Thursday, January 18, 2018

KENANI KIHONGOSI KUFANYA KAZI NA MNEC SALIM ASAS KUNATUONGEZEA KASI YA KUKUZA CHAMA MKOANI IRINGA

Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa iringa Kenani Kihongosi akiwa na baadhi ya viongozi wa umoja huo wakiongea na waandishi wa habari juu ya kazi zinazofanywa na chama pamoja na MNEC wa mkoa wa Iringa
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama hicho Kenani Kihongosi akiwa mjumbe wa halmashuri kuu ya taifa ya chama hicho Salim Asas

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa umesema kuwa utaendelea kumuunga mkono juhudi za kimaendeleo zinazofanywa na mjumbe wa halmashuri kuu ya taifa ya chama hicho Salim Asas kwa kuwakikisha Iringa inakuwa kimaendeleo na kufikia kuwa hadhi ya kuwa jiji.

Akizungumza na blog hii mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama hicho Kenani Kihongosi alisema kuwa chama na mkoa wa Iringa umepata viongozi ambao wanania ya kuleta maendeloa kwa wanan na sio wapenda rushwa kama viongozi wengine.

“Huyu MNEC wetu bwana Asas anafanya kazi sana kwa wananchi wa mkoa wa iringa kwa kutoa misaada mbalimbali kwa ajili ya maendeleo na sio kitu kingine hivyo vijana wote tunatakiwa kumuunga mkono ili aendelee kujitolea kufanya kazi za kimaendeleo” alisema Kihongosi

Kihongosi alisema vijana wa mkoa wa Iringa wa UVCCM wanafuraha ya kufanya kazi na viongozi wote waliochaguliwa katika uchaguzi wa chama ulipita kuwa asilimia kubwa wote ni wapenda maendeleo hivyo kwa sasa kuna fursa za mkoa wa iringa kukua kimaendeleo kwa haraka na kasi kubwa.

“Mwaka huu tumepata viongozi ambao sio njaa njaa hivyo na kila mmjoa anakazi zake hivyo imekuwa rahisi hata kuchangia shughuri za chama kuhakikisha kitekeleza kazi zake na kuongeza wanachama wapya” alisema Kihongosi

Aidha Kihongosi alisema Asas amekuwa akitekeleza ahadi kwa wakati mfano toka siku ya juzi wameanza kufanya shughuli za kimaendeleo za wananchi kama ilivyokuwa ahadi yake na ya MNEC

“Mwandishi ukiangalia hapa unawaona mafundi wanaendeleoa na kazi hivyo najua baada ya muda mufupi kila kitu kitakuwa kimemalizika na kuanza kutumika kwa faida ya wananchi wa kata ya kihesa” alisema Kihongosi

Kihongosi alisema kuwa anamshukuru MNEC Salim Asas kwa kutekeleza ahadi alizowahidi wakazi wa kihesa kwa kuwa tayari ameshatoa mifuko mia mbili (200) ya saruji katika shule ya sekondari ya Kihesa na tayari mafundi wapo kazini wameanza kumalizia ujenzi wa jengo la biashara ambalo litaongeza ajira kwa wakazi wa kata ya Kihesa na nje ya kata hii.

“Hii unayina hapa ni saruji ambayo imetolewa na Salim Asas na hapa pia unawaona mafundi wanaendelea na kazi hivyo kazi hii inakwenda kwa kasi ili kutoa fusa ya ajira mapema iwezekanavyo na kupuza jamii tegemezi” alisema Kihongosi

Wakati huo huo mwenyekiti huyo ametoa tamko juu ya kuchomewa nyumba kwa katibu wa vijana wilaya ya Iringa amesema kuwa umoja wao unalaani tukio hilo kwa kuwa limeleta hofu kwa wakazi wa mkoa wa iringa.

Kihongosi ameeleza kuwa matukio hayo hayakubaliki katika jamii kwa kuwa yanatoa tafsiri mbaya hasa katika siasa za mkoa wa iringa

Katika hatua nyingine ameliomba jeshi la polisi kuwachukulia hatua za kisheria wale wote ambao wamehusika na tukio hilo.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More