya ya Iringa vijijini haina mfano
anafanya kazi kubwa sana na hayo ni maeneo machache tu bali amefanya kazi
katika maeneo mengi ambayo sisi kama serikali tulikuwa bado hatujafika” alisema
Masenza
Masenza alisema kuwa amalizia
na swala la ujenzi wa barabara ya kutoka kising’a kwenda Ilambilole kuna eneo
amelijenga na kusaidia wananchi kupita hata leo kwenye msafara wa ziara ya mkuu
wa mkoa gari zote zimepita kwenye barabara.
“Haya ndio ambayo nimejionea
mwenyewe kwenye ziara yangu hii fupi ambayo yamefanywa nah ii kampuni ya Asas
hivyo naomba wasituchoke waendelee kutusaidia kutatua changamoto pale
wanapoweza basi nasi serikali tutaendelea kutekeleza pale tunapotakiwa kutekeza
kutokana na miongozo yetu” alisema Masenza
Nichukue fursa kuiomba kampuni
hii iendelee kutusaidia kutatua kero ambazo wanaona zinafaida kwa jamii na sio
kwa mtu binafsi.
0 comments:
Post a Comment