Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki kuchimba msingi kwenye kituo cha afya cha Masumbwe Wilayani Mbongwe. |
Wananchi wakishiriki kwenye ujenzi wa msingi kwenye kituo cha afya cha Masumbwe Wilayani Mbongwe. |
Mkuu wa Wilaya ya Mbongwe ,Mathar Mkupasi akizungumza na wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kuunga mkono jitihada za serikali za ujenzi wa jengo la kupasulia kwenye kituo cha afya cha Masumbwe. |
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM,Wilayani Mbongwe Johari Juma akisisitiza wanachama wa chama hicho kuwa mstari wa mbele kushiriki katika shughuli za maendeleo. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza namna serikali ilivyojipanga kupunguza changamoto ya huduma za afya Mkoani humo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mbongwe. |
Na,Joel Maduka,Geita.
Jumla ya Sh
Bilioni 3 zilizotolewa na serikali Mkoani Geita zinatarajiwa kuboresha
miundombinu katika Vituo saba vya afya .
Mganga mkuu
wa Mkoa wa Geita Dr Japhet Simeo alisema lengo
kuu la hizo fedha ni kuboresha miundo
mbinu kwa maana ya chumba cha upasuaji kujenga wodi ya watoto,wakina mama ,maabara
na chumba cha kuhifadhia maiti na kwamba wanatarajia kuona fedha hizo zinafanyika
kuboresha mandhari ya kituo kwa maana ya bustani na majengo ambayo yamechakaa.
Simeo
alizitaja wilaya ambazo zimepatiwa fedha hizo ni wilaya 5 ikiwemo halmashauri ya wilaya ya Geita ambayo imepewa kiasi cha sh ,Milioni 500
kwenye kituo cha afya cha Nzera na
kwamba hadi sasa wameshajenga majengo
manne ambayo yamekaribia kukamilika , Mbogwe milioni 800 ambazo zimegawa kwenye
vituo viwili vya afya, Bukombe milioni
400 kwaajili ya kituo cha afya cha uyovu , Chato wamepatiwa fedha kwaajili ya vituo viwili
ambvyo ni Bwanga Milioni 500 na Karumwa milioni 400 na Wilaya ya Nyang’hale
milioni 400 kwaajili ya kituo cha afya cha Nyang’hale.
Juma Mabura ni
moja kati ya wananchi wa Wilaya ya Mbongwe ambapo ameelezea kuwa kumekuwape na
changamoto kubwa ya upungufu wa majengo na kwamba kukamilika kwa baadhi ya
majengo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma ya afya.
Mkuu wa Mkoa
wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi amesema kuwa majengo yaliyo kwenye hatua ya
renta na maboma yakikamilika watakuwa kwenye asilimia 55 kwa maana ya zahanati
262 na kwamba nyingine wameanza ujenzi .
Aidha
amesisitiza kuwa lengo la serikali ni kuondoa kero ya kimiundombinu kwenye
sekta ya afya ili kuwawezesha watanzania kupata huduma bora za afya.
0 comments:
Post a Comment