Baadhi ya wachimbaji wa kijiji na kata ya Rwamgasa wakiendelea na kazi ya uchanjuaji wa madini ya dhahabu. |
Moja kati ya wamiliki wa mialo ya uchenjuaji wa madini ya dhahabu akionesha risti ambayo sio ya EFD ambayo wamekuwa wakipatiwa baada ya kununua kifaa cha kuzimia moto. |
Eneo la kuchenjulia dhahabu likiwa limefungwa na jeshi la zima moto na uokoaji. |
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Wilayani Geita,Barnabas Mapande akikagua moja kati ya mtungi wa kuzimia moto wakati alipofika kuzungumza na kusikiliza changamoto za wachimbaji. |
Kifaa cha kuzimia moto kikiwa kwenye eneo la kuchenjulia dhahabu. |
Na,Joel Maduka,Geita.
Chama cha
mapinduzi Wilayani Geita kimelaani kitendo cha jeshi la zima moto na uokoaji
kuwatoza gharama kubwa bila ya kuwapa
stakabadhi za serikali baadhi ya
wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye kijiji cha Lwamgasa huku wakifungiwa shughuli za uchenjuaji madini hayo kutokana na baadhi
yao kugoma kununua kifaa cha kuzimia moto.
Akizungumza
baada ya kufika kwenye machimbo hayo na kujionea namna ambavyo wachimbaji hao
wamefungiwa shughuli zao Katibu Mwenezi wa CCM Wilayani Humo Bw Jonatham
Masele,amesema CCM imesikitishwa na jeshi la zima moto kuwatoza Sh Lakini moja na elfu ishirini.
“Kiukweli
sisi kama chama tumesikitishwa sanaa na kitendo cha jeshi la zima moto kuuza
kwa bei kubwa bila ya kutoa risti mitungi hii ya gesi ya kuzimia moto na jambo
jingine kuwafungia watu shughuli zao bila ya kuwapa elimu jambo hili sio nzuri
tunaomba wajitahidi kuwaelimisha kwanza awa watu nasio kujichukulia hatua ya
kuwafungia”Alisema Masele.
Bw Lehamu
Lugiko , Mzee Mathew Kajoro na
Mwananyanzara Hamis wameelezea sababu kubwa ambayo imeendelea kuwapa mashaka
wachimbaji kuwa ni kuuziwa mitungi ya kuzimia moto bila ya kupewa Elimu ambayo
itawasaidia kupambana na majanga ya moto huku wakisikitishwa na kitendo cha
kufungiwa kwa shughuli zao.
Mkuu wa
Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani
Geita Bw Elisa Mgisha amesema wao sio wasambazaji kwani kuna watu ambao ni
mawakala na kwamba suala la risti za EFD inatokana na wafanyabiashara wenyewe
na kuhusu kuuziwa kwa bei kubwa ni kwamba wao wanapotoa kibari cha mawakala
yeye ndiye mwenye jukumu la kupanga bei ya kuuza mtungi vile ambavyo anaonelea.
Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Geita Bw Barnabas Mapande amemtaka mkuu wa jeshi la zima moto
kushughulikia tatizo hilo na kuacha kuendelea kuwakandamiza wananchi na wafanyabiashara
pindi wanapokuwa kwenye shughuli zao za kujitafutia kipato.
0 comments:
Post a Comment