Diwani wa Kata ya Kihesa Jully Sawani akiwa ametoka kuchukua mifuko miambili kutoka kwa MNEC Salim Asas kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Kihesa na hiyo ni baadhi tu ya mifuko ya safuri huku mingine ikiwa tayari imeshatangulia shuleni kuanza Nazi.
Mafundi wakiwa kazini kihakikisha jengo hilo linakamilika mapema ili lianze kufanya kazi na hiyo nayo ni kazi ya MNEC Salim Asas
Diwani wa Kata ya Kihesa Jully Sawani akiwa katika jengo linamaliziwa kwa ufadhili wa MNEC Salim Asas
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas ameanza mara moja kutekeleza ahadi zake alizowahidi wakazi wa kata ya Kihesa wakati wa kupokea hati ya diwani wa chama cha mapinduzi (CCM) wa kata hiyo Jully Sawani.
Mafundi wakiwa kazini kihakikisha jengo hilo linakamilika mapema ili lianze kufanya kazi na hiyo nayo ni kazi ya MNEC Salim Asas
Diwani wa Kata ya Kihesa Jully Sawani akiwa katika jengo linamaliziwa kwa ufadhili wa MNEC Salim Asas
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas ameanza mara moja kutekeleza ahadi zake alizowahidi wakazi wa kata ya Kihesa wakati wa kupokea hati ya diwani wa chama cha mapinduzi (CCM) wa kata hiyo Jully Sawani.
Akizungumza kwa niaba ya MNEC
huyo diwani wa kata ya Kihesa Sawani alisema kuwa toka siku ya jana wameanza
kufanya shughuli za kimaendeleo za wananchi kama ilivyokuwa ahadi yake na ya
MNEC
“Mwandishi ukiangalia hapa
unawaona mafundi wanaendeleoa na kazi hivyo najua baada ya muda mufupi kila
kitu kitakuwa kimemalizika na kuanza kutumika kwa faida ya wananchi wa kata ya
kihesa” alisema Sawani
Sawani alisema kuwa anamshukuru
MNEC Salim Asas kwa kutekeleza ahadi alizowahidi wakazi wa kihesa kwa kuwa
tayari ameshatoa mifuko mia mbili (200) ya saruji katika shule ya sekondari ya
Kihesa na tayari mafundi wapo kazini wameanza kumalizia ujenzi wa jengo la
biashara ambalo litaongeza ajira kwa wakazi wa kata ya Kihesa na nje ya kata hii.
“Hii unayina hapa ni saruji
ambayo imetolewa na Salim Asas na hapa pia unawaona mafundi wanaendelea na kazi
hivyo kazi hii inakwenda kwa kasi ili kutoa fusa ya ajira mapema iwezekanavyo na
kupuza jamii tegemezi” alisema Sawani
Sawani aliongeza kuwa kazi ya
kukarabati miundombinu ya barabara katika mtaa wa Mafifi unaendelea nao kwa
kufanya kazi karibu na wananchi wa eneo hilo na kuhakikisha kuwa wananchi
hawapati shida ya barabara katika kipindi hiki cha masika.
Hapo awali Akihutubia mamia ya
wananchi walijitokeza katika hafla hiyo ya kukadhiwa cheti cha kuwa diwani wa
kata hiyo Jully Sawani, MNEC Salim Asas alisema kuwa atatoa mifuko miambili ya
saruji kwa ajili ya kutatua kero hiyo ya ujenzi wa madarasa katika shule ya
sekondari Kihesa na kuahidi kuwa ataitembelea shule hiyo kujua changamoto
nyingine.
“Leo naanza kwa kutoa mifuko
miambili ya saruji lakini nitakuja hapo shule kujionea changamoto nyingine za
shule hiyo ili niweze kuzitatua kabisa na kuwaacha wananfunzi wakisoma kwa
uhuru kwa lengo la kukuza kizazi chenye elimu bora na kuja kusaidia taifa
katika kuleta maendeleo wote tunajua kuwa bila elimu huwezi kupata maendeleo
hivyo nitasaidia sana kwenye elimu” alisema Asas
Asas aliwakata viongozi wa kata
hiyo kuandaa bajeti ya kumalizia jingo hilo ambalo litaongeza ajira kwa
wananchi wa kata hiyo ambao kwa sasa hali zao za kiuchumi zimedolola hivyoa
atafanya linalowezekana kuhakikisha kuwa wananchi wa kata hiyo wanabadili na
kuacha kuishi kimazoea.
“kata ya Kihesa anayoijua yeye ni ile yenye
vijana wengi wasio na ajira ambao kwa bahati mbaya wamekuwa wakishughulishwa
kwenye siasa badala ya kuhamasishwa kufanya shughuli za maendeleo” Alisema Asas
Hivyo MNEC huyo ameshaanza kutekeleza ahadi zake kwa
kuonye kuwa anaendana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John
Pombe Magufuli ya hapa kazi tu na yeye ndio anafanya hivyo
0 comments:
Post a Comment